Acheni kukatisha watu tamaa.
Tafuta sehemu yenye mzunguko mkubwa, kama wadau walivyosema hapo juu faida yake ni ndogo sana.
Ila, kama unapata mzunguko mkubwa faida utaiona.
Mimi naifanya hii biashara japo siitegemei kunilisha, nimemuweka wife.
Hizi hapa bidhaa zinazotoka sana na faida zake.
Mafuta ya kula 20 ltrs, bei yake 90,000 jumla, bei ya rejareja ni 5200x20=104,000 elfu 14,000 faida, kama unapata mzunguko mzuri unauza mpaka ndoo 2 au 3 kwa siku.
Sukari 25kgs 71000 jumla, bei rejareja 3200x25=80,000, elfu 9,000 faida
Sembe 25kgs 27,000 jumla, bei ya rejareja 1400x25=35,000 elfu nane faida.
Maji sansum 1.8 cartoon moja jumla elfu nne, bei ya rejareja 1,000x6=6,000 faida elfu mbili.
Maji afya 1.6 ltrs bei ya jumla 3400, rejareja 800x6=4800 faida 1400.
Hivyo ni baadhi tu, vitu ni vingi sana. Mkuu usikatishwe tamaa humu, tafuta sehemu yenye mzunguko mkubwa. Mwanzo huwa mgumu pambana mkuu utafanikiwa.