Namshukuru Mwenyezi Mungu kidogo hizi Timu mbili Kubwa baadhi ya Wachezaji Wao ' Waandamizi ' kabisa hadi Viongozi Wao baadhi ni Marafiki zangu wakubwa na wazuri tu ila kwa Kiwango ' Kibovu ' nilichomuona nacho leo Chama ' Tripple C ' naanza sasa kupata hisia kwamba huenda ile mbinu iliyotumika ' Kumuua ' Kimpira Kiungo aliyekuja vizuri na alikonga nyoyo si tu za Yanga SC bali hata Sisi Simba SC Papy Kabamba Tshishimbi na leo ' Kwishnei ' kabisa.
Wapenzi wa hizi Timu mbili Kubwa walivyo au tulivyo ' Wapuuzi ' tukishampenda tu Mchezaji fulani basi haraka sana tutaanza Kumnunulia Bia, Kumtafutia Mademu tena yale Mashangingi kabisa ( Malaya ) wa Mjini huku ' tukidalalia ' ili Yule Demu akiwa anahongwa basi na Wewe hapo hapo unajua kuna 10% yako.
Kama ambavyo Tshishimbi amepotezwa Kimpira na Mimalaya ya Dar es Salaam, bila kumsahau Mtu mwingine Mshambuliaji Mzambia Felix Sunzu, Boniface Ambani sasa kwa huu ' Umaarufu ' wa ghafla wa Chama naona nae anaelekea huko huko ' Kupotezwa ' na Wajanja Wajanja. Lakini hata Waandishi wa Habari wa Kike nao kwa Kiasi Kikubwa mno wanachangia ' Kuua ' Vipaji vya Wachezaji wengi mahiri na wakubwa wa Ligi Kuu ya Tanzania hasa kwa ' Kujitongozesha ' Kwao Kilazima ili wawe nao na wawe wanapata ' Vijisenti ' vyao lakini pia wawe kama ndiyo ' Sources ' wao Wakubwa Kihabari na kuwarahisishia Kazi zao. Ipo Siku ' Mizimu ' yangu ikinipanda na ikikasirika nitawaanika hao Waandishi wa Habari wote wa Kike ambao wana huu ' Upuuzi ' kwa Wachezaji ila kwa sasa nawastahi kwa Kuwatunzia tu Heshima ila wajirekebishe.
Haruna Niyonzima alikuwa ni Swala Tano kabisa ila nikisema hapa alivyobadilika Kipindi cha mwisho alipokuwa Yanga SC na hata mwanzoni alipokuwa Simba SC wengi mnaweza mkalia bure kama siyo Kusikitika japo kidogo sasa baada ya Kusemwa semwa na Watu wake wa karibu ameanza Kubadilika. Beki kama Nadir Haroub ' Cannavaro ' siyo wa Kutundika daluga sasa hivi ila nae nikiweka hapa hadharani kilichommaliza / kilichomuua Kimpira hamtoamini ila nae namtunzia Heshima yake.
Chama asipowekwa chini, akaonywa na kujitambua sasa hivi nae yatamkumba ya Wenzake Tshishimbi na Niyonzima.