Mliowahi kufanya biashara za kuuza duka la Mangi naombeni ushauri

Mliowahi kufanya biashara za kuuza duka la Mangi naombeni ushauri

Wataalamu wa izo kaz apa bongo ni waha,wachaga na wasukuma hao wote wanajulikana kua ni wakulima wazuri na watu wa dili chafu (waha na wasukuma hulima na kuchuuza mashamban na kuja kuuza madukan mwao ukija wachaga hawa ndio wazee wa dili na magendo na michongo)
 
Wadau ambao mshawai kufanya au bado mnafanya biashara ya duka la mangi katika mitaa mbalimbali DSM huwa zinamuhitaji mtu awe na mtaji wa kiasi gani

Mbinu na strategy zipi zinatumika kukua kwa haraka zaidi
Duka la Mangi ndio kila kitu kwangu....toka kitambo,,,,kwa Dar kama upo kwenye makazi mapya inalipa zaidi,,,,muhimu zingatia namna ya kupata vitu(siku hizi waletewa kila kitu dukani) jitahidi kuweka vitu mixer,,,hasa vya genge...genge linaleta hela nzuri sana...pia weka pombe mixer,,,,,,
 
Usiwe na haraka ya faida, hakikisha uwe na kipato kingine cha kujiendesha. Maisha yako yasiegamie duka mpaka hela ya mahitaji kila siku itoke hapo.

PIga hesabuza kufunga hesabu kila siku ile akili yako isiwaze kuhusu faida upate ya kuchukua. Faida kuu kama biashara ikishika angalia mwisho wa mwezi tu. Utapiga heaabu toa faida na mtaji na ujue hasara.​
 
Acheni kukatisha watu tamaa.

Tafuta sehemu yenye mzunguko mkubwa, kama wadau walivyosema hapo juu faida yake ni ndogo sana.

Ila, kama unapata mzunguko mkubwa faida utaiona.

Mimi naifanya hii biashara japo siitegemei kunilisha, nimemuweka wife.

Hizi hapa bidhaa zinazotoka sana na faida zake.

Mafuta ya kula 20 ltrs, bei yake 90,000 jumla, bei ya rejareja ni 5200x20=104,000 elfu 14,000 faida, kama unapata mzunguko mzuri unauza mpaka ndoo 2 au 3 kwa siku.

Sukari 25kgs 71000 jumla, bei rejareja 3200x25=80,000, elfu 9,000 faida

Sembe 25kgs 27,000 jumla, bei ya rejareja 1400x25=35,000 elfu nane faida.

Maji sansum 1.8 cartoon moja jumla elfu nne, bei ya rejareja 1,000x6=6,000 faida elfu mbili.

Maji afya 1.6 ltrs bei ya jumla 3400, rejareja 800x6=4800 faida 1400.

Hivyo ni baadhi tu, vitu ni vingi sana. Mkuu usikatishwe tamaa humu, tafuta sehemu yenye mzunguko mkubwa. Mwanzo huwa mgumu pambana mkuu utafanikiwa.
 
Kama unatafuta sehemu ya kupotezea muda fungua.
NB: ukae ww dukani hapo utatoboa.
 
Ukiuza 100,000 faida10,000
Ukiuza 200,000 faida 20,000
Ukiuza 300,000 faida 30,000
Unataka Nini tena??
Wewe kazi yako ni kupambana kukuza mauzo yako, na uwe na nidhamu ya pesa tu(. Nidhamu ya pesa ni Kila mahali)

Nb: Mchaga hawezi kung'ang'ania kitu kisichokua na faida....!!! Stukeni....! Na huu uvumi wa duka la mangi halilipi wanauanzishaga wao. Au ukiona mtu anasema duka halilipi hajapata site nzuri.
Wachaga wanatajirikia kwenye maduka alafu nyie mnadanganywa eti duka halilipi?
 
Back
Top Bottom