Mliosomea uchumi msaada tafadhari.

Mliosomea uchumi msaada tafadhari.

kidonto

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2014
Posts
1,961
Reaction score
2,918
Majuzi nimerudi toka south africa nikipita nchi za zambia na zimbabwe, kilichonishangaza ni thamani ya kwacha ya zambia kuwa juu kuliko rand ya south africa, je? Ni kweli zambia wana uchumi mzuri kuliko tanzania , kenya ama south africa? Wakati rand 1 ni sawa na t' sh. 150, kwacha 1 ni sawa na t'sh. 300, ni nini kimefanya zambia wawe juu hivi? Sababu ya shaba? Mbona south africa wana gold? Ambayo kwa uelewa wangu ni zaidi ya shaba? Mbona hata kwa muonekano lusaka huwezi kuilinganisha na dar es salaam? Achilia mbali j'burg? Nlijaribu kuwauliza wenyezi wakasema serikali ilichofanya ni kuondoa sifuri kwenye noti zao, baadala ya 10,000 wakatoa sifuri 2 ikawa 100, 5,000 ikawa 50, zamani ulihitaji kutoa kwacha 3000 kununua soda leo unatoa kwacha 3, nasikia mpaka msumbiji nao wameondoa sifuri kwenye noti zao na mitikashi yao leo sio ile ya zamani, kama issue ni kuondoa sifuri kwa nini na sisi tusiondoe sifuri na noti kubwa ikawa 100?
 
na kweli tusaidiane ...niliwahi kwenda Maputo nikachanganyikiwa eti wanaondoa sifuri ! ukichanganya na lugha gongana nilishindwa hata kupata pipi ,kwan sikuelewa Rand /Mitksh zinabadilshwaje !
 
Hawa Zambia walichokifanya ni kudrop '000' lakini bado ZAR iko juu kithamani ukilinganisha na Kwacha.

Ina maana kama zamani walikuwa wakinunua kitu kwa ZMW 1,000, kitu kile kile kwa sasa kitakuwa kinauzwa kwa ZWM 1, ila hiyo haimaanishi kwamba thamani ya pesa yao imepanda.
 
Majuzi nimerudi toka south africa nikipita nchi za zambia na zimbabwe, kilichonishangaza ni thamani ya kwacha ya zambia kuwa juu kuliko rand ya south africa, je? Ni kweli zambia wana uchumi mzuri kuliko tanzania , kenya ama south africa? Wakati rand 1 ni sawa na t' sh. 150, kwacha 1 ni sawa na t'sh. 300, ni nini kimefanya zambia wawe juu hivi? Sababu ya shaba? Mbona south africa wana gold? Ambayo kwa uelewa wangu ni zaidi ya shaba? Mbona hata kwa muonekano lusaka huwezi kuilinganisha na dar es salaam? Achilia mbali j'burg? Nlijaribu kuwauliza wenyezi wakasema serikali ilichofanya ni kuondoa sifuri kwenye noti zao, baadala ya 10,000 wakatoa sifuri 2 ikawa 100, 5,000 ikawa 50, zamani ulihitaji kutoa kwacha 3000 kununua soda leo unatoa kwacha 3, nasikia mpaka msumbiji nao wameondoa sifuri kwenye noti zao na mitikashi yao leo sio ile ya zamani, kama issue ni kuondoa sifuri kwa nini na sisi tusiondoe sifuri na noti kubwa ikawa 100?

Kwakukusaidia lazma kwanza uelewe si mara zote thamani ya shilingi kua ndogo au kuwa juu kwenye nchi inakua kiashiria cha moja kwa moja kwamba uchumi katika nchi hio uko juu au uko chini,lakini pia inategemeana hii shilingi imeshuka kwa kiasi gani,
Wakati mwingine shilingi ya nchi kua chini ukilinganisha na nchi nyingine hasa kama kuna muingiliano wakibiashara katika nchi hizo,inakua ni kichocheo ktk biashara za nje(exportation) sambamba na ku discourage importation ya bidhaa kutoka nje ili kulinda soko la ndani kwenye nchi ambayo value ya currency yake iko chini.
Kama utauza nje inamaana utauza kwa pesa ya huko ambayo thamani yake ni kubwa nchini mwako hivyo utakapo rudi kununua bidhaa nchini mwako utapata bidhaa nyingi.
Na atakae kuja kuuza bidhaa(importation) kwenye nchi ambayo thamani ya pesa iko chini sana itam discourage kwani atauza kwa pesa ya nchi hio na atakaporudi nchini mwake ku exchange currency ili kununua tena bidhaa ile pesa thamani yake ni ndogo.
Kama ni mfuatiliaji wa mambo mfano mzuri ni China ambayo mwaka juzi ilishusha thamani ya shilingi yake(currency devaluation) kwa makusudi ili kuchochoa biashara ya nje(expotation trade) kitu ambacho kilileta mgogoro na nchi za magharibi kwani unapo import nchini mwao wakati thamani ya pesa yao ipo chini hupati faida.
Mara nyingi hii hufanywa ili kulinda viwanda vya ndani.
Ila kama currency inashuka sana hapo ndipo kunakua na tatizo.
 
Kuna faida na hasara za thamani ya fedha kuwa juu au chini, na ni kweli kwamba thamani yafedha kuwa juu si kwamba na uchumi wa nchi husika uko juu, Thamani ya fedha ya kama sikosei Qatari iko juu vibaya mno kuliko USD, lakini uchumi wa Qatari unazidiwa na hata jimbo moja la Calfonia,

Ish ya dha kuwa juuhufanywa na benk kuu, na mara nying kwa nchi za kwetu huwa haina faida sana
 
Kwakukusaidia lazma kwanza uelewe si mara zote thamani ya shilingi kua ndogo au kuwa juu kwenye nchi inakua kiashiria cha moja kwa moja kwamba uchumi katika nchi hio uko juu au uko chini,lakini pia inategemeana hii shilingi imeshuka kwa kiasi gani,
Wakati mwingine shilingi ya nchi kua chini ukilinganisha na nchi nyingine hasa kama kuna muingiliano wakibiashara katika nchi hizo,inakua ni kichocheo ktk biashara za nje(exportation) sambamba na ku discourage importation ya bidhaa kutoka nje ili kulinda soko la ndani kwenye nchi ambayo value ya currency yake iko chini.
Kama utauza nje inamaana utauza kwa pesa ya huko ambayo thamani yake ni kubwa nchini mwako hivyo utakapo rudi kununua bidhaa nchini mwako utapata bidhaa nyingi.
Na atakae kuja kuuza bidhaa(importation) kwenye nchi ambayo thamani ya pesa iko chini sana itam discourage kwani atauza kwa pesa ya nchi hio na atakaporudi nchini mwake ku exchange currency ili kununua tena bidhaa ile pesa thamani yake ni ndogo.
Kama ni mfuatiliaji wa mambo mfano mzuri ni China ambayo mwaka juzi ilishusha thamani ya shilingi yake(currency devaluation) kwa makusudi ili kuchochoa biashara ya nje(expotation trade) kitu ambacho kilileta mgogoro na nchi za magharibi kwani unapo import nchini mwao wakati thamani ya pesa yao ipo chini hupati faida.
Mara nyingi hii hufanywa ili kulinda viwanda vya ndani.
Ila kama currency inashuka sana hapo ndipo kunakua na tatizo.

maelezo mazuri, naona umeni pre-empty nilichotaka kucomment. ila kuongezea tu, currency depreciation/ devaluation is not necessary bad to the economny. kuna nchi nyingine zinakuwa na mikakati ya ku-weaken currency yao kwa ajili ya kuprotect their trade balances, na pia kama kichocheo cha wao kuuza zaidi nje, wakati huo kupunguza manunuzi ya bidhaa kutoka nje ya nchi

depreciation inafanya domestic goods to be cheap compared to foreign goods. ili depreciation kuwa-work inadepend kwny
  • import to GDP ratio ya nchi. kwa nchi ambayo kiasi kikubwa cha bidhaa zinazotumika nchini zinakuwa imported, inaweza isiwe good strategy. maana hai-make sense kuzuia bidhaa zisiingie kutoka nje wakati nchi haina uwezo wa kuzalisha hizo bidhaa. matokeo yake (kwenye uchumi) wanaita ni consumer loss.
  • export. kama nchi haina bidhaa za kuuza nje, ina maana hakutakuwa na significant increase ya income from the export sector
  • fall of import bill inatakiwa kuwa kubwa (since import ni function ya price na quantity) kwamba amount ya imports inatakiwa ipungue sana kuliko ongezeko la price za foreign goods linalotokana na depreciation.

gimmy's hapo juu katoa mfano wa china, ila Japan nayo imekuwa ikitumia hiyo strategy ili kuongeza competitiveness yake kwenye world market. USA imekuwa ikilalamika khs Japan ku-weaken currency yake, hata ile Asian crisis ya 1990s, japan na china zili-trigger ile crisis

in short, kitu cha muhimu kwenye currency siyo thamani yake ukilinganisha na currency(ies) nyingine, bali ni how stable the currency is. kama thamani ya fedha inaflactuate mara kwa mara (haipo stable) ni tatizo zaidi kwa uchumi. people cant make longterm decisions kwa kutumia hiyo currency. hapo ndio unakuta mikataba yote watu wanaingia kwa USD
 
Dah.. nilikuwa nasinzia sana kwenye lecture za International Economics...
 
Back
Top Bottom