Mliosoma au kuifahamu Tumaini - Iringa, je hii ni kweli?

Mliosoma au kuifahamu Tumaini - Iringa, je hii ni kweli?

Kimbori

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
6,112
Reaction score
4,540
Katika kupiga stori huku mtaani nimekutana na hii.
Kuna jamaa mmoja alihitimu shahada ya kwanza ya Utalii (Cultural Anthropology and Tourism ) hapo Tumaini - Iringa mwaka 2008. Jamaa huyo anajuta sana, tena sana, kwa kuwa haajiriki. Tangu ahitimu, miaka takribani mitano iliyipita, kila anapokwenda kuomba kazi anaambiwa alivyosoma si sahihi (irrelevant), hivyo yupo chini ya ubira (under qualification). Na si kwake yeye tu bali hata wahitimu wenzake wanaambiwa vivyo hivyo.
Anasema inaweza walifundishwa visivyo kwa kuwa walifundishwa na waalimu waliojua masuala ya Utalli, mfano Linguisics.
Binafsi nimeshtuka kidogo, kusikia mtu amesotea miaka miatau katika shahada, ila haajiriki kwa kua alisoma 'matango pori'. Naomba kujua, je kweli?
 
Wewe mwenyewe akili hakuna kabisa yaani mtu akisoma lazima aajiriwe...
 
mm cjawah kukisikia kwann asingeenda vyuo vinavyotambulika bse enzi zake tcu hawakuwepo so alaumiwe nan?
 
Wewe mwenyewe akili hakuna kabisa yaani mtu akisoma lazima aajiriwe...

Ahsante kwa kashfa. Ahsante sana. Ila nakuomba, kama unaweza, soma tena mada na utafakari kidogo. Wakati huo na mimi najitafakari kama nina akili aui sina.
 
mm cjawah kukisikia kwann asingeenda vyuo vinavyotambulika bse enzi zake tcu hawakuwepo so alaumiwe nan?

Miongoni mwa vyuo alivoomba na kupata ni Tumaini - Iringa na SAUT (Mwanza). Aliamua kusoma Tumaini baada ya SAUT kuchelewesha majibu, pia anaishi Iringa Mjini, hivyo ilikuwa rahisi kusoma kwa gharama nafuu.
 
Sio kweli hio kitu ni uzushi tu suala la mtu kukosa ajir kwa sasa ni kawaida sana mbona wapo kibao walosoma iyo course pale tumaini na wameajiriwa

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom