Mliofanikiwa kwenye Network Marketing tunawaomba mtoe Ushuhuda hapa

Mliofanikiwa kwenye Network Marketing tunawaomba mtoe Ushuhuda hapa

Good morning!!(changa la macho la kwanza)
Ukipigwa hiyo salamu unawehushwa kwanza jeshini tunasema wiki sita za kutolewa uraia kuingizwa jeshini pili unapigwa speech kali wakimrefer Bill Gates na kitabi cha poor dad rich dad cha kiyosaki cjui ukimalizwa hapo unapewa mda uje presentation ya pili hiyo ucipoenda hata home kwako watakutimbia utaonyeshwa kitabu kina saa mikufu na vifaa vingne vya nyumbani unaambiwa bei ya chini ni dola 2000 cjui saa ya golden rose limited edisheni(edition) ***** zao ukiwa naela ukiweka umeumia ukisema sina unapigwa sound uza hata kiwanja within one year utapiga pesa ndefu unaweza nunua nyumba posta kundindiku so usijali hako kakiwanja mda huo washaidharaulisha ajira yako yaan unalipwa laki saba kazi ilivyongumu ile achana nayo anatoa mfano wa.kisenge nlikuwa mhasibu anakitajia likampuni nlikuwa nalipwa milioni 2 ila nimeacha kazi baada ya hapa qnet kufanya vzr maisha yangu duuuh usipoingia kama mm ww ni Genius
 
Kuna mmoja wa Uganda alinitumia friend request FB nilipoaccept chini ya Dk moja naona txt messenger akaanza txt za kawaida kusalimiana ghafla akaja na huu mzigo

Now i want you to go to the offices of Alliance in motion Global in TZ located on number 477 Mwai Kibaki Road Mikocheni, Infront of KFC Restaurant, Daressalaam and meet one of the Country Manager called Mr Edmund Rula this is his number he is a filipino +255784025630 ok tell him that Emesu Justine from Uganda has sent me to you so that you help me to attand a program called Opportunity Presentation Plan(OPP) which starts at around 10:30am ok after that i want to register you names under my names Justine Emesu ID Number UG 153796 and we start to make alot of money online and offline ok remember it is all about trust ok i am doing Alliance in motion Global it pays up to 5480 dollars everyday ok you can check on our website www.allianceinmotion.com for more information ok.

Sikumjibu mpk leo
Oooh Jeief itabaki kuwa juu, I was about kuingizwa kingi na rafiki yangu mfilipino tulikutana humu mitandaoni akaanza kunipa sound hz ananirushia watu wa Uganda matajiri waliotoka thro AIM global [emoji23] [emoji23] picha linaanza wakanialika semina kule mikocheni nikaenda kuona watachozungumza aise wako vzur kwenye ushawishi yani wale madogo ma motivation speaker sijui walisomea wapi unaweza acha kazi ukaanze biashara ile ,wamepiga suti wako kisharobalo unaweza sema pesa iko hapa [emoji23] [emoji23] ila nilipoangalia type ya washiriki kuna kitu kikagonga kichwani yani wameweka mapandikizi wa kushangilia na kutoa ushuhuda nikajua this is another Deci.
 
mi kuna mrembo mmoja matata sana alinitumia email, sikuwa namjua na sijui hata email yangu alipata wapi, tukakutana pale Holiday inn mida ya mchana akiwa na mkaka mmoja hivi. Wakaniwekea kikao nikawaza hapo leo kuna dili kubwa sana. Yule dada English nyiingi na mavitabu yenye picha nzuri nzuri tu. Sikuhamasika. Mwishowe akawasha laptop kanionyesha mapicha picha ya waliofanikiwa, wengine wako na magari mazuri, wengine na mijengo ya ajabu ajabu naona ananitolea fomu eti nijaze niweke na mtaji wa kuanzia laki 2 within one weeke nitaona mrejesho wake. mwishowe nikamwambia Ahsante sana dada tutawasiliana kwa njia ya email. Hadi leo asee. Siku namuona anapanda daladala ya Mbezi tena saa tisa mchana pale posta, nadhani mmenielewa
 
Good morning!!(changa la macho la kwanza)
Ukipigwa hiyo salamu unawehushwa kwanza jeshini tunasema wiki sita za kutolewa uraia kuingizwa jeshini pili unapigwa speech kali wakimrefer Bill Gates na kitabi cha poor dad rich dad cha kiyosaki cjui ukimalizwa hapo unapewa mda uje presentation ya pili hiyo ucipoenda hata home kwako watakutimbia utaonyeshwa kitabu kina saa mikufu na vifaa vingne vya nyumbani unaambiwa bei ya chini ni dola 2000 cjui saa ya golden rose limited edisheni(edition) ***** zao ukiwa naela ukiweka umeumia ukisema sina unapigwa sound uza hata kiwanja within one year utapiga pesa ndefu unaweza nunua nyumba posta kundindiku so usijali hako kakiwanja mda huo washaidharaulisha ajira yako yaan unalipwa laki saba kazi ilivyongumu ile achana nayo anatoa mfano wa.kisenge nlikuwa mhasibu anakitajia likampuni nlikuwa nalipwa milioni 2 ila nimeacha kazi baada ya hapa qnet kufanya vzr maisha yangu duuuh usipoingia kama mm ww ni Genius
😂😂😂😂Bora TATUMZUKA na BIKO
 
Mimi mdada aliyekuja kunipanga nijunge nao aliniambia wanaimiliki timu ya man city... Nikamuuliza unaijua hata timu yenyewe na unamfahamu shehe Mansoor alibaki kutoa macho nikamfukuza.
hahahahahaha wee jamaa nux sana
 
Kuna mmoja wa Uganda alinitumia friend request FB nilipoaccept chini ya Dk moja naona txt messenger akaanza txt za kawaida kusalimiana ghafla akaja na huu mzigo

Now i want you to go to the offices of Alliance in motion Global in TZ located on number 477 Mwai Kibaki Road Mikocheni, Infront of KFC Restaurant, Daressalaam and meet one of the Country Manager called Mr Edmund Rula this is his number he is a filipino +255784025630 ok tell him that Emesu Justine from Uganda has sent me to you so that you help me to attand a program called Opportunity Presentation Plan(OPP) which starts at around 10:30am ok after that i want to register you names under my names Justine Emesu ID Number UG 153796 and we start to make alot of money online and offline ok remember it is all about trust ok i am doing Alliance in motion Global it pays up to 5480 dollars everyday ok you can check on our website www.allianceinmotion.com for more information ok.

Sikumjibu mpk leo
Ukiwa wakuja lazima wakuokote mkuu
 
mi kuna mrembo mmoja matata sana alinitumia email, sikuwa namjua na sijui hata email yangu alipata wapi, tukakutana pale Holiday inn mida ya mchana akiwa na mkaka mmoja hivi. Wakaniwekea kikao nikawaza hapo leo kuna dili kubwa sana. Yule dada English nyiingi na mavitabu yenye picha nzuri nzuri tu. Sikuhamasika. Mwishowe akawasha laptop kanionyesha mapicha picha ya waliofanikiwa, wengine wako na magari mazuri, wengine na mijengo ya ajabu ajabu naona ananitolea fomu eti nijaze niweke na mtaji wa kuanzia laki 2 within one weeke nitaona mrejesho wake. mwishowe nikamwambia Ahsante sana dada tutawasiliana kwa njia ya email. Hadi leo asee. Siku namuona anapanda daladala ya Mbezi tena saa tisa mchana pale posta, nadhani mmenielewa
😂😂😂😂Pengine hakupata kitu chochote tumboni tangu asubuhi.
 
Wakuu,
Mwishoni mwa mwaka jana Mdogo wangu (Mwanafunzi wa chuo Kikuu Ardhi) alinitumia ujumbe Uliosomeka " Bruv! Nimepata platform ya kupiga pesa, Sure am telling you bruv am gonna be a great millionaire in just few coming days". Nikamuuliza, "Vipi umepata dili la kuwa Contena?(kwa maana ya Msafirishaji wa madawa ya kulevya)" .......Akanijibu "Bruv i just need you to lend me 560k Tshs nimepata nafasi ya kuwa milionea kwa kutengeneza pesa na Kampuni moja ya Kifilipino inaitwa Alliance In Motion Global after one year hata wewe nitakuwa nakupumulia kisogoni". I was shocked kivipi laki tano na sitini izae mamiloni ndani ya mwaka mmoja!! Nilimuuliza dogo iwapo amefanya utafiti wa kutosha juu ya hiyo anayooita "platform" na kunijibu kuwa ameshafanya na anawajua watu wengi waliotusua kupitia hiyo Alliance.

Binafsi nampenda sana mdogo wangu, Sikutaka afikirie kuwa namnyima nafasi ya kutekeleza,adhma yake (Japo nilikuwa na wasiwasi) niliamua Kumtumia Sh. Laki 7 ili akifanya hayo mambo yake abaki na balance ya kutumia kwa muda (ili tusisumbuane tena).....Now ni mwezi wa 6 huu unaelekea wa 7 tangu ajiunge sioni mabadiliko yoyote, mara ananiambia "Bruv, Haya mambo hayataki haraka pesa ipo inakuja". Mara, "oh! natengeneza Pair ya watu wangu ili nianze kulipwa".....Kuanzia hapo nikajua tu kuwa mdogo wangu alipotea njia kwa kufuata mkumbo na kukubali kuingizwa mkenge coz mpaka sasa hazipiti wiki mbili bila kuniomba pesa za,matumizi.

Siku moja tena ya Mwezi February kuna dada alinifuata ofisini akataka tuongee ili anishirikishe busness yao alijitambulisha kwa A.k.A ya Cherry...nilimpomkubalia akaniambia kuwa anafanya kazi na kampuni ya QNET na kuna mtu alim'direct kwangu (alisita kumtaja) ndipo akaanza kutoa "Likitabu" lake lina picha za simu, saa, mikufu nk. Kwa ufupi tu ni kwamba alinieleza kuwa kwa kiasi cha kuanzia dola 2000 kwa maana ya Shilingi milioni tano pekee naweza kununua bidhaa moja kama vile saa au mkufu na nikishirikisha wenzangu wengine nitaanza kulipwa pesa...Niliposikia hivyo nilimwangalia yule dada nikamwambia kwa ufupi ".Sista nipo busy sana kwa sasa na pia siwezi kufanya hiyo biashara yako am so sorry".aliondoka akiwa na mfadhaiko usoni mimi sikujali coz Niligundua kuwa hawana tofauti na wale Alliance waliomtapeli mdogo wangu miezi kadhaa iliyopita.

Nyie watu Wa Hayo makampuni tajwa hapo Juu na ninyi mliofanikiwa kupitia haya makampuni (kama mpo humu) hebu jitokezeni mtujuze mlitumia njia gani..otherwise i declare you kama Matapeli mliofumbiwa macho na Serikali.
njoo oriflame madam kampuni ya urembo asilia unajiungakwa 10,000 elfu kumi unaamua mwenyewe kama umejiunga kwa biashara au matumiz binafsi kampuni yetu inashika nafasi ya 2 kwa ubora wa bidhaa dunian.its made from sweden,inspired by natural of beauty
 
Nilishawahi kujiunga Forever Living wakati nikiwa chuoni, mwaka 2009 nakumbuka, nilipewa mapromise ya kufa mtu. Niliifanya ile kazi kwa mda wa mwaka mmoja hivi ila kiukweli nilikuwa napata pesa za kawaida sana, unakuta zile bonus za mwezi ni kama laki moja au laki mbili, japo nilikuwa nasikia wale waliotutangulia wanapiga pesa sana mpaka milioni 200!!
Kimsingi nilishindwa kuendelea maana natumia efforts kubwa sana kufanya marketing ya bidhaa zao na malipo ni ya kawaida tu.
 
komenti zenu zinanipa raha sana, niliachana na mpz kisa haya mambo nimempa mkwanja kapeleka huko. siku natimba kwake nakuta mifuko mi 3 ya global alliance akaanza stori za kuwa bilionea nikamwambia unaibiwa rafiki yangu stori ikaishia hapo
naondoka nyuma ikafata msg mahusiano yameisha maana staki maendeleo yake na hawezi ambatana na mtu mtu mwenye kukatisha tamaa.

baada ya miezi 3 ananiomba buku 10 ya kula nikampa mara eeeh ikawa kila siku nikamkumbusha yeye ni mfanyabiashara mkubwa akachukia.

kifupi alisha pigwa maana naona sasa ana njaa kali kuliko mwanzo
 
Back
Top Bottom