Mliofanikiwa kwenye Network Marketing tunawaomba mtoe Ushuhuda hapa

njoo oriflame madam kampuni ya urembo asilia unajiungakwa 10,000 elfu kumi unaamua mwenyewe kama umejiunga kwa biashara au matumiz binafsi kampuni yetu inashika nafasi ya 2 kwa ubora wa bidhaa dunian.its made from sweden,inspired by natural of beauty

Oyaaa .. naona na wewe umeanza sasa? Nafasi ya 2 kwa ubora wa kitu gani sana?
 
Wakala [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hii thread inataiwa ipestiwe kwenye magroup ya whatsapp ili watu ambao bado hawajajiunga, waweze kujua kile kinachoendelea huko mtaani.

Kwani binafsi nnakumbuka, kuwa nliambiwa nisiwaambie watu hadi pale ntakapo kuwa nshajiunga.

Kilicho niacha bumbuwazi, pale mmoja wa presenter aliponambia kuwa, hii sio biashara ya kila mtu. Ni kwa ajili ya watu wachache ambao, ndio maana aliyenialika aliamua kunipendelea ili na mimi niweze kufanikiwa kama yeye, ndio maana akaamua kunialika, hivyo nisiichezee hiyo bahati, pia natakiwa kumheshimu sana business partner aliyenialika kwani amenionyesha ulipo utajiri uliokusudiwa kwangu mara baada ya kuzaliwa. Nisiiache hiyo bahati inipite.

Akanambia,
Hii biashara ingekuwa ni kwa ajili ya kila mtu,
Basi hapo nje pangekuwa hapatoshi kwa mafuriko ya watu
Wanaotaka/gombania kujiunga. Ila wameifanya special isiwe kwa kila mtu
Ili utakapofanikiwa na wengine wakakuona mtaani, waweze kukuuliza wao wenyewe, na wala sio wewe tena kwenda kuwatangazia biashara.

Binafsi tena kimoyo moyo,
Nkawa najisemesha, hayo mafuriko ya watu anayozungumzia kuwa
Hapo nje pangekuwepo na rundo la watu wanaotaka kujiunga kama hii biashara ingekuwa ni fursa kwa kila mtu, nkajiuliza

“Kwa usawa huu wa Magu, ni nani ambaye yuko tayari kwenda ku risk 5m yake kwenye Deci”
kwanza upatikanaji wake tu ulivyo mbilinge.

Huwezi amini,
Ukiwa QNET au AIM GLOBAL, unashawishiwa hadi kuuza
Nyumba,kiwanja,gari au chochote cha thamani
Ulichonacho huku wakiku laghai kuwa ndani ya miezi3, hela yako inakuwa imerudi na kutengeneza rundo la utajiri.

Jamani,
No easy money.
Tujitume, tufanye kazi.

NB; biashara ya PONZI SCHEME kama ni mpya na ndo kwanza imeingia nchini, jaribu ku risk, kwani wale wa mwanzo, uwezekano wa kupiga hela ni mkubwa kama mtaweza kuitangaza vizuri biashara yenu.

Kuna moja iliwahi kunitoa,
Ilipo ingia, nkagundua kuwa ndio kwanza tuko watu 15 tu kwa TZ,
nkapiga mpunga 56m,
Wakati nlichokuwa nmeinvest ilikuwa ni 1.8m
Hutoweza ku feel utajiri kwani hela yenyewe inakuwa inaingia
Gradually. Na wewe huku ukiwa na mahitaji ya kila siku.
 
hiyo biashara ni ngumu sana, kwa mfano hao q net hawauzi bidhaa kiuhalisia, hizo bidhaa ni geresha/fictious ili kuwafumba watu, au kupewa kibali. Wao wanacheza upatu, huwezi kumuuzia mtu mkufu au saa ya elfu hamsini kwa milioni 5
 
[emoji23] [emoji23] balaa
 
Hivi hyo milion 5 si afadhali tu uwe unalipia SIGNAL FOREX upge pesa japo sio hzo nying kama za Q-NET maana ukiwa na $45 tu unalipia Premium signals ambazo wewe kazi yako inakuwa na kuweka tu pair wala sio tena ufanye technical analysis. tena unaweza ukajikuta 1m tu inakutosha na hzo 4 ukafanyie ata mambo mengine. KWELI WATU WANAPESA ZA KUCHEZEA.
[
 
Forever living wana PRODUCTS so kidogo ukiwa mchapa kazi utafanikiwa kwa hle small commision but Q-NET hakuna product ukishatapeliwa na wewe tafuta wawili wa kuwatapeli ili sijui ubalance ndio upate $200 apprx 500,000. FOOLISH BUSINESS, ila forever products zao ni ghali tu but ni nzuri alaf inaitaji watu wenye Skills za marketing at least wanaweza wakafanikiwa
 
This is a business of trust, ndio maana ukijoin tu unambiea fasta umuingize mke/mume/ baba/mama. Those people ambao wanakuamini, that is to say, in this business, TRUST ndio msingi mkubwa wa business plan yao.vingine vyote mbwembwe tu.yaani huku mwanamke anaweza hata kukuvulia chupi umgegede ilimradi tu skushawishi ujoin chini yake, hahahaaa.
 
Yaani ukampa mkwanja akaenda kujiunga, alafu baadae akakutema ya kuwa hupendi maendeleo yake??
 
njoo oriflame madam kampuni ya urembo asilia unajiungakwa 10,000 elfu kumi unaamua mwenyewe kama umejiunga kwa biashara au matumiz binafsi kampuni yetu inashika nafasi ya 2 kwa ubora wa bidhaa dunian.its made from sweden,inspired by natural of beauty
Nafasi ya kwanza inashikwa na kampuni gani?
 
Yaani ukampa mkwanja akaenda kujiunga, alafu baadae akakutema ya kuwa hupendi maendeleo yake??
iyo hela ya kumpa mwanzo hakusema kama ni biashara iyo, pale nilipo enda kwake namkuta na vimifuko flani ya global alliance ndo kumwambia iyo mambo si mambo aachane nayo ile naondoka nikasindikizwa na msg hawezi kuwa na mtu anaye katisha tamaa na asiye taka maendeleo ya mwenzake
 
speechless😎
 
Unajiunga kwa 10k. Then unaanza kuuza bidhaa Kama za skin care, weight loss, perfume etc wanakupa guiding sheet ya selling price. Pia you can add people and get paid.
Another umachinga but komaa ata Harmonize na Diamond walianza mdogo mdog kwa kutembeza bidhaa now wapo ndani ya Lamborghini
 
Haka kajaama nimecheka sana ,kana hamasisha watu Facebook,wajiunhe na hizo PYRAMID SCHEME/MARKETING.
kucheki Profile lake daaah [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wakenya bhana
 
Kuna mtu mimi namfahamu aliuza gari yake na kujiunga QNET, ana zaidi ya mwaka sasa hajapata hata mtu mmoja wa kumuunganisha anajutia tu sasaivi.
Hao jamaa ni matapeli aisee. Mimi kuna ndugu yangu alinialika kwenye izo presentation zao, nikamwambia hiyo pesa milioni tano hata mkinikopesha siitaji kujiunga na huu upuuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…