Hii thread inataiwa ipestiwe kwenye magroup ya whatsapp ili watu ambao bado hawajajiunga, waweze kujua kile kinachoendelea huko mtaani.
Kwani binafsi nnakumbuka, kuwa nliambiwa nisiwaambie watu hadi pale ntakapo kuwa nshajiunga.
Kilicho niacha bumbuwazi, pale mmoja wa presenter aliponambia kuwa, hii sio biashara ya kila mtu. Ni kwa ajili ya watu wachache ambao, ndio maana aliyenialika aliamua kunipendelea ili na mimi niweze kufanikiwa kama yeye, ndio maana akaamua kunialika, hivyo nisiichezee hiyo bahati, pia natakiwa kumheshimu sana business partner aliyenialika kwani amenionyesha ulipo utajiri uliokusudiwa kwangu mara baada ya kuzaliwa. Nisiiache hiyo bahati inipite.
Akanambia,
Hii biashara ingekuwa ni kwa ajili ya kila mtu,
Basi hapo nje pangekuwa hapatoshi kwa mafuriko ya watu
Wanaotaka/gombania kujiunga. Ila wameifanya special isiwe kwa kila mtu
Ili utakapofanikiwa na wengine wakakuona mtaani, waweze kukuuliza wao wenyewe, na wala sio wewe tena kwenda kuwatangazia biashara.
Binafsi tena kimoyo moyo,
Nkawa najisemesha, hayo mafuriko ya watu anayozungumzia kuwa
Hapo nje pangekuwepo na rundo la watu wanaotaka kujiunga kama hii biashara ingekuwa ni fursa kwa kila mtu, nkajiuliza
“Kwa usawa huu wa Magu, ni nani ambaye yuko tayari kwenda ku risk 5m yake kwenye Deci”
kwanza upatikanaji wake tu ulivyo mbilinge.
Huwezi amini,
Ukiwa QNET au AIM GLOBAL, unashawishiwa hadi kuuza
Nyumba,kiwanja,gari au chochote cha thamani
Ulichonacho huku wakiku laghai kuwa ndani ya miezi3, hela yako inakuwa imerudi na kutengeneza rundo la utajiri.
Jamani,
No easy money.
Tujitume, tufanye kazi.
NB; biashara ya PONZI SCHEME kama ni mpya na ndo kwanza imeingia nchini, jaribu ku risk, kwani wale wa mwanzo, uwezekano wa kupiga hela ni mkubwa kama mtaweza kuitangaza vizuri biashara yenu.
Kuna moja iliwahi kunitoa,
Ilipo ingia, nkagundua kuwa ndio kwanza tuko watu 15 tu kwa TZ,
nkapiga mpunga 56m,
Wakati nlichokuwa nmeinvest ilikuwa ni 1.8m
Hutoweza ku feel utajiri kwani hela yenyewe inakuwa inaingia
Gradually. Na wewe huku ukiwa na mahitaji ya kila siku.