Jaman mlioko ndoan ndan ya miaka 5 nakuendelea mmewezaje??
Yan mmewezaje kuishi wawil mpaka miaka hiyo
Yaan mi miaka 2 tu nataman dunia igeuke kichwa chini miguu juu
Yan ukimuona mwenzio unapata hasira gafla
Akisafir unataman asirudi du!!!
Mmewezaje jaman nipen mbinu
In a scale of 0 to 10 (10 the highest)
1. Wengi mnaingia kwenye ndoa mkiwa na imani kuwa mawifi si watu wazuri. TAYARI HUJAANZIA 0, MAY 4. Hivyo siku akilikoroga, unaanza kwenye 5. The same kwa wakwe
2. Wengi mnaingia kwenye ndoa huku mkiwa na UNREALISTIC expectations nyingi sana ambazo mwenzi asipozifikia, stress huanza
3. Wengi mnaishi maisha ya wengine, si yenu... Yaani mnatamani maisha ta wazazi wenu, kaka, dada au ya mtu mliyewahi ishi naye kwenye hatua mbalimbali za maisha. Ndiyo maana kulinganisha ni kwingi sana
4. Wengi mkiingia kwenye ndoa, UVUMILIVU UNAWASHINDA SANA... kudhani ungefunga ndoa na EX wako maisha yangekuwa matamu, kupo sana. Yaani wengine hutamka kila wanapopatwa na hasira..BORA NINGEOLEWA/NINGEMUOWA FULANI KULIKO KIMEO WEWE...!! Lugha za hivi ON daily Or weekly bases unatefemea nini..???
5. Imani za mfumo dume na beijing zimeuwa na zitaendelea kuuwa na kuwachosha wanandoa wengi sana... Wengine hudai mambo kisa kaona kwa fulani, kaambiwa na mwingine. Kuna watu huleta maisha ya ndoa nyingine kwenye yao bila kuhali mazingira yao yapoje