Mliooa "boxer" mnaanika wapi?

Mi huwa naanika kama nguo nyingine tuu,ukiona mtu anashangaa ujue ndio wale watembea uchi.
 
Sijaoa lakini huwa nazianika nje tu, ila kwa wadada naona huwa inakuwa shida kidogo, kwa ushauri wangu kwa kina Dada au mtu yeyote anayeona aibu kuanika nguo yake ya ndani hapo nje, chukua kitamba, mtandio au kanga nyepesi kisha ukishaianika hiyo nguo yako au zako za ndani kwa juu unazifunika na hiyo kanga au kitambaa chepesi, hapo zitakauka vizuri tu bila wasi wasi
NB: Muanuaji uwe mwenyewe vinginevyo itakuwa balaa, maana akianua mwingine hatojua kilifunikwa nini
 
Huku uswazi kwetu huwa burudani sana ukikuta chupi zimeanikwa...

Kuna watu wana chupi kubwa buanaaaa...unaweza ukadhani ni kitambaa cha kufunika 'coffee table'
 
Unaanika nje juu ya kamba na kama unaona aibu unapachika juu kanga kishkaji kama vile unafunika
Ila unafunika za nini?? Kama zina rangi nzuri na hazijagimbaa unaanika hivyo hivyo
 
Wewe huwa unapasi chupi? b honest...Mimi sipasi..kiukweli..
 
Changamoto Wale Wanaokaa Nyumba Za Kupanga Na Mna Watoto Kama Wa 3 Hv Differ Sex
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…