Mliopiga Misumari Fraga na sasa Lwanga, mnatukosea wana Simba

Kwenye soka mkuu wangu huwa siamini uchawi! Hadi Akina Pogba,Hazard, Neymar n.k huwa wanakuwa majeruhi ulaya na kukaa nje muda mrefu sasa wao pia huwa wanarogana, na wakipona wanarudi na kuanzia walipoachia. Anyway poa mkuu yote ni Imani!
Usifanishe ulaya na Tz tume kulia kwenye tamaduni tofauti na mazingira tofauti, hii kitu ipo mimi nilisha simuliwa na mchezaji mmoja wa Simba vitu hivi vipo.
 
Kwenye soka mkuu wangu huwa siamini uchawi! Hadi Akina Pogba,Hazard, Neymar n.k huwa wanakuwa majeruhi ulaya na kukaa nje muda mrefu sasa wao pia huwa wanarogana, na wakipona wanarudi na kuanzia walipoachia. Anyway poa mkuu yote ni Imani!
jipe muda wa kufuatilia kisha sahihisha imani yako mkuu.
 
Huko Yanga ,Mapinduzi Balama , yakuba , Boxer . Yasini msitapha n.k. walipigwa na nani hiyo misumari mkuu? Hizo ni ajali kama zilivyo ajali nyingine kazini. Muhimu ni kuwaombea wanaokumbwa na hayo masaibu wawe wanapona haraka ili kuendelea na majukumu yao.
 
Fraga Ameshapona, Hili Dirisha Dogo wa Mrudishe kama Wakiona Majeruhi ya Lwanga ni Ya Muda mrefu, Fraga imeshakuwa Mwaka 1 na Nusu Sasa, Sidhani kama Atapata Injury Tena
 
Mzamiru,mkude na Ajibu ndiyo michezo yao
 
Nimeshangaa sana injury ya kumuweka nje Lwanga aliipatia mechi gani??? Kuna wachezaji pale Simba wanawachezea hawa wageni kwa ushirikina injury aliyoipata Fraga ya ajabu ajabu ndio hiyohiyo ya Lwanga.

Viongozi wafanye maamuzi magumu hii ni too much.
 
Mpige misumari halafu umzidi kiwango cha ajabu unampiga misumari na kiwango chako bado duni
 
Simba hiyo ni tabia yao kwa ujumla,si wachezaji si viongozi kupigana misumari ndio jadi yao.
Simba wameionea sana Yanga kwenye kuwapiga misumari wachezaji wao,sasa kibao kimegeuka wanapigana wao kwa wao.
Wacha mvua iendelee kunyesha tuone panapo vuja.
 
Kwenye soka mkuu wangu huwa siamini uchawi! Hadi Akina Pogba,Hazard, Neymar n.k huwa wanakuwa majeruhi ulaya na kukaa nje muda mrefu sasa wao pia huwa wanarogana, na wakipona wanarudi na kuanzia walipoachia. Anyway poa mkuu yote ni Imani!
Kamuulize torres pale chelsea mbele ya drogba alifanywa nini ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€yeye na goli game ya united na akapiga nje.....sisi waafrika kwa jicho la tatu tulijua nini kafanyiwa na drogba ila yeye naamini mpaka anastaafu hajui kama aliwahi fanyiwa mazingaombwe mamaeee
 
Imani potofu
Uchawi ungekuwa unasaidia hao wachezaji si wangeenda Ulaya wakawapige misumari kina Ronaldo?
 
Misumari ipo ila sijajua kwa ngazi za vilabu vya ligi kuu hali ipoje.

Enzi hizo tunashiriki UMISETA, mchezaji anakichafua ngazi za chini. Ikifika hatua ya kutafuta timu ya mkoa hali inakuwa ngumu sana. Unakuta siku moja kabla ya mchujo mchezaji anaugua jipu kwenye dole gumba. Uchaguzi wa timu ya mkoa ukimalizika, dole gumba linapona na anarudi nyumbani.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ