Mliowahi kukopa benki na badae kuachana na mikopo na kubaki na mitaji yenu tupeane ujuzi nasi tujikwamue

harder king

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
3,970
Reaction score
6,907
Habari za mda huu wanajamvi!

Sina shaka maana na jua kwa rehema za MUNGU mmeamka salama na baadhi tiari mpo makazini kuijenga nchi yetu.

Kwa wale ambao hawapo poa kiafya na kiakili Mungu awatie nguvu na afya mpate kurejea mapema vitani

Kama kichwa cha thread kinavyosema, mliowai kukopa mikopo mikubwa bank na baadae kuirejesha na kutokukopa tena mlitumia mbinu gani?

Binafsi ni mhanga wa hili janga kwa zaidi ya miaka5.
Nilikopa ili kuupa nguvu mtaji wangu uliokua mdogo mwanzoni sikupata tabu kurejesha..tatizo ni kwamba kila mwaka najikuta nashawishika kuongeza ukubwa wa mkopo

Na kwakua dhamana yangu inaruhusu basi ata jamaa wa bank huongeza ushawishi wa kukuongezea
Shida ni kwamba tangu mwaka jana nimeanza kula msoto usiowakawaida.

Mkopo nliokua nao nilirejesha kwa tabu sana,nliapa nikimaliza sintakopa tena,kumbe nlikua najidanganya tu.

Yaan baada ya kumaliza nilikaa bila mkopo kwa miezi miwili tu nikarudi tena kujisalimisha waniokoe.

Hapa nilipo nipo kwenye tabu na mateso ya marejesho yani biashara inavyokua ngumu ndio kabisa naiona siku ya rejesho kama siku ya ukumu.
Imebidi nisimamishe shughuli zingine ili niweze kuinusuru dhamana yangu.

Ukweli ni kwamba mpaka sasa sijakutana na mtu binafsi aliejingiza kwenye mikopo akatoka huko salama,nimeona matajiri wengi wenye mitaji mikubwa lakini mtego wa kujinasua kwenye banio la mabenk limewashinda.

Wengi wao hadi mauti yanawakuta na kuacha benk ikiwadai tena madeni yasiolipika kiraisi.

Vijana wengi wameaga mashindano baada ya kushindwa kurejesha mikopo na dhamana zao kupigwa mnada.

Je wewe uliefanikiwa uliwezaje?
Na nini kinachofanya sisi tushindwe?

Hapa hatuwaongelei wale wanaokopa kwa kutumia salaryslip zao.

Onyo: Wale mliozoea kutoa povu kavulieni nguo hapa sio mahala pake.

Karibuni.
 
Mkopo huwa unatija kama faida ya biashara unayoipata na asilimia 75% - 100%, ila kama biashara yako faida ni ndogo sana kuzidi mkopo basi kutoka kwenye mikopo ni ngumu sana, binafsi sijawahi kukopa bank nadunduliza nilichonacho, ila wengi waliokopa wameishia kwenye madeni zaidi na kupoteza hata mali zao walizozitafuta kwa jasho, ila wanaonufaika ni wale wanaochukua na kufanya biashara(deal) za faster, yani unamteja anataka mzigo wa milioni 100 na huna hiyo pesa unachukua mkopo unamletea mzigo anakulipa unarudisha bank pesa yako faida unatia kibindoni.
 
Hyo biashara ya faster ipo vizuri ila ni ngumu kupata hlo deal mkuu.
Kingine sio kwamba mikopo tunayochukua hailipi maana wengi tulichukia mikopo tukiwa tiari tuna mtaji kiasi so mkopo tulitumia kama buster

Shida ni kwamba kila unaporejesha unaitaji kujibust tena na hii hutupa ugumu wa kujinasua huko

Wakati mwingine nafikia kuwaza labda mabank kuna mambo hutufanyia yasio ya kawaida kiasi kwamba kila tukiwaza kujitoa kwao inakua ngumu mpaka pale tunapo shindwa na dhamana yetu kuchukuliwa ndio inakua mwisho wao na sisi.
 
Shida nyingine ni aina ya uwekezaji tunao ufanya Mara nyingi tunawekeza kimazoea

Mfano una biashara yako imesimama vizuri unakopa na kulipa bila shida yoyote kosa kubwa unapo anza kuongeza miradi afu teamwork yako unachukua sijui binam mara mdogo wako kisa hana kazi unawaweka pale wao wanakuona umefanikkiwa tayari hivyo umewaleta pale na wao watoke kimaisha lkn kumbe wewe umekopa pesa hizo
 
Huu ni ukweli mkuu japo mm kumuajiri ndugu siwezi wao uniona nina mafanikio bila kujua kilichopo nyuma ya pazia

Ukwel kwenye kazi inayoendeshwa kwa mkopo ukimuingiza huko ndugu umekwisha japo sio wote
 
[emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] daaa umeniliza sana,ndugu ndugu ndugu sina hamu nao.
 
Huu ni ukweli mkuu japo mm kumuajiri ndugu siwezi wao uniona nina mafanikio bila kujua kilichopo nyuma ya pazia

Ukwel kwenye kazi inayoendeshwa kwa mkopo ukimuingiza huko ndugu umekwisha japo sio wote
Sio wote ila 99.9% wako hivyo
 
Huu ni ukweli mkuu japo mm kumuajiri ndugu siwezi wao uniona nina mafanikio bila kujua kilichopo nyuma ya pazia

Ukwel kwenye kazi inayoendeshwa kwa mkopo ukimuingiza huko ndugu umekwisha japo sio wote
100% correct
 
Huu ni ukweli mkuu japo mm kumuajiri ndugu siwezi wao uniona nina mafanikio bila kujua kilichopo nyuma ya pazia

Ukwel kwenye kazi inayoendeshwa kwa mkopo ukimuingiza huko ndugu umekwisha japo sio wote
Na wakati mwingine sio tu ndugu bali aina ya biashara na usimamizi wake
 
Hongera sana mkuu kwa kuwa mpambanaji na pole kwa marejesho. Hakuna kizuri bila ugumu. Nnachojua principle moja ya kukopa ni kwamba usikope zaid ya 50% ya mataji wako halisi. Hapa itakufanya kwanza usifanyerejesho kwa presha,pili biashara itakua kwani utajumua mzigo unaozunguka ili kufanya marejesho kwa wakati.
Biashara na mkopo sio kitu kibaya kikubwa balansi ratio ya mkopo:mtaji wako halisi
 
Pia usikope kama mzunguko wako unajiweza. Yaani hauna upungufu wa bidhaa dukani then usikope. Kuna watu wanamsimamo wa kutokopa na akikopa anakopa bidhaa na sio hela. Hivyo unadunduliza mtaji wako na pia ukikopa bidhaa mara nyingi hakuna riba ni wewe tu kukimbizana na kuuza ili urudishe hela za wenye mzigo.
Hii njia nzuri sana hasa kwa sisi wenye mitaji midogo ingawa kumpata mtu wa kukupa mzgo kwa mali kauli ni lazma muwe mmefanyabiashara kwa muda mnajuana.
 
Nashukuru mkuu!
Ni kweli biashara na mkopo sio maadui ila tatizo ni ugumu wa kujitoa kwenye mkopo ili ubaki na mtaji wako

Mfano una ml10 ukaenda kopa ml5 baada ya rejesho kuisha ni ngumu kutorudia kukopa...yani ipo kama kamari jinzi unavyokula unataka kula zaidi

Mwisho wasiku wengi wameliwa adi kile kilichokua kwao
 
Mkopo ni kama some sort of addiction, mtu akishaanza kuacha kazi sana. Matajiri wengi almost 90% wana run biashara kwa mikopo tena mikubwa sana ambayo sometimes hailipiki. 2004 mzee wangu akiwa nazo alikuwa na marafiki kma kina gachuma, lameck airo,patel na wengine nilijifunza wengi huendesha biashara kwa mikopo.

The difference ni kwamba wenzetu cjui wanafanyeje kuishi na madeni miaka yote mpk wanakufa na vizazi vinaendeleza madeni. Mpk leo i dont what went wrong mzee alikuwa na mtaji wa 800 milion back 2000 ilikuwa pesa kubwa tu kufikia 2005,alikuwa n 500 milioni fixed Account crdb,mpk benki ikamzawadia land cruiser mpya coz alikuwa akiweka pesa hatoi!

Wakawa wanamfuata mzee kukopa yaani anabembelezwa kabisa kukopa, hapo ndipo tatizo lilipoanza. To make the story short cjui kilitokea nn kufikia 2009 ,mzee alifilisiwa vibaya sana hawana hata chembe ya huruma walifilisi hadi kijiko. Infact tulitolewa kwenye nyumba na nguo zetu tu mpk leo mzee hayuko sawa,ana presha, kisukari ,magonjwa ya moyo yaani utadhani yeye ni benki ya magonjwa ! Hao watu watamu ukiwa unalipa ukiyumba utajuta kuzaliwa, i learned sitakuja nikope hata mia benki better litle with peace of mind
 
Pole sana ndugu
 
Poleni sana mkuu.

Hii kitu inanichanganya sana,mikopo mingi ina mwisho mbaya na wa kutisha,

sijawai sikia mwisho mzuri wa mkopo ila hatuna namna maana nasi tunaitaji vitu vizuri kama wengine japo hatujui tutadumu navyo au lah
 
Unapoanza biashara epuka mikopo ikianza kukua kopa kidogo sana kwa tahadhari kubwa ,ukikua sana asee kopa kwa ushauri wa wataalamu tuu Tena nyingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…