Mliofanikiwa kwenye Network Marketing tunawaomba mtoe Ushuhuda hapa

Mliofanikiwa kwenye Network Marketing tunawaomba mtoe Ushuhuda hapa

Hakuna aliyefaidika na hizi Biashara haramu. Kama QNET hawaweki hata bango kwenye ofisi zao yaani ni kimya kimya tu.
 
Wakuu,
Mwishoni mwa mwaka jana Mdogo wangu (Mwanafunzi wa chuo Kikuu Ardhi) alinitumia ujumbe Uliosomeka " Bruv! Nimepata platform ya kupiga pesa, Sure am telling you bruv am gonna be a great millionaire in just few coming days". Nikamuuliza, "Vipi umepata dili la kuwa Contena?(kwa maana ya Msafirishaji wa madawa ya kulevya)" .......Akanijibu "Bruv i just need you to lend me 560k Tshs nimepata nafasi ya kuwa milionea kwa kutengeneza pesa na Kampuni moja ya Kifilipino inaitwa Alliance In Motion Global after one year hata wewe nitakuwa nakupumulia kisogoni". I was shocked kivipi laki tano na sitini izae mamiloni ndani ya mwaka mmoja!! Nilimuuliza dogo iwapo amefanya utafiti wa kutosha juu ya hiyo anayooita "platform" na kunijibu kuwa ameshafanya na anawajua watu wengi waliotusua kupitia hiyo Alliance.

Binafsi nampenda sana mdogo wangu, Sikutaka afikirie kuwa namnyima nafasi ya kutekeleza,adhma yake (Japo nilikuwa na wasiwasi) niliamua Kumtumia Sh. Laki 7 ili akifanya hayo mambo yake abaki na balance ya kutumia kwa muda (ili tusisumbuane tena).....Now ni mwezi wa 6 huu unaelekea wa 7 tangu ajiunge sioni mabadiliko yoyote, mara ananiambia "Bruv, Haya mambo hayataki haraka pesa ipo inakuja". Mara, "oh! natengeneza Pair ya watu wangu ili nianze kulipwa".....Kuanzia hapo nikajua tu kuwa mdogo wangu alipotea njia kwa kufuata mkumbo na kukubali kuingizwa mkenge coz mpaka sasa hazipiti wiki mbili bila kuniomba pesa za,matumizi.

Siku moja tena ya Mwezi February kuna dada alinifuata ofisini akataka tuongee ili anishirikishe busness yao alijitambulisha kwa A.k.A ya Cherry...nilimpomkubalia akaniambia kuwa anafanya kazi na kampuni ya QNET na kuna mtu alim'direct kwangu (alisita kumtaja) ndipo akaanza kutoa "Likitabu" lake lina picha za simu, saa, mikufu nk. Kwa ufupi tu ni kwamba alinieleza kuwa kwa kiasi cha kuanzia dola 2000 kwa maana ya Shilingi milioni tano pekee naweza kununua bidhaa moja kama vile saa au mkufu na nikishirikisha wenzangu wengine nitaanza kulipwa pesa...Niliposikia hivyo nilimwangalia yule dada nikamwambia kwa ufupi ".Sista nipo busy sana kwa sasa na pia siwezi kufanya hiyo biashara yako am so sorry".aliondoka akiwa na mfadhaiko usoni mimi sikujali coz Niligundua kuwa hawana tofauti na wale Alliance waliomtapeli mdogo wangu miezi kadhaa iliyopita.

Nyie watu Wa Hayo makampuni tajwa hapo Juu na ninyi mliofanikiwa kupitia haya makampuni (kama mpo humu) hebu jitokezeni mtujuze mlitumia njia gani..otherwise i declare you kama Matapeli mliofumbiwa macho na Serikali.
Kuna jamaa yangu alijiunga Forever na akanunua bidhaa zao, mpaka sasa hana wa kumuuzia zaidi ya yeye kuvitumia.
 
Good morning mkuu
Hii imenikuta wiki moja iliyopita mpangaji mwenzangu kanifuata kaniambia ana project moja matata sana ndani ya miaka kadhaa atakua bilionea,nikamwomba anipe dili hilo siku ananiita kunitambulisha hiyo biashara nakutana na huu upuuzi wa QNET nikawasikiliza na hilo likitabu lao la picha mikufu na mbwembwe zingine ,nikawaambia tutawasiliana ,then nikaja hapa jf kuuliza kama ulivyofanya wewe but kiufupi ni ubabaishaji huyo Mdogo wako kaingia chaka tu hakuna pesa za mkato kiasi hicho
Salamu yao ya Goodmorning..hata kama ni sa mbili usiku
 
Nilishawahi kujiunga Forever Living wakati nikiwa chuoni, mwaka 2009 nakumbuka, nilipewa mapromise ya kufa mtu. Niliifanya ile kazi kwa mda wa mwaka mmoja hivi ila kiukweli nilikuwa napata pesa za kawaida sana, unakuta zile bonus za mwezi ni kama laki moja au laki mbili, japo nilikuwa nasikia wale waliotutangulia wanapiga pesa sana mpaka milioni 200!!
Kimsingi nilishindwa kuendelea maana natumia efforts kubwa sana kufanya marketing ya bidhaa zao na malipo ni ya kawaida tu.
Pole sana Mr Foreva Livingi😂😂
 
komenti zenu zinanipa raha sana, niliachana na mpz kisa haya mambo nimempa mkwanja kapeleka huko. siku natimba kwake nakuta mifuko mi 3 ya global alliance akaanza stori za kuwa bilionea nikamwambia unaibiwa rafiki yangu stori ikaishia hapo
naondoka nyuma ikafata msg mahusiano yameisha maana staki maendeleo yake na hawezi ambatana na mtu mtu mwenye kukatisha tamaa.

baada ya miezi 3 ananiomba buku 10 ya kula nikampa mara eeeh ikawa kila siku nikamkumbusha yeye ni mfanyabiashara mkubwa akachukia.

kifupi alisha pigwa maana naona sasa ana njaa kali kuliko mwanzo
Hahahahahahh halafu ni wabishi vibaya mno!
 
Ni wabishi hao acha kabisa, alafu hayo mafanikio hata huyaoni kwao.
Wanakera sana....binafsi mdogo wangu ananiomba sana hela wakati aliniaminisha kuwa angekuwa milionea.
 
Danh sijui ni Mungu kaniambia leo nipite JF aisee kesho nikuwa napeleka 500k account moja nianze kupiga pesa Kwa akili yangu

Bora nikanunue kuku huu mzigo
😁😁😁😁Una bahati kinyama wewe ungeliwa hela yako bure!!
 
Mi kuna siku wale wa stem cells,nilikua zangu mcity mgahawan napata juice wadada wa4 mara hao kwenye meza yangu,

Wakaanza ongea pale maneno meeng,mapicha kibao,na product zao .eti in a month ntaingiza $20,000...

Skujib neno hata moja,..mwisho nkawatolea jib tuu kua

"Dada zangu,...wrong person"..taften wengne wale kule,mi nazijua vzur hzo ishu kuliko nyie...wale wadada ikabid wajikusanye waondoke.
 
Back
Top Bottom