Mliofanikiwa kuacha kazi na kujiajiri mlitumia mbinu gani?

Labda uvivu tu wa kutowafatilia vijana.
Ukiacha kazi ukaisimamia mwenyewe biashara bado utawahitaji vijana tu wa kukusaidia eidha usipokuwepo au wa kukusaidia ukilemewa.

Cha kufanya mi nakushauri usiache kazi, bado unaweza kupiga hatua ukiwa hukohuko kazini. Ni vile unalea vijana wanaokupa hasara. Labda una huruma sana mkuu, hesabu ni njia nzuri ya kumkamata mwizi kwenye biashara.

Inawezekana wewe ni moja ya wafanyabiashara "wakabia macho" yaani yeye akifika dukani anaangalia shelf kama lina vitu basi roho kwatu anajua biashara iko safi.
Hufanyi stock, unaenda kuwapokea vijana ukitoka job bila makabidhiano ya hesabu yoyote zaidi ya fedha tu.
Hapo hata kama vijana sio wezi ila unawatamanisha waibe, na wataiba kweli.
 
The world is not fair.....wakati wengine tuko benchi miaka Saba wewe unawaza kuacha kazi[emoji24][emoji24]
 
Labda uandike barua kwa mkurugenzi ukiomba rikizo ya mwaka bila ya kulipwa mshahara,ruhusa hii ipo kwa wafanyakazi wa serikalini hasahasa walimu
Nakazia ✍️✍️
Baada ya mwaka atapata jibu sahihi kutokana na performance ya biashara yake
 
Sasa mtu kakuibia 1.5 m unajua nyuma aliiba ngapi[emoji848] kamata weka ndani huyo mtu akili imkae sawa....., Halafu kwa biashara kama hyo tayari ni kubwa mbn kuna app nyingi za kucontrol biashara
 
Sio wote wamefanikiwa kuwa na biashara
Lazima ujue ya kuwa kama umefikia hatua ya kuwa na biashara tena aina tofauti, basi umefika pazuri sana na utaendelea zaidi

Kuhusu kazi yako hiyo huna ulazima nayo ila ni uoga wako tu
Usichanganye biashara na kazi unless una partners wenye shares sawa na wewe

Lakini kama ni zako basi acha kazi enedelea kuza biashara zako na ukizisimamia vizuri utaendelea sana kwa moyo mmoja na mtangulize Mungu sana na umuombe sana na kama humuamini basi hata mizimu yenu sawa tu

Hakuna aliefika mahali bali bahati tu na jitihada zake
Ukiacha kazi unaweza kuongeza biashara ambazo utazimudu kuzisimamia kila siku

Nakuombea mafanikio mema
Na kama una ndugu ambao unajua wanakuhitaji kila mwezi na wanaweza kujituma basi wape kazi upate Baraka zao
 
Biashara zina nyakati, sio kila siku zitafanana.

Kuna mtu alikuwa na biashara ya vyakula kubwa sana hadi kuna wakati alivamiwa kutokana na hesabu kubwa aliyokuwa anafunga kwa siku.

Ilitokea ya kutokea lile eneo likavunjwa kwa ajiri ya kupisha ujenzi wa barabara.

Alihamisha biashara yake sehemu tofauti kidogo na pale na hakuweza tena kupata hesabu hata nusu ya aliyokuwa anapata.

Huo ni mfaano tu ni sawa na ununue bajaj alafu iibiwe ikavunjwe vunjwe huko.

Tafuta vijana waaminifu pia funga camera zitasaidia kuweka umakini lkn pia waambie ukweli na uwaambie wakishindwa kuwa waaminifu hutaweza kuendelea nao.
 
Asante mkuu,Kuna muda najiona bwege sana honestly,kiuhalisia Pato langu la biashara ni mara Tano ya mshahara lkn hofu IPO juu balaa
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
100%,Biashara huwa ina sifa moja kubwa ya kuwa kigeugeu,watu wengi wasio na experience ya biashara hawawezi kujua hili.
 
Unawaza nini omba likizo isiyo na malipo ya mwaka mmoja (zingizia chochote huko kazini) komaa hapo then baada ya mwaka utakuwa umepata jibu mujarabuu kabisa uendelee na kazi au ufanye biashara..
 
Tafuta namna nzr ila usiache kazi!! Ni Bora upunguze idadi ya wasimamizi hasa vijana wa3 ukabaki na mmoja unayemuona ana akili na uaminifu ndo muwe mnasaidiana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…