Mlionidhihaki na Kudai Mimi ni Yanga SC pale nilipotoa Angalizo la Kiufundi kuihusu Simba SC naomba na leo endeleeni Kunidhihaki tena!

Ila we jamaa hodari sana aisee.
Hivi umeajiriwa JF maana hamna siku hujatoa nyuzi kama sio mbili tatu.

Aisee hongera mkuu
 
Na kwa Kipigo hiki cha Kikatili / Kishalubela sijaona sababu yoyote ya Simba SC kutokucheza Mechi zake za ' Viporo ' vya Ligi na nadhani huenda Simba SC ingekuwa inacheza pia na Mechi zake za Ligi labda ingewasaidia kidogo katika Kujenga Kikosi chake na Kukiandaa zaidi na angalau basi hata kama tungefungwa basi zingekuwa ni Goli labda 1 au 2 tu na siyo ' Kiganja / Tano ' kwani zinauma mno na hadi hivi sasa zimenikosesha Usingizi na hata hamu ya ' Mbunye ' ya Mke wangu leo sina japo naiona ile pale Kitandani ipo tayari tayari ikinisubiri.
 
mleta uzi hongera kwa kuyaona haya kwenye mechi ya leo..
huwa najiuliza. shabalala huwa wanampanga wa kazi gani?? mfupi namna ile hana ubavu kama genta anavyosema. ni mara mia hata kwasi acheze ubavu wa kushoto kuliko shabalala!..
lile goli lá kona liliniacha na maswali mengi kuhusu wawa.. kwanza mpira ulipita juu yake na yeye hakuruka angalau aurudishe hata kule kwenye kona au hata nje kwa kichwa.. jamaa wa as vira akaruka free kabisa..
pia pale kwenye kiungo mkude pekee ndo alioneaha kuwa na uchungu na mechi hiyo..
 
Kuna wafuasi wa timu nchi hii hata useme ukweli kuhusu madhaifu ya timu zao na TFF yao hawawezi kukuelewa. Mtu anaamka asubuhi anaanza kuifananisha Simba na Real Madrid, kesho yake mwingine anainuka anailinganisha Yanga na Juventus (Kibibi Kizee cha Turin) kisa tu haijapoteza mechi kama Juve. Wafuasi wa timu za Tanzania ndio chanzo cha ubovu wa timu za Tanzania. Na kwa bahati mbaya wafuasi hao ndio wanaochagua viongozi wa kusimamia timu hizo kwa hiyo wanaochaguliwa nao wanakuwa na akili kama za wafuasi wao, ukienda kinyume na akili za wafuasi huchuguliwi tena.
NIANZE NA TFF;
Shirikisho hili linaendeshwa kama Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini. Sina ushahidi lakini sidhani kama Dunia hii kuna nchi klabu inapewa mapumziko ya ligi siku 13 eti ijiandae kwa mechi ya kimataifa na katika hizo siku 13 hakuna hata mechi moja ya kujipima nguvu, Halafu kocha naye anakubaliana na mgao huo wa "Laziness holiday". TFF iko kama ofisi ya Masajili anavyotaka kuwafuraisha CCM na CDM kwa kubalance maamuzi. Yaani unampa mtu kitu hata kama kina madhara kwa vile tu na mwenzake ulimpa. Kuna kipindi TFF (FAT wakati huo) kwenye mechi ya Simba Vs Yanga waliwahi kununua mipira miwili mmoja ukiwa na rangi zinazotumiwa na Simba na mwingine ukiwa na rangi zinazotumiwa na Yanga, kila mpira ulitumika kipindi kimoja ili kila timu iridhike. Kwani hiyo ilizuia malalamiko? Simba walifungwa na mpira wenye rangi ya njano na nyeusi, yaliyozuka yalisababisha tunaojitambua tuache kushabikia Usimba na Uyanga kamwe.
Umbumbu huu wa TFF ndio unaosabaisha leo tofauti ya mechi kati ya Simba na wengine kufikia hadi mechi 6 na Simba wenyewe wanaona sawa tu. Hawakumbuki huko mbele watajipa mzigo wa viporo vya mfululizo unaoweza kuwasababishia majeruhi yatokanayo na uchovu wa mechi mseleleko ikawasababishia kukosa Mwana na Maji ya Moto.
WAFUASI WA TIMU
Binafsi naamini Tanzania ina mashabiki wachache sana wa mpira na wengi ni wafuasi wa timu. Wengi wako tayari kutetea hata rafu ilitochezwa na mchezaji wao ili tu waonekane wana mapenzi ya dhati na timu. Hata Jana Wawa alipoacha mpira na kufuata mwili wa mpinzani alupata watetezi, na hili hata kwa Yanga pale Kambarage lilikuwepo. Mashabiki wanaibeba timu kwa kuwa wachezaji wa12 kwa vile ni washangiliaji, wahamasishaji, wafariji na kikubwa wakosoaji, ndiyo maana Ulaya mchezaji ukifanya ujinga labda wa kujisababishia kadi nyekundu ya kizembe siku ukirudi unazomewa na mashabiki wa timu yako, lakini kwa Tanzania utaaifiwa na kuitwa mbabe wao hata kama kadi hiyo itagharimu timu.
Tatizo lingine la wafuasi wa timu za Tanzania ni Ku Overate wachezaji na kusababisha wachezaji wajione babu kubwa tofauti ni uhalisia. Miaka ya nyuma Yanga alitokea mchezaji anaitwa Said Sued "Scud', huyu si tu hakuwa na kiwango cha kawaida, bali alikuwa na kiwango cha chini cha mpira. Ila alikuwa na bahati ya kuifunga Simba, humwambii chochote mfuasi wa Yanga kuhusu " Scud", wanamuona bonge la striker lakini wa ovyo tu toka pale Kigoma. Hili ndilo linalowakumba Simba kwa sasa hadi kufikia kumfananisha Chama na Ngolo Kante (Kichuguu na Mlima). Sisemi hajui ila ni mchezaji anayecheza na jukwaa muda wote. Badala ya kutekeleza majukumu yake anataka kusikia jukwaa linasema nini juu yake. Anasahau kuwa timu ilijengwa juu yake na hivyo hatakiwa kufanya masihara, matokeo yake almeiangusha timu na alipotolewa waliobaki wakajua kumbe Leo hatuna letu maana hata nguzo ya timu imeshindwa kazi.
MECHI YA JANA
Hebu mwangalie mchezaji kama Fabrice Luamba, kiungo wa SC Vita aliyekoroga mipango yote ya Simba Jana. Wala hakusubiri wangapi wanapiga makofi kwake, alifanya alichotumwa na sifa kazipokea baada ya ushindi.
Kingine kilichoiangusha Simba ni ule ugonjwa wa wachezaji wengi wa Tanzania yaani Stamina (siyo yule mwanamuziki rafiki wa Roma), hii iliwafanya waonekane wepesi kila walipopokea mipira au kukaba. Ni mchezaji mmoja tu aliyeonekana mkamilifu katika hili, Medy Kagere, wengine waliobaki hasa beki 3 alikuwa mwepesi kam under 14.
HITIMISHO
Timu inaweza kufanya vizuri zaidi ya Jana, kama tu inatajijenga kimpira na siyo kisanii.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli kabisa...Simba inahitajika kusajili mabeki wazuri na kusajili viungo ili kuongeza nguvu katikati, jana Vita walikuwa wanatekeza kuanzia katikakati hadi kwenye mabeki, mfadhali wa Simba atoe pesa wasajili wachezaji, ukweli mpaka sasa mbadala wa Kapombe hajapatikana, kule kwa Husein nako ni tia maji tia maji, tumeona ubovu wa timu kwa kucheza na timu bora..Kuhusu Kocha yupo vzr ila wachezaji alionao ndio wanamuangusha.
 
Nakubaliana nawe kupigwa hamsa inauma sana,beki ya Simba ianapwaya sana bila marekebisho tutalia zaidi na forward nako bado washambuliaji ni butu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamati ya usajili ya simba pia iangaliwe kwa jicho pevu, hauwezi kumsajili mtu kama yule culibali kama una akili timilifu, na unaitakia timu mema, uyo shabalala ndio hkna mchezaji kbsa hpo, back Pas zake ni za hovyo kbsa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakuunga mkono.
 
Unazi ulisababisha watu kusema hakuna mchezaji Tanzania anayeweza kupata nafasi kwenye line up ya Simba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna ukweli mwingine kuwa simba hawana goalkeeper wa mashindano makubwa, huyo waliyenaye ana bahati tu ya kupendwa ila hafai, hata kwa taifa stars
 
Kocha bomu unafungukaje ugenini na timu kama AS Vita

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba haina mfadhili. Halaf daaah wabongo wepes wa kusahau... si mlikuwa mnaisifu line ya viungo ya simba majuzi tu hapa. Tambo za "hakuna team bora zaid ya mnyama ktk ukanda wetu huu, mara blah blah" leo team 'mbovu'
 
Niyonzima anakuja alikuwa swala 5 tena muumini ile mbaya kipindi anakaa makuti ila huwezi amini akaja kuwa mvuta bangi aliyekubuhu alikuwa akija kitaa kuna mshikaji wana ukaribu sasa akija huwa ni shangwe mapuli yananunuliwa na pombe hapo ni mwendo wa kunyonga na kunywa

Niyonzima migo imembadilisha sana..niyo alikuwa ustazi ,shehe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha ha ha ha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…