Mliokosea kujaza fomu za mikopo helsb 2015

wakusepa

Member
Joined
Jan 24, 2013
Posts
83
Reaction score
5
Habarini vijana wenzangu,poleni na mchakato mzima wa ujazaji hizi fomu za helsb kwakuwa zimekuwa na changamoto tofauti.
Sasa kwa wale ambao katika fomu wamejaza details zao na kisha ku thibitisha(confirm) taarifa ambazo kwa namna moja ama nyingine zimekosewa naomba kusema kuwa huwezi kufanya marekebisho yoyote,
angalizo,huwezi ku print fomu kama hujakamilisha kuijaza na pia kufanya confirmation.
Ushauri wangu hawa bodi mara nyingi ni watu wepesi kukusikiliza shida yako na kukuahid watalishughulikia tatizo lako lakin nikwambie utangoja milele,, wiki tatu zilizopita niliwapigia simu akapokea dada mmoja kumueleza tatizo hili akasema kitengo cha IT wanaliweka sawa subiri after a week utaweza ku edit,sasa zimepita siku na muda huo wa mwisho unakaribia ,cha msingi rafiki jifanye mwehu tu chukua collection fluids futa ulipokosea ingiza taarifa sahihi katika fomu ambatanisha taarifa muhimu subiri mpaka tar 30 june muda wa kusubiri kama itawekwa sehemu ya edit kama hawataweka sehemu ya kuedit tuma rafiki,baadae huwa wanarudisha majina wenyew kwa waliokosea kujaza na kuwapa muda wa ku submit taarifa zenu upya pale ofisi zao.
"HELSB KAZI NI KWAKO"
 
Mzazi alifariki miaka ya 1980 vipi nafanyaje kupata death certificate
 
hii mikopo inatakiwa uwe makini sana kujaza vinginevyo unakosa mkopo
 
Pole sana mkuu inaonesha ni kweli ulikosea hata hapo umeandka HELSB badala ya HESLB. Inahitaji umakini sana ili kuepusha usumbufu
 
Km umekosea kujaza poleni sana lakin jalibu tena kulogin kwenye account zenu kisha mjalibu kuedit
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…