Mliopata ajira za serikali wasaidieni wale walokosa ajira kinamna hii

Mliopata ajira za serikali wasaidieni wale walokosa ajira kinamna hii

kishuga

Member
Joined
Jan 24, 2023
Posts
35
Reaction score
136
Hongereni wote mliopata mliopata ajira katika kada ya Ualimu na Afya ni wakati wa kwenda kulitumikia Taifa na kuwafuta machozi wale waliokuwa wanawategemea makubwa hasa baada ya kumaliza Elimu.

Lengo la uzi ni kuwaomba wale wote waliochaguliwa ajira serikalini na kwa hakika katika hao kuna asilimia kubwa pia ya watu waliochaguliwa walikuwa wanafanya kazi katika sekta binafsi kama partime, wengine waliajiriwa kabsa na wengine walikuwa wanajitolea na angalau mlikuwa mnapata chochote kitu huku mnaongeza ujuzi wenu.

Lazma kutakuwa na magape tu huko mlikotoka mkakimbilia fursa za serikali, muhimu ni kuwajuza sehem mlizokuwa mnafanyakazi wale mnaowafahamu ambao wamekosa ajira na hawana pa kukimbilia waende wakajaribu bahati zao huko mlipokuwa nyie.

Kikubwa ni kumpa mtu taarifa kituo cha kazi kilipo namna ya kufanya kupata kazi unaweza kumuachia mwenyewe. Na ikiwa pia una uwezo wa kumsaidia kuingia moja kwa moja kazini itakuwa vizuri zaidi.

Kuna kijana mmoja ameweza kumsaidia mwenzake Mwalimu kwenda kufundisha private amempigania mpaka ameweza kupata nafasi aliyekuwa anafundisha yeye baada ya Mungu kumjaalia kupata ajira. Naona wengine msaidiane namna hiyo.

Msaidie yeyote yule utakuwa umemuinua kikubwa zaidi yeye pamoja na wale wanaomtegemea.
 
Kuna Uzi mwingine wa juzi kama hivi lakini akuna ata Mmoja aliyetoa code hiki kitu kwa cc wabongo shidah tuna roho mbaya
 
Back
Top Bottom