Mliooa "boxer" mnaanika wapi?

Me naanika chumbani.ipo sehemu maalum yenye nguo zangu na nguo za mkewangu
 
Sidhani kama kuna ubaya ukianika nje kwenye mwanga wa jua. Kila mtu anatumia ivyo hakuna ubaya. Mi daily natundika boxer nikirudi jioni naanua tu nakuta imeshakauka
 
Kuwa nazo za Monday-Friday unafua zote Saturday unazianika nje kwenye jua. Nunua mbili tatu za ziada kama mvua zinanyesha.

Sisi tukiwa safarini to the moon inabidi tufue kila siku.
Hiyo safari unakuwa babu yangu Aspirin au mwenyewe????
 
Sijui kwanini boxer/chupi inaonekana kitu cha ajabu! Si unaanika nje kwenye kamba au zimefubaa na zina matundu?! Mimi nalundika wiki nzima au zaidi nikifua naanika kamba nzima.
 
Tunaanika sebuleni (sitting room) mkuu
 
unaanika nje ila unatafuta kanga unafunikia kwa juu na kubana na vibanio zisianguke. Nguo za ndani pamoja na soks zinapaswa kuwanikwa juani ili kuua fungus.
 
Mmh. Itakuwa haziko vizuri ndio sababu unajiuliza pa kuanika.

Mwambie mkeo akizifua aanike nje pia jitahidi uwe nazo za kutosha angalau afue kwa wiki mara moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…