Mliokula chumvi tusaidieni haya mambo sisi vijana

Mliokula chumvi tusaidieni haya mambo sisi vijana

Majibu yako yanafanana na ukweli ila umesimuliwa kijiweni.
sio kama unavyodhani! Wakati mrema anatumbuliwa mim nlikuwa darasa la nne na mpaka leo daftar ambalo nlidalajia gazet la heko lililokuwa na hyo habar nnalo! Na kuhusu kina g55 ni kundi lililodai tanganyika na ndio chimbuko la white paper ambayo ilikusanya maoni juu ya kurejesha mfumo wa vyama ving nchin! So mim sio mhuni wa kijiwen kama ww
 
Kama unaongelea kilichomtoa Mrema kwenye Serikali na CCM kwa ujumla sio dhahabu bali ni issue ya Chavda. Goggle kwa taarifa zaidi.
Issue ya Chavda ndio ilipelekea Mr.Mrema ajiuzuru,na Chavda scandal ililetwa Bungeni kwa mara ya kwanza na Mh.TMN Sanga(rip)huyu mbunge alikua akisimama kuongea, Bunge lote linatulia kumsikiliza SIO vihiyo wa Sasa waliopo bungeni
 
Alikisahau pale Karimjee siku hiyo alikuwa na hasira sana na walanguzi, ilikuwa ni kipindi azimio la Arusha lipo moto... Akaondoka kwa hasira kuelekea kwenye landrover yake kifimbo akakisahau, shida ilianzia hapo. Pia ilisemekana alikiacha makusudi ila za chinichini.
 
Augustino Lyatonga Mrema hakujiuzulu Uwaziri alifukuzwa

Kisingizio kilikuwa kutofautiana na msimamo wa Serikali kuhusu Mashamba ya Muhindi mmoja anaitwa Chavda

Mrema alikuwa Waziri wa Mambo ya ndani na Naibu Waziri Mkuu

Ilipofika 1994 baada ya sakata la G55 kuisha ikabidi Rais Ally Hassan Mwinyi avunje baraza la Mawaziri na kuunda

Mrema kutokana na umaarufu wake wa wakati ule akajua ndio atakuwa Waziri Mkuu lakin badala yake Waziri Mkuu akateuliwa Cleopa David Msuya na yeye akapelekwa kuwa Waziri wa kazi na maendeleo ya Vijana…safari hii hakuongezewa kile cheo chake cha naibu Waziri Mkuu

Yeye kumbe hesabu zake ni urais wa 1995 na system ilishamuona hafai

Baada ya kuona kama kashushwa cheo akaanza visa vya kwenda kinyume na Serikali hadi kupingana na msimamo wa serikali hadharan tena Bungeni hadi Rais Mwinyi akashindwa kumvumilia akamtimua

Baada ya kutimuliwa ndio akajiuzulu Ubunge wa Moshi vijijini na akajivua uanachama wa CCM na kwenda kujiunga na chama cha NCCR Mageuzi na kupewa uenyekiti na kuwa Mgombea wa Urais 1995
Ahsante sana mkuu kwa mchango wako. Kwahiyo Mrema hakufukuzwa uwaziri?
 
Back
Top Bottom