Uwezo wako mdogo sana, unakubali majibu mepesi yenye usanii mwingiWakuu,
Hapa juzi juzi tuliona Tigo imebadilisha jina kuwa Yas na kukawa na tetesi kuwa wanakwepa kodi.
Akijibu swali bungeni kuhusu makampuni yanayobadilisha majina ili kukwepa kodi Mwigulu amesema
"Kupitia sheria ya usimamizi wa kodi ya 238, serikali imeweka sharti kwamba mamalaka ya mapato Tanzania itahakikisha namba ya utambulisho wa kodi yaani TIN inabaki ile ile hata kama kampuni imebadilisha jina. TIN inatumika kufatilia historia yote ya ulipaji wa kodi wa kampuni hivyo mabadiliko ya jina hayaondoi wajibu wa kodi"
Walimkimbia Tundu haoHapa juzi juzi tuliona Tigo imebadilisha jina kuwa Yas na kukawa na tetesi kuwa wanakwepa kodi.
Hata jinalake alibadili!!Uwezo wako mdogo sana, unakubali majibu mepesi yenye usanii mwingi
Huyo mwenyewe kila siku anabadilisha jina la timu yake ya Singida
🐼Uwezo wako mdogo sana, unakubali majibu mepesi yenye usanii mwingi
Huyo mwenyewe kila siku anabadilisha jina la timu yake ya Singida
TIN ikibakiki hiyo hiyo , hakuzui MTU kupata nafuu ya Kodi ya uwekezaji na akumbuke TIN inatumika katika biashara ya mauzo na manunuzi ya kila siku kirahisi Una weza kusema Kodi ya mauzo, sasa nafuu ya Kodi inayoongelewa hapa ni Kodi ya faida ya makampuni, unapofunga Mahesabu ya Mwaka.
SERIKALI KUTUMIA TIN KUDHIBITI KUKWEPA KODI KWA MAKAMPUNI YA KIGENI YANAYOBADILI MAJINA
Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akijibu swali bungeni jijini Dodoma la Mbunge wa Tarime Mjini, Mhe. Michael Mwita Kembaki, aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na Serikali kwa wawekezaji wa nje ambao kila baada ya miaka kadhaa hubadili majina ya Kampuni kwa lengo la kukwepa kodi
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amesema Serikali imechukua hatua madhubuti kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi unaosababishwa na mabadiliko ya majina ya kampuni za kigeni kwa kuhakikisha Namba ya Utambulisho wa Kodi (TIN) inabaki ile ile hata kama kampuni itabadilisha jina.
Hayo ameyasema bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Tarime Mjini, Mhe. Michael Mwita Kembaki, aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na Serikali kwa wawekezaji wa nje ambao kila baada ya miaka kadhaa hubadili majina ya Kampuni kwa lengo la kukwepa kodi.
Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa Sheria ya Kampuni, Sura 212, ambayo inawataka wawekezaji kutoa taarifa kwa Msajili wa Kampuni (BRELA) wanapobadilisha jina la kampuni.
“Historia ya mabadiliko yote ya majina ya kampuni huhifadhiwa kwenye kumbukumbu rasmi ili kuhakikisha majina mapya hayawezi kutumika kuficha madeni ya kodi au kushiriki katika shughuli zisizo halali”, alisema Dkt. Nchemba.
Alisema kuwa kupitia Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura 438, Serikali pia imeweka sharti kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha Namba ya Utambulisho wa Kodi (TIN) inabaki ile ile hata kama kampuni itabadilisha jina kwa kuwa TIN hutumika kufuatilia historia ya ulipaji kodi wa kampuni, hivyo mabadiliko ya jina hayaondoi wala kufuta wajibu wa kodi.
Aidha, akieleza kuhusu kodi zinazotozwa wakati wa kubadili jina la Kampuni kwa watanzania na wageni, Dkt. Nchemba alisema kuwa kubadili jina la Kampuni haiathiri wala haihusiani na masuala ya kikodi.
Alisema kuwa kinachosababisha kuwepo na kodi au ukwepaji wa kodi ni mabadiliko ya umiliki kwa kuuza Hisa ambazo zitaleta kipato cha ziada ambacho kinatakiwa kulipiwa kodi kutokana na faida iliyopatikana.
“Kama mmiliki ni yuleyule ameamua kubadilisha jina la Kampuni kwa ajili ya matangazo ya kibiashara na Namba ya Mlipa Kodi ni ileile, haileti badiliko lolote kwenye kodi”, alifafanua Dkt. Nchemba.
Alisema kuna kampuni za nje ambazo zinamiliki sehemu ya kampuni nchini na hazina shughuli zaidi ya zinazofanyika Tanzania, ikitokea wamebadilishana umiliki unaozidi asilimia 50, hapo kuna kodi ambayo ni lazima ikusanywe.
Alisema Serikali imefanyia kazi kwa kiasi kikubwa suala hilo lililokuwa likijitokeza katika maeneo ya mawasiliano, madini na mengine na amewatoa hofu wabunge kuwa Serikali imeweka kwenye Sheria na inafuatilia kwa umakini panapotokea jambo hilo na kodi stahiki ya Serikali inakusanywa.
Muongo mkubwa sana huyo.Wakuu,
Hapa juzi juzi tuliona Tigo imebadilisha jina kuwa Yas na kukawa na tetesi kuwa wanakwepa kodi.
Akijibu swali bungeni kuhusu makampuni yanayobadilisha majina ili kukwepa kodi Mwigulu amesema
"Kupitia sheria ya usimamizi wa kodi ya 238, serikali imeweka sharti kwamba mamalaka ya mapato Tanzania itahakikisha namba ya utambulisho wa kodi yaani TIN inabaki ile ile hata kama kampuni imebadilisha jina. TIN inatumika kufatilia historia yote ya ulipaji wa kodi wa kampuni hivyo mabadiliko ya jina hayaondoi wajibu wa kodi"
🤣 🤣 🤣Hata jinalake alibadili!!
Na wewe ujuaji mwingi wakati kichwani hamna kituMuongo mkubwa sana huyo.
Hivi bado ana fikra potofu kwamba Wananchi wote kabisa wa Tanzania ni Wajinga wa kiasi hicho anachofikiri yeye?
Wale Watu wa 'Zidumu Fikra za Mwenyekiti' wamebaki wachache Sana, wengi wao walishatangulia mbele za haki.
Watu wengi zaidi waliopo zama hizi ni Watu wa 'Kizazi Cha Kuhoji.' Anapaswa kulitambua Jambo hili
Ujinga mzigo mkubwa mno ulionao.Majina ya kampuni hununuliwa pia unaponunua kampuni.Waweza kataa kulipia jina ukaja na la kwako .Hivyo kupunguza gharama za kununua kampuniWalimkimbia Tundu hao
Una uelewa mdogo mno unatoa jibu rahisi kwenye hoja nzito..Na kubadilisha jina hakuwasafishi na madai ya kushirikiana na Magufuli kumdukua Tundu Lissu.
MmmmmmKumbe ukishaona VAT imefika usipoweza unafuta kampuni au kubadilisha usajili jina kuanza upya. Au sio
Usifikiri kwamba Mimi Sina akili kama ulivyo wewe.Na wewe ujuaji mwingi wakati kichwani hamna kitu
Uelewe kitu kimoja unaponunua au kuuza kampuni huwa kuna vitu vinne mnakubaliana kwenye kuuziana
Cha kwanza mnauziana mali za kampuni
Cha pili mnauziana madeni ya kampuni
Cha tatu nnauziana wafanyakazi wa kampuni
Cha nne mnauziana jina la kampuni au kwa lugha ingine mnauziana brand ya kampuni brand bei yake huwa kubwa sana sababu mtu kaijenga muda mrefu sana kuifanya biashara ifahamike sokoni
Hivyo kila kitu huwa na bei yake.Mnunuzi aweza amua kuwa nanunua mali tu za kampuni.Madeni sichukui ,wala wafanyakazi sichukui au ,wala brand au jina la kampuni sichukui nitatengeneza brand au jina langu mwenyewe
Au aweza sema nitachukua mali na wafanyakazi baadhi au wote ,madeni sichukui na jina sichukui nk
Hivyo kujua kwa nini mtu anabadili jina lazima uende ukaaangalie mkataba wa mauziano alinunua nini lakini kwa kawaida tu bei za brand huwa kubwa mno kuliko hata mali za kampuni mara ingineb.Mfano unataka kununua timu mfano Yanga au simba bei yake sio ya kitoto bei ya jina au brand itakuwa kubwa kuliko majengo na mabasi waliyonayo ndio maana wengine huamua kuanza na brand name zao mpya kama AZam ,Namungo nk
Kwa wajuzi wa biashara wanaelewa kuwa aliyenunua Tigo ni wazi aliona bei ya brand kwake mziki mrefu akaamua tu asinunue aanzishe tu brand yake ya yaas maxxc
Watanzania hasa ngozi nyeusi uzoefu wa biashara wengi uko zero kazi kuhisi hisi vitu tu kuwa ooh yule kanunua kampuni kabadili jina mwizi anatuibia kodi na unakuta anayesema hivyo maisha yake yote hajawahi uza hata peremende lakini ujuaji mwingi wa kijinga Kama wa kwa kwako huo