Mliowahi kupigana darasani leteni ushuhuda wenu hapa

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Mkuu alikubana kila idara[emoji1787][emoji1787]

Alitawala sana,
Miaka ile wanafunzi wengi walikuwa na maumbo makubwa tofauti na kipindi hiki, in short alikuwa ni kipande cha mtu.
 
Nlimtafuta ila sikufanikiwa ku revenge.. company ake ilkua ni majitu ya miraba minne.. kwa hiyo nikawa nakosa ujasiri wa kum face na baadae alikuja kuhama shule.
[emoji1787][emoji1787][emoji23]
Dah school moments noma sana
 
Nilizichapa na Ticha wa sayansi uvumilivu ulinishinda alikua anapiga vidole vyetu kwa rula. Nilimngata meno nikiwa nalia nikakimbilia juu ya madawati. Akija huku nahamia upande mwingine hakuna aliyenigusa maana niliku nishashika bikali.

Huyu ticha ni best yangu sana tukikutana nampa heshima yake.. na tunapiga stori vizuri tu.
...Bro Himid alinipiga ngumi ya sikio darasani nikaanguka chini nikalia weeee hapo nikaamka nikachukua bikali nikamfuata..Niliizamisha bikali yote mgongoni. Toka siku hiyo hakunigusa na nibest yangu sana
 
😄😄😄 Lkn nlivuliwa umonitor kw kichapo kikali kw staff nzim na kuzungushw kila darasa na kutangazw assemble
Ahahahahaha ukapewa cheo cha Gaidi kama Hamza au haramia?
 
Hilo pambano gani la masaa mawili aisee au mlikuwa mnakabana sana 😅! Nakozi za maana haziwezi kumaliza dakika 40 lazma mmoja aombe yaishe.

Hio ilikuwa inaitwa “parling” au kuzipanga “mtu mbike!” Maeneo ya Morogoro Golf Club pale ndio ilikuwa eneo la maangamizi.
 
Aisee darasa la 7 nakumbuka nilipigana na mwalimu, alikuwa kijana kijana halafu anapenda sifa sasa siku hiyo kaingia kakuta watu wanapiga kelele, mimi naye ndio naingia ndani nilikuwa nimepitiliza mapumziko maana kipindi hicho walimu hawafundishi tena, tunasubiria mtihani wa taifa.

Sasa mwalimu akaniwakia na kutaka kunichapa eti mimi ndio kilaza kabisa hata kufuata kengele siwezi, ile karusha fimbo anichape mkononi nikaidaka sijui ni ujinga gani ukaniingia nikaona huyu jamaa mbona namuweza nikaanza purukushani naye darasani nikamzidi nguvu sijui aliona aibu nikamgaragaza chini nikakimbia🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️.

Ilikuwa katikati ya wiki sasa kurudi shule kesho yake aisee walimu walinikomesha nilipelekwa ofisini kuna wamama hao walinishikilia mikono wengine walikuwa wanachapa bakora nafikiri nilipigwa kwa muda zaidi ya saa 2 na walimu wa shule nzima, yaani wengine walikuwa wanachapa wanaenda kunywa chai wakirudi wanasema hili bado lipo wanachapa, nililia nikaachwa nikae kabisa katikati ya ofisi anayekuja anacharaza viboko anaondoka, nilikoma aisee
 
Hilo pambano gani la masaa mawili aisee au mlikuwa mnakabana sana 😅! Nakozi za maana haziwezi kumaliza dakika 40 lazma mmoja aombe yaishe.
Umenikumbusha kuna masela walikamatwa wanapigana na ticha darasani, akawaita mbele pale pale darasani wazipige nakozi kavu kavu halafu yeye ndio kama refa, ilikuwa kama dakika 5 msela alizidiwa akaanza kulia maana zilikuwa zinapigwa unasikia sauti kama muvi za wachina kila mtu yupo kimya hamna kupiga kelele unajua kabisa hiyo imengia vilivyo usoni, ticha akamwambia mshindi aende akakae halafu yule aliyepigwa akamcharaza viboko 🤣
 
Hahahahahah ticha alikuwa muhuni sana huyo! Hilo pambano lilikuwa rasmi kabisa bila kiingilio 😅! Hahahah ningeinjoy sana yani.
 
Shule zetu za vidumu na mfagio mambo haya ya ngumi yalikuwa Kawaida sana kutokea.

Nimeshuhudia mechi nyingi sana za ngumi,mechi inaandaliwa mapema,njiani wakati wa kurudi ndio muda wenyewe.

Mimi nilikuwa si mtu wa vurugu japo nishawahi piga mtu katika harakati za kujinasua,,alinivamia anipige kwa chuki zake tu..
Nikamtandika.
 
Kuna dogo mmoja alikuwa anaitwa Hery barton mjuaji sana nakumbuka alizichapa na mchizi mmoja anaitwa Daniel Msuya! Sikuhio mapema sana kabla ya assembly saa 12 asubuhi.

Aisee zile ngumi zilikuwa level za kimataifa yani! Hamna kushikana hapo ni nako 2 nako yani ikipenya unaskia shavu limeitika fyo.toooh. Pale ndio tulipata taste ya kina Tyson kabisa huku hery barton akila nakoz za kwenda maana Daniel alikua na utulivu sana kwenye kuzipachika.
 
Hahahahahah ticha alikuwa muhuni sana huyo! Hilo pambano lilikuwa rasmi kabisa bila kiingilio 😅! Hahahah ningeinjoy sana yani.
Ticha alitumia ubunifu wa hali ya juu 🤣
 
Raha ya ngumi aisee ziwe ni nakoz wakishaanza kukabana inakuwa haina ladha tena, atakayebahatisha kumkaba mwenzake vilivyo basi ndio anakuwa mshindi ili zikirushwa kwa mpangilio aisee ni zaidi ya muvi na anayeshinda anaheshimika zaidi 🤣
 
Nakumbuka wakat nipo darasa la nne nilikuwa napenda ugomvi sana yaan mm mda wote nimejiandaa kimapambano niko na t shirt na kivaa ndan ya shart kwa jili ya mapambano.

Sasa siku hiyoo nikaingia mkenge kwa lijaama tulikuwa tuna lita taralila limerudia darasa alaf lirefu ebwana eeh liliniangusha chini likanipiga ngumi za pua kwa mara ya kwanza natolewa damu
Yaan mpk narudi home nafikiria lile jamaa ikabidi nikakae nyuma ya nyumba maumivu ya poe
 
Mda huu tulikuwa tunauita “after bell rings” yani baada ya kengele ya mwisho ya kutoka shule wahuni wanajimwaga golf club kufundishana heshima na adabu!

Nakumbuka kuna mtoto mmoja wa kihindi anaitwa Huzeifa bonge hivi alijimix kwa mtoto wa kiluguru Ramadhani hussen amevimbia chini kama twaha kiduku! Asee alichofanywa yule ponjoro ilikuwa ni bad news 😅 aliondoka kaoteshwa vinundu kaiva kama jezi ya simba 😅
 
Raha ya ngumi aisee ziwe ni nakoz wakishaanza kukabana inakuwa haina ladha tena, atakayebahatisha kumkaba mwenzake vilivyo basi ndio anakuwa mshindi ili zikirushwa kwa mpangilio aisee ni zaidi ya muvi na anayeshinda anaheshimika zaidi 🤣
Mzee kimya kilitawala na mashabiki hatukuwa wengi sababu ilikuwa asubuhi ile tuliowahi tu ndio tulishuhudia kichapo kile kwenye quality ya 4K yani kimya vinasikika vitasa tu pwaaah!

Wakikumbatia inakuwa kama mademu bana!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Eti jezi ya Simba [emoji38]

Kuna muda mwalimu alikamata washangiliaji wote wa ngumi..
Kumbe alichelewa kutoka aiseeee...tuliruka kichura siyo Cha nchi hii..halafu mwalimu Mwenyewe ni bimkubwa .

Nilirudi nyumbani Sina hali,akasema kesho urudie tena kubaki kushabikia ngumi.
 
Kama hujawahi kupigana class basi wew ukapimwe akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…