Mliofanikiwa kuacha kazi na kujiajiri mlitumia mbinu gani?

Labda uandike barua kwa mkurugenzi ukiomba rikizo ya mwaka bila ya kulipwa mshahara,ruhusa hii ipo kwa wafanyakazi wa serikalini hasahasa walimu
Ajichanganye Sasa aone.... Siku hizi kanuni za utumishi zinamuelekeza muajiri KUKURUDISHA IWAPO TU KUNA UHITAJI/ULAZIMA ... Unaweza kukaa benchi mpaka ukome...
 
Sijui wewe unasimiaje ila hakikisha hao vijana watatu uliowaeka hapo mmoja wapo awe kiongoz wawote hi itakusaidia kupata mtu wa kudeal nae pale unapoona mambo hayaend sawa sikushaur uache kaz au ufunge biashara . Nashndwa kuandka sana unaeza ni dm nikuelekeze mana nina kauzoefu kdgo
 
Bro kabla hujaacha kazi hakikisha una Mali zinazokuingizia pesa hata ukiwa umelala, Jenga nyumba maeneo ya mjini hata 4 tu pangisha ule Kodi kila mwez, huku unaendeleza biashara zako , ukifika hiyo hatua unaweza kuacha kazi,
Biashara ikiyumba unaingia bank unaweka rehan nyumba moja maisha yanaendelea [emoji23][emoji23] hivyo ndivyo wajasirimali wanavyoishi mjin
 
Pole sana kwa changamoto zinazokukabili

Usiache kazi sababu unachokipata ulikitoa huko kwenye ajira .

Kuhusu biashara ndugu zingatia maslahi mazuri kwa wafanyakazi wako alafu ongeza usimamizi madhubuti .

Tafuta wafanyakazi walio na elimu ya kawaida kidogo ila walio na future mbeleni usisahau kuwa na hofu na Mungu wao huwezi juta sana .

Vijana waaminifu wapo shida mnabeba yeyote kutokana na shida zake za muda huo bila kuwaza yeye anajiona wapi na anataka kuwa wapi muda huo maana ni kweli ndoto ya mtu moyoni inaweza kumdrive kufanya lolote ila ukimjua ni kheri umpe maslahi yaliyo na njia thabiti kuzielekea ndoto zake
 
Biasahara mzee ni risk na haina security kama ilivyo kwenye ajira., ukiamua kuwa mfanyabiashara lazima uwe risk taker.
Inatakiwa uisikilize kwanza nafsi yako kabla hujapata ushauli wetu, kisha unakuja kulinganisha ushauri wetu na mtazamo wako. Kwa upande wangu nakushauli piga chini kazi an take risk ili uwe na mda mzuri wa kupambana zaidi.
 
Kama unafanya kazi serikalini, Usithubutu kuacha kazi. Baada ya Samia anaweza kuja mvurugaji akaua uchumi. Ni Bora ubadili biashara utafute unayoweza kuifanya bila usimamizi wako wa moja kwa moja.
Biashara zote zinahitajj usimamizi madhubuti..kuacha biashara inayokuingizia faida ili ubadir kwangu sio salama pia..Kama ....ukiwa na fikra za uoga namna hii biashara huwezi fanyaaa
 
Naunga mkono hojaa
 
Kiukweli siwaelewagi watu wa Hivi ...yaaan unaacha biashara yako yenye faida kwa ajiri ya serkal kisa security 🤣🤣 ndomana ngumu sana kukuta muajiriwa tajiri
 
Ukiwa muajiriwa fanya biashara ya vitu vinavyohesabika kiurahisi ili ussimamie kwa urahisi
 
Mkuu uko dm unakwendwa kumtumia voice notes??
 
Mshika mawili moja humponyoka, chagua kile ambacho moyo wako unakuwa na amani ufanyapo, usisahau kumtanguliza Mungu.
 
Mimi nina experience na kazi lakini nashukuru nina experience na mazingira ama maisha mtu apitiayo wakati ameacha kazi. Nilikuwa Mwalimu kwenye shule moja hivi, baada ya kutokea recession pale shule, uongozi ukawa disseminated mambo yakaenda mrama.

Basi,nikajitungua tuu kwenda mtaani, nimeziona fursa nyingi sana ambazo zikanifanya nijutie kwanini siku save mkwanja wa kutosha ili nije kuzi execute mtaani.

In short mtaa unahitaji maamuzi na kujiamini, unapaswa kuwa na akili tofauti ila msimamo mmoja tu. Kwa sasa hivi nina wakati mgumu sana, ila si kwamba najuta kuacha kazi.Ila najuta kwanini, sikuwa nazifahamu hizi fursa mapema na kuziwekea mkwanja. Kama umeajiriwa as Mwalimu, demand ya walimu sio kwamba mwisho wake ni kwako, kama una biashara zako tayari unaweza ku focus huko mpaka zinatapoanza kujiendesha zenyewe, ukaja kurudi darasani kula vumbi baadae. najua ni uoga tuu kwa sasa, ingawa kubadili mazoea napo ni kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…