GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Nimepokea Kwa Masikitiko Makubwa Kifo Cha Mhadhiri Mwandamizi na Aliyewahi Pia Kuwa Mkurugenzi Wa Iliyokuwa Redio Tanzania Dar es Salaam Na Mwandishi Wa Vitabu Na Makala Za Uhakika Mr. Nkwabi Ng'wanakilala Kilichotokea Usiku Wa Ijumaa ktk Hospitali Ya Rufaa Ya Bugando Baada Ya Kufanyiwa Oparesheni Ya Tumbo. Hakika SAUT Haswa Idara Ya Mawasiliano Ya Umma Na Uandishi Wa Habari Tumepoteza Mtu Muhimu Mno na Binafsi Nitamkumbuka Sana Kwa Ufundishaji Waji Ambao Ulikuwa Wa Uhakika Na Very Friendly Na Alinisaidia Mno ktk Kufanya Research Yangu Na Kuniongoza ktk Masuala Mengi Ya Masuala Ya Communication Na Journalism Na Nilifarijika Sana Kufundishwa Na Marehemu. Kila Nikumbukapo Ucheshi Wake Darasani Napatwa Na Simanzi Mno Na Hakika Alikuwa Ni Mtu wa Watu. Najua Wale Mass Comm Wote Wa 2006 Hadi 2009 Na Wengineo Pia Tutamkumbuka Marehemu Kwa Mengi. Bwana Ametoa Na Bwana Ametwaa Jina Lake Lihimidiwe Amen. RIP Mr. Nkwabi Ng'wanakilala.