Mlioko karibu na wakili Mwabukusi asiogope "kutikisa m'buyu"

Mlioko karibu na wakili Mwabukusi asiogope "kutikisa m'buyu"

Ni kweli wananchi wengi Wana uhitaji mkubwa sana wa Watu wenye misimamo Kama ya Mwabukusi, isipokuwa tatizo ni kwamba hakuna njia ya kumpitisha mtu wa namna hiyo ili afike Ikulu. Hili ndio tatizo lililopo.
Kafara kubwa inahitajika ili kutengeneza njia ya kuweza kuwapitisha Watu wa namna hiyo. Je, upo tayari kwa hilo??
Wala HAKUNA cha kafara wala nini, ni upumbavu Tu wa Tanzania
 
Mtu mwenye jazba kama yule hafai.
 
Anafaa zaidi kuwa Rais wa nchi.
Kwa nchi kama Tanzania tunamuhitaji mtu mwenye misimamo thabiti inayoeleweka na isiyoyumba kama alivyo Mwabukusi.

Tunataka Kiongozi ambaye akisema No, ni kweli kwamba anamaanisha Hapana, na akisema Yes, ni kweli kwamba aunamaanisha Ndiyo, wala siyo vinginevyo. Na mtu kama huyo si mwingine bali ni MWABUKUSI.
na tutamlinda kwa njia ya maombi, maana watu wa hivyo wanakuwaga na maadui sana.
 
Mtu mwenye jazba kama yule hafai.
jazba zipi. kuonesha hisia zako kwenye jambo ovu ni nzuri sana. huonesha unamaanisha! mtu afichaye hisia zake huwa ni mnafiki.

say what u mean and mean what u say!
 
Kutokana na IQ yake kubwa, ujasiri, uzalendo, misimamo, elimu yake, asiogope kugombania nafasi hiyo kubwa kabisa nchini. anafaa. Wananchi tunamhitaji mtu wa hivyo.

naomba kuwasilisha
Yaani Tanzania hadi Samia na Magufuli wameweza kuwa marais, halafu utasikia watu wakiku diss kwa hili la Mwabukusi.
Nchini Tanzania ukishakuwa na akili timamu na unayejielewa watu wanakuona haufai kuwaongoza, wanakuwa wapo tayari kuongozwa na watu wenye akili za mang’ombe kuliko wanaojielewa.
 
ni kama wako chini ya laana flani
 
Unaweza kumrudisha Magufuli madarakani ?
sio Mimi. Mungu akitaka anaweza. Mungu ndiye afanyaye kwa makusudi yake, sio sisi. Watu wengi sana wameshawahi kurudishiwa uhai wao baada ya kufa. kina Thabitha (Dorcas), Lazaro, Eutiko, na wengineo

JESUS IS LORD&SAVIOR
 
Ni kweli wananchi wengi Wana uhitaji mkubwa sana wa Watu wenye misimamo Kama ya Mwabukusi, isipokuwa tatizo ni kwamba hakuna njia ya kumpitisha mtu wa namna hiyo ili afike Ikulu. Hili ndio tatizo lililopo.
Kafara kubwa inahitajika ili kutengeneza njia ya kuweza kuwapitisha Watu wa namna hiyo. Je, upo tayari kwa hilo??
na utamu wa ugali bamia na dagaa rost jameni? siasa waachien wenyewe wewe mrad unapata ugali wako na watoto
 
Back
Top Bottom