antimatter
JF-Expert Member
- Feb 26, 2017
- 47,274
- 126,778
Duh! Mkuu pole sana.. Very interesting story ingawa hukusema alikopa kiasi gani..Mkopo ni kama some sort of addiction, mtu akishaanza kuacha kazi sana. Matajiri wengi almost 90% wana run biashara kwa mikopo tena mikubwa sana ambayo sometimes hailipiki. 2004 mzee wangu akiwa nazo alikuwa na marafiki kma kina gachuma, lameck airo,patel na wengine nilijifunza wengi huendesha biashara kwa mikopo.
The difference ni kwamba wenzetu cjui wanafanyeje kuishi na madeni miaka yote mpk wanakufa na vizazi vinaendeleza madeni. Mpk leo i dont what went wrong mzee alikuwa na mtaji wa 800 milion back 2000 ilikuwa pesa kubwa tu kufikia 2005,alikuwa n 500 milioni fixed Account crdb,mpk benki ikamzawadia land cruiser mpya coz alikuwa akiweka pesa hatoi!
Wakawa wanamfuata mzee kukopa yaani anabembelezwa kabisa kukopa, hapo ndipo tatizo lilipoanza. To make the story short cjui kilitokea nn kufikia 2009 ,mzee alifilisiwa vibaya sana hawana hata chembe ya huruma walifilisi hadi kijiko. Infact tulitolewa kwenye nyumba na nguo zetu tu mpk leo mzee hayuko sawa,ana presha, kisukari ,magonjwa ya moyo yaani utadhani yeye ni benki ya magonjwa ! Hao watu watamu ukiwa unalipa ukiyumba utajuta kuzaliwa, i learned sitakuja nikope hata mia benki better litle with peace of mind
Kwa ujumla mikopo ina kanuni zake.
Kwanza, usikope for biashara mpya unless ni long term.
Pili, usikope kwa kushawishiwa, kopa kama biashara inahitaji hvyo, tena kiasi sahihi, na kuna hesabu zake.
Unaeza kuta mtu ana biashara ya mtaji wa kama m30, biashara inahitaji jeki (working capital) ya 4m, anaenda kuchukua 15m. Maana yake 11m itakuwa idle au itatumiwa kwny mambo tofauti. Deni kama hilo halilipiki kamwe.
Pia, deni ya muda mfupi ikizidi 20% ya mtaji inakuwa kama kamari.
Kingine, usithubutu kuweka dhamana nyumba unayoishi, tumia kiwanja, shamba au nyumba ya ziada. Hii itakuepusha na ugonjwa wa moyo.
Kumbuka pia, kama umeamua kujilipua na mkopo, ni afadhali benki (au Saccos za jumuia kwa mikopo midogo) kuliko ki-microfinance cha mtu.. wanasema kwny hizi micro, mkopeshaji akipenda dhamana uliyoweka ataichukua tu.. Na pia usisahau kuelewa na kujiridhisha na masharti yote ya mkopo kabla ya kujifunga kwny mkataba