Mliokopa salio la kawaida kwenye Airtel mmekutana na hiki kitu kwenye kulipa?

Mliokopa salio la kawaida kwenye Airtel mmekutana na hiki kitu kwenye kulipa?

Dawa ya deni kulipa acheni janja janja aisee😅😅
 
Nashangaa line yangu(airtel) siwezi hata kukopa salio, hii imekaaje? Kuna siku nilikuwa sina hela kwenye simu nikajaribu kukopa(sina utaratibu wa kununua vocha ya kukwangua), nimejaribu naona sina sifa wala vigezo..nikastaajabu sana.
 
  • Kicheko
Reactions: amu
Na adhabu juu
Mm nlikopa 100 ya kuongezea kununua bando aisee ,riba cjui 1% per day ile Eh bhan nikaipotezea si Boss bhan kushtuka sms inagonga deni limefikia bukuuu😅😅😅😅
 
Kazini wakiingiza muda wa maongezi mwanzo wa mwezi wanakata pesa yao. Inayobaki natumia ikiisha nakopa tena. Nina ka ulemavu ka kutonunua salio.
Sasa kazini wakiingiza usikope tumia hito tu....hutu tu mia mbili mbili twa riba mwisho wa mwezi unakuta ni 10, 000 umewapa
 
Sijaelewa.
Haani unadaiwa jero salio la kawaida.
Ukiweka 20,000 airtel money wanakata jero yao na inayobaki 19,500 inabadilishwa kuwa salio la kawaida?
Mbona umeelewa mama😆
Airtel huwa inachekesha sana.
Huwa naona mtu mwenye mkopo wa salio akianza kupiga simu jambo la kwanza ni masimango...utasikia kwa sauti "AKAUNTI YAKO INADAIWA"

Huwa nacheeka sana poleni watumia airtel🤣🤣
 
Mbona umeelewa mama😆
Airtel huwa inachekesha sana.
Huwa naona mtu mwenue mkopo wa salio akianza kupiga simu jambo la kwanza ni masimango...utasikia kwa sauti "AKAUNTI YAKO INADAIWA"

Huwa nacheeka sana poleni watumia airtel🤣🤣
Sasa kama amewema laki moja kwenye akaunti yake ya airtel na ana daiwa salio la 1,000 jamani si hasara hii?
Hii haiko siriasi bana.
 
Nashangaa line yangu(airtel) siwezi hata kukopa salio, hii imekaaje? Kuna siku nilikuwa sina hela kwenye simu nikajaribu kukopa(sina utaratibu wa kununua vocha ya kukwangua), nimejaribu naona sina sifa wala vigezo..nikastaajabu sana.
Line una muda gani
 
Shamba la bwana Heri mbuzi wa bwana Heri hakuna kesi hapo.
 
Salamu wadau.

Kifupi sio kulipa labda niseme utaratibu wao mpya sio mzuri.

Juzi kwa dharura nimekopa salio la kawaida nimpigie jamaa nikafanikiwa sasa kesho yake nimeenda kwa wakala niweke hela nashangaa ghafla napigwa na kitu kwamba salio lako ulilokopa limekatwa deni lako na hela iliyobaki imepelekwa kwenye salio lako la kawaida.!!

NIKABAKI kushangaa tu nimetoa macho kama nimebanwa kwenye bawabu za mlango wa mbao.Najiuliza huu utaratibu umeanza lini mbona hawasemi kwanini wasitujuze kama wavotumaga sms zao za matangazo?

Halafu kitu kingine mimi nimekopa salio la kawaida inakuwaje nyinyi mnakata kwenye airtel money? Kama umekutana na hii kitu hebu lete mrejesho kama nado jaribu na wewe kidogo halafu uone.
Mlizoea janja janja, unakopa hela unakimbilia kwenye airtel money kukwepa deni. Sasa ukikopa deni linaingizwa kwenye namba ya simu, kila muamala unalipa deni.
 
Sasa kama amewema laki moja kwenye akaunti yake ya airtel na ana daiwa salio la 1,000 jamani si hasara hii?
Hii haiko siriasi bana.
Mikopo ya makampuni ya aimu ina wizi mkubwa mno
 
Hela iliyopo airtela money haiguswi kabisa.

Kwenye airtelmoney yako una 100,000

Ulikopa muda wa maongezi wa 1,000 jumlisha riba inakuwa 1,200

Baadaye ukaamua kukwepa deni. Ukataka kununua kifurushi cha cha 2,000 kwa airtel money.

WATAKACHOKUFANYIA
Watakata deni lao la 1,200. Kisha 800 itapelekwa kwenye muda wa maongezi. Ukitaka kukopa, kopa tena ili iwe 2000 kamili.

IELEWEKE HIVI
Salio lako la airtel money haliwezi kubadilishwa kuwa muda wa maongezi bila wewe kuamua. Kinachobadilishwa kuwa muda wa maongezi badala ya kifurushi ni kile kiasi cha muda wa maongezi kilichobaki baada ya kukatwa deni juu kwa juu maana kinakuwa hakitoshi kununua kifurushi ulichokusudia.
 
Hela iliyopo airtela money haiguswi kabisa.

Kwenye airtelmoney yako una 100,000

Ulikopa muda wa maongezi wa 1,000 jumlisha riba inakuwa 1,200

Baadaye ukaamua kukwepa deni. Ukataka kununua kifurushi cha cha 2,000 kwa airtel money.

WATAKACHOKUFANYIA

IELEWEKE HIVI
Salio lako la airtel money haliwezi kubadilishwa kuwa muda wa maongezi bila wewe kuamua. Kinachobadilishwa kuwa muda wa maongezi badala ya kifurushi ni kile kiasi cha muda wa maongezi kilichobaki baada ya kukatwa deni juu kwa juu maana kinakuwa hakitoshi kununua kifurushi ulichokusudia.
Kwa hiyo hapo kinachowindwa ni kiasi kinachoelea njiani yaani kinachotoka kwenye airtelmoney na kinachoingia.
 
Back
Top Bottom