Mliowahi kukopa benki na badae kuachana na mikopo na kubaki na mitaji yenu tupeane ujuzi nasi tujikwamue

Mliowahi kukopa benki na badae kuachana na mikopo na kubaki na mitaji yenu tupeane ujuzi nasi tujikwamue

Duh! Mkuu pole sana.. Very interesting story ingawa hukusema alikopa kiasi gani..
Kwa ujumla mikopo ina kanuni zake.
Kwanza, usikope for biashara mpya unless ni long term.
Pili, usikope kwa kushawishiwa, kopa kama biashara inahitaji hvyo, tena kiasi sahihi, na kuna hesabu zake.
Unaeza kuta mtu ana biashara ya mtaji wa kama m30, biashara inahitaji jeki (working capital) ya 4m, anaenda kuchukua 15m. Maana yake 11m itakuwa idle au itatumiwa kwny mambo tofauti. Deni kama hilo halilipiki kamwe.
Pia, deni ya muda mfupi ikizidi 20% ya mtaji inakuwa kama kamari.
Kingine, usithubutu kuweka dhamana nyumba unayoishi, tumia kiwanja, shamba au nyumba ya ziada. Hii itakuepusha na ugonjwa wa moyo.
Kumbuka pia, kama umeamua kujilipua na mkopo, ni afadhali benki (au Saccos za jumuia kwa mikopo midogo) kuliko ki-microfinance cha mtu.. wanasema kwny hizi micro, mkopeshaji akipenda dhamana uliyoweka ataichukua tu.. Na pia usisahau kuelewa na kujiridhisha na masharti yote ya mkopo kabla ya kujifunga kwny mkataba
Mkuu... Unaweza ukatupa hizo kanuni za mikopo? Just briefly.
 
Watu Wauchumi wanasema Hivi. Mikopo siyo Njia Sahihi ya Kujikwamua Kimaisha...

Kama Una akili Fikiria Hili. Mie huwa nakwepa sana Mikopo
Vipi kama ni mkopo usio na riba kabisa?
 
Kama huna mikosi benki ni mkombozi ukicheza kwa mahesabu makali . Miradi mikubwa mara nyingi ni mikopo na watu wanatoka .
 
Nilishaachana na mikopo nikiapa kuwa, mtu akimiona nakopa tena, anichinje kwa msumeno ila sasa nahisi kuitamani, tamani!
 
Yaan Leo nimetoka kupiga passport tayar Kwa kuelekea NMB kukopa, nimesoma comments za wadau Kwa makini saana.Nimejifunza ifuatavyo;-
1. Kopa Kwa lengo maalum.
2. Kopa Kwa lengo la kibiashara ili uweze kulipa P+I na hatamaye kubak na faida.
3. Hata Kama unauwezo wa kukopa kiasi kikubwa benk lakin kopa kiasi kile tu unachohitaji.
Kutokana na hayo itabid Kwanza kesho nihairishe kwenda benk Hadi hapo nitakapojika amri nyingine.😃😃😃
 
Kwanza kabisa kukopa si kubaya=ni sawa na kuchukua pesa za watu na kufanyia kazi so ni kitu kizuri.Ukitoka kwenye mkopo maana yake kiwango chako cha kukua na kuzalisha ni kibaya.Kuna aina nyingi ya mikopo ikiwamo overdraft ambao ndio mkopo mzuri kwani huu unatumia na kulipia kile kiasi unachotaka.Kwa kawaida mfanya biashara anatakwa akikopa mkopo mkubwa ambao sio fixed basi uende kwenye asset au capita expenditure na akikopa mkopo wa operational basi uwe overdraft.Sasa ndugu yangu mkopo wako umeenda kwenye asset purchase ama umeenda kwenye operations?Ukinijibu hilo nitakupa njia ya kujinasua
 
Baba unavosema operational unamaanisha nin? Nafiriki nianzie Kwanza hapo kabla sijakujibi tayar Kwa kupata mawazo toka kwako.
 
Naomba mnipe ufafanuzi zaidi wajuzi,,, nimekopa benk flani nimelipa mkopo wangu kwa asilimia 70% Biashara imeyumba kidogo na nimewandikia barua kuwa mzunguko umekuwa mdogo je hili linaweza kuniletea shida? Kama kuuza dhamani nk?
kama unaona utayumba sana omba wakufanyie restructure ya mkopo rejesho lipungue Ingawa utalipa hela nyingi ila itakuwa ni afadhali kuliko kuhatarisha dhamana. Ni benki gani hiyo
 
Yaan Leo nimetoka kupiga passport tayar Kwa kuelekea NMB kukopa, nimesoma comments za wadau Kwa makini saana.Nimejifunza ifuatavyo;-
1. Kopa Kwa lengo maalum.
2. Kopa Kwa lengo la kibiashara ili uweze kulipa P+I na hatamaye kubak na faida.
3. Hata Kama unauwezo wa kukopa kiasi kikubwa benk lakin kopa kiasi kile tu unachohitaji.
Kutokana na hayo itabid Kwanza kesho nihairishe kwenda benk Hadi hapo nitakapojika amri nyingine.😃😃😃
Ongezea na kujua aina ya mkopo unaotaka kuchukua,kuna mtu alichukua overdraft akaitumia kama term loan , deni linamsumbua tu,
 
A
Narudia tena, wote manolalamika kuwa Awamu hii hakuna pesa, mlikuwa wapiga deal, pesa zimerudi kwa watu waliokuwa wanazipata kihalali, ridhika na hicho unachopata, ndicho kilitakiwa kuwa halali yako tangu Awamu zilizotangulia.
Acha kujitoa ufahamu wewe.
 
Kwanza kabisa kukopa si kubaya=ni sawa na kuchukua pesa za watu na kufanyia kazi so ni kitu kizuri.Ukitoka kwenye mkopo maana yake kiwango chako cha kukua na kuzalisha ni kibaya.Kuna aina nyingi ya mikopo ikiwamo overdraft ambao ndio mkopo mzuri kwani huu unatumia na kulipia kile kiasi unachotaka.Kwa kawaida mfanya biashara anatakwa akikopa mkopo mkubwa ambao sio fixed basi uende kwenye asset au capita expenditure na akikopa mkopo wa operational basi uwe overdraft.Sasa ndugu yangu mkopo wako umeenda kwenye asset purchase ama umeenda kwenye operations?Ukinijibu hilo nitakupa njia ya kujinasua
Mkuu ukisema operation unamanisha nn
 
Iyo mikopo tuna ngangania tu, ila Mwenyezi Mungu kayakataza hayo...(riba) Familia nyingi leo zinapitia wakati mgumu sana. Wazungu watatuletea mengi sana...
Mkuu mbona ata barabara unayotumia ni ya mkopo?

Ata uwe nani maisha bila mkopo ni uongo! labda uwe umevikuta au umeamua kufa maskini kitu ambacho ata MUNGU mwenyewe hapendi!
 
Back
Top Bottom