katika kukabiri swali kama hili unatakiwa kiwa makini sana. kwanza inabidi uwe umeandaa majibu
ya swali kama hili mapema(hutakiwi kuchukua muda mrefu kufikiri ili kujibu swali kama hili, vinginevyo itaashiria unatunga majibu na kwamba hujifahamu vizuri wewe mwenyewe:
sasa natuanze na uimara wako.
siku zote kile kile kinachomfanya mtu kuitwa bora kuliko mwingine ndio uimara wake. pia kumbuka uimara wa mtu hubadilika kutegemeana na kazi au eneo la kazi. namaanisha ukatiri ni uimala wa mtu aombaye kazi ya jeshi, lakini ni udhaifu kwa aombaye kazi ya udactari(ni mfano tu)
ili kujibu vizuri uimara wako, fanya yafuatayo kabla ya kwenda kwenye interview
- soma mahitaji ya uwezo binafsi unaotakiwa mbali na taaluma ya darasani maana wote mtakuwa nayo. basi hapo ndipo unapotakiwa kuundia uimara wako. mfano anatakiwa mtu mwaminifu, mchangamfu,mwenye kujisimamia kazi,uwezo wa kuongoza au kuanzisha mahusiano kirahisi
- kama hawakuandika kwenye tangazo, basi fikiria mambo ya pekee ambayo mtu wa nafasi hiyo anapaswa kuwa nayo nje ya elimu ya darasani.
- epuka kutaja uimara wako moja kwa moja kama: mimi ni mwaninifu, mimi ni mchapa kazi sana. ninauwezo wa kufanya kazi zaidi ya moja kwa muda mmoja n.k HAIFAI KABISAA TENA NASEMA HAIFAI. Taja uimara wako kwa kuelezea matukio yaliyo kupelekea kutambulika kuwa na uimara huo na si vinginevyo. mfano, anaweza ukasema hivi: mwaka 2000 nilipewa dhamana ya kusimamia fedha za miradi wa ujenzi mara baada ya kurejesha pesa nilizo okota baada ya mhasibu kupoteza. wakati wa kupewa dhamana hiyo niliambiwa uaminifu wangu ndio ulionipa nafasi hiyo. au anza hivi: tangu nikisoma nimekuwa mtu wa kupigania kufikia malengo ya kwenda shule amboyo yaliikuwa ni kufaulu masomo na kweli nilifaulu kwa kila hatua. mpaka leo dhamira ya kufanikisha malengo niliyojiwekea au kuwekewa ni ya lazima niwapo kazini. Au sema hivi: nimejifunza vitu vingi vipya nikiwa ....(TBL) kama ....., ......., ....., na ......... vingine sijapata kuvitumia popote hadi leo, ila vilivyo vingi ndo vimenipa cheo pale Cocacola Co.hata sijui ilikuwaje nikaweza kujifunza vitu vingi kwa haraka namna hiyo. n.k
- Vyovyote utakavyojibu Ndugu ni sawa ila kumbuka kuweka viambatanisho,yaani usiwape mifupa bila nyama
- Pia unapokuwa kwenye interview, kumbuka kujieleza kwa namna ambayo wasilikiliza watavutiwa kukusikiliza. Kila wanapokuuliza swali chukulia kuwa kweli hawajui na wewe ndo unatakiwa kuwajuza kwa muda mfupi sana ila kwa namna ambayo hawatakusahau kirahisi hata baada ya watu kumi watakaofuata.
Kwa leo tuishie hapa, Namna ya kujibu
udhaifu wako itafuata baada ya kujiridhisha kwamba hii ya kwanza imeeleweka. tafadhali iliza popote unapodhani hapajaeleweka