Mliokuwepo miaka ya 70s mtuambie el nino ilianzaje, tuchukue tahadhari

Mliokuwepo miaka ya 70s mtuambie el nino ilianzaje, tuchukue tahadhari

hermanthegreat

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2021
Posts
1,274
Reaction score
3,282
Wakuu, wazee, hivi hata El nino ya 70s nayo ilikuwa inanyesha kidogo kidogo kwa mda mrefu kama hii ya dar?
Tusimulieni kidogo jinsi mlivyoiona huku mkiifananisha na hii tuchukue tahadhari.
 
Usinikumbushe Tanzania yote ilijaa maji nakumbuka kutoka singida kwenda dodoma watu walikua wanaenda na mitumbwi.

Enzi hizo nilikua na miaka 38 ilibidi nitumie kopo la kuogea nachota maji singida namwaga upande wa tabora shinyanga ili yaende ziwa victoria
 
Wakuu, wazee, hivi hata El nino ya 70s nayo ilikuwa inanyesha kidogo kidogo kwa mda mrefu kama hii ya dar?
Tusimulieni kidogo jinsi mlivyoiona huku mkiifananisha na hii tuchukue tahadhari.
kipindi hicho nilikuwa na miaka 17 daah Hali ilikuwa mbaya Sana mvua ilivyunja madaraja,nyumba ,na mabanda ya mamantikie

Ah asee sitokuja kusahau kipindi hicho Mzee anafanya kazi posta pale, alichukuliwa maji maeneo ya jangwani.... alhmdullillah akanasia kwenye jiti kubwa ndio ilikuwa salama yake vinginevyo angekuwa kashabadikishwa jina

Ila kwahii mvua sioni Dalili za elnino

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Usinikumbushe Tanzania yote ilijaa maji nakumbuka kutoka singida kwenda dodoma watu walikua wanaenda na mitumbwi.

Enzi hizo nilikua na miaka 38 ilibidi nitumie kopo la kuogea nachota machi singida namwaga upande wa tabora shinyanga ili yaende ziwa victoria
hahahhahahh dah komenti zingine humu ni balaaa
 
Watu wengi wanaoongea kuhusu hii mvua ni raia wa Dar, kwan mna shida gn nyie pipo za Dar mbona ht mikoani mwingine mvua inanyesha ya nguvu au hy El Mino Ipo kwenu tuu.?
 
Usafiri wa treni dar kwenda mwanza ulistop tukaanza kuzungukia kenya na uganda ili kufika mwanza,ilikuwa fedhea
 
Usinikumbushe Tanzania yote ilijaa maji nakumbuka kutoka singida kwenda dodoma watu walikua wanaenda na mitumbwi.

Enzi hizo nilikua na miaka 38 ilibidi nitumie kopo la kuogea nachota maji singida namwaga upande wa tabora shinyanga ili yaende ziwa victoria
Daah mamaee [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nakumbuka ya mwaka 1997 ilikuwa siyo kwamba inapiga kwa fujo, la hasha! Inapiga kwa utulivu ila muda mrefu halafu inanyesha siku nyingi, jua linawaka siku chache sana.
 
Nakumbuka ya mwaka 1997 ilikuwa siyo kwamba inapiga kwa fujo, la hasha! Inapiga kwa utulivu ila muda mrefu halafu inanyesha siku nyingi, jua linawaka siku chache sana.
Ndio kama hii
 
Wahenga si mnaitwa lakini...[emoji1787][emoji1787]

Mbona kama mnajificha hivi [emoji1787][emoji1787]
 
Sie wakazi wa magomeni mapipa nilikuwa la kwanza mpaka leo nakumbuka mvua ilikuwa taratibu ili haikomi kuna wakati ikipoa Dar pwani inayoyoma.

Matukio ninayokumbuka edikopta zilikuwa zinatega mto msimbazi pale Madaba, jangwani na kigogo kuokoa watu waliosombwa na mafuriko na edikopta nyengine ilikuwa inatoa watu na watoto kwenye mabati ya nyumba ukisikia nakufaa nisaidie ujue tayari mto ushasomba watu ni kipindi cha majonzi.

Wengine walikuwa wanategea vitu vyao vya dhamani pale jangwani na wengine wezi humohumo.
 
Back
Top Bottom