Mliowahi kupigana darasani leteni ushuhuda wenu hapa

Huu Uzi nimecheka sana ,ila hapa kwako nimecheka zaidi
 
Yaaani stories za humu[emoji23] mimi kiukweli kabisa mapambano yote ya primary sijawahi kushinda , kila pambano nilikua nadundwa sababu nilikua chembamba afu nilikua karefuu so ilikua rahisi kunikata mtama nikaanguka mzima mzima[emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaah.
 
Ilikua darasa la 4 nimehamia kwenye shule mpya baada ya miezi kadhaa kuna binti tukapishana kauli class basi akaniambia atanikomesha,nkashangaa yani huyu demu aniletee dharau mm kidume ,sasa ngoma ikawa kesho yake tumetoka nje ya shule bhana sikuamini kumbe yule demu wapo wawili ni mapacha wanafanana kila kitu aisee si wakanifata tulizichapa walinichangia kiukweli walinipiga[emoji23][emoji23]kumbe kwao wana ma bro wanawafundisha ngumi.
Heshima ikawepo mpaka tunamaliza la 7 wao ndo ma best zangu tunakaa dawati moja even mpaka leo nimemaliza chuo they are my best friends sana tunapendana
 
Unatakiwa uwachape kwa nyama
 
Nachokumbuka nilipgwa kichwa kimoja na kaka mkuu akili ilrudi nikiwa nyumbani na damu kama maji zinamwagika
Nyieee
 
Shule za kata bhana ! Sisi shuleni kwetu ugomvi ulikuwa wa kimtaa shuleni , maana mtaani kwetu tunajuana nani mbabe na viwango tunavijui,ukimwonea wa mtaa mmoja make sure siku hiyo baada ya kengele ya kurudi nyumbani unatoroka na kubadili njia.

Siku moja tulikuwa paredi ili tutawanyike tuende manyumbani,sasa kulizuka mchezo ukikaa kizembe umejisahau mtu anakuja kwa nyuma anakuvuta kaptula gafla halafu anakimbia,au umesimama umejisahau anakupiga ngwara unapiga mweleka halafu anakimbia.

Sasa jamaa akaninyemelea akanipiga ngwara nilipiga mweleka wa hatari chini ,kugeuka nyuma wote wametulia wanacheka ,nikahisi jamaa flani nikanyamaza sina ushahidi.

Mara nimejisahau tena akavuta kamptula yote ilishuka mpaka chini halafu sikuvaa hata kitu kingine kwa ndani bahati nzuri shati nililovaa lilikuwa ndefu kwahiyo hamna aliyeona mapu...mbu.


Uzuri awamu hii nilimwona jamaa mwenyewe huwa ananifanyia bullying sana. Nikaanza kupewa bichwa tuzichape ,aisee tulizichapa nilikuwa namzidi ila alikuwa anawahi upande wa mchanga anauchota kwa mguu na kunirushia machoni,nikianza kufuta macho ananiwahi ananipa ngumi mfululizo ,nikapata akili nikawa namzuia upande wa mchaga asiupate. Mwalimu alivyofika wanafunzi wakaropoka " walikuwa wanapigana ". Tulitandikwa ,tulipotawanyishwa tu tuliorganize tena kuzichapa njiani na kundi linafuata tu kuona ngumi, tukaanza tena ,jamaa alikuwa ananizidi ngumi,kuna ngumi ya sikio nilipata nikasikia tu tiiiiiiiiii na mawenge juu ,nikasema huyu jamaa simwezi nikaanza kumkimbia na kuokota mawe,akinimbiza namchega kidogo nageuka nampa namlega mawe za uso, ananikimbiza tena nasimama gafla nampa mawe ya uso, si nikampiga jiwe la jicho,akapiga kelele "naona gizaaa" nikasema hii mbinu tu anatania ,nikamwahi hapo hapo nikaanza kumpa ngumi mfululizo.

Sasa sijui nilimpiga wapi huko tumboni au kwenye mbavu ,jamaa akaanguka kama punzi inakata vile,tukamlaza vizuri na kumpepea kama lisaa moja jamaa anatetemeka balaa kuamka shida. Sasa ishu ikaja kumpepea pale apone ili taarifa zisifike nyumbani ,akazidiwa ikabidi wazazi wake waambiwe ,wakaja kumchukua na kumpeleka zahanati. Nilipofika nyumbani taarifa nayo imeshafika , nilipoingia tu mzee akafunga mlango akaikunja vizuri kamba ya ng'ombe ,alinitandika balaa.

Ile ishu ilimalizwa tu kifamilia.
 
Huyo hery Barton namfahamu anavyoonekana tuu sio bondia nzuri
 
Yaaani stories za humu[emoji23] mimi kiukweli kabisa mapambano yote ya primary sijawahi kushinda , kila pambano nilikua nadundwa sababu nilikua chembamba afu nilikua karefuu so ilikua rahisi kunikata mtama nikaanguka mzima mzima[emoji23][emoji23]
Nachukuwa nafasi hii kumtangaza Financial services ndio bondia aliyepoteza mapambano yote hakuwai kushinda pambano hata moja Hadi alipostafu
 
Nachukuwa nafasi hii kumtangaza Financial services ndio bondia aliyepoteza mapambano yote hakuwai kushinda pambano hata moja Hadi alipostafu
Mkuu 😂😂😂 waliokua wananipiga nikiwacheki sahivi ukubwani natamani turudie mapambano yote niwadunde , maana naona kabisa hawana nguvu sijui ilikuaje wakanipiga aisee😂😂
 
Huyo hery Barton namfahamu anavyoonekana tuu sio bondia nzuri
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 zile ngumi zingekuwa televised jamaa wangekula medali kabisa. Ngumi za kiwango cha lami kabisa za kisomi
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Shule ya Msingi nilimuotea Jamaa mmoja alikuwa anaitwa Zakaria.

Jamaa alikuwa anatoka kama kilomita kumi na kitu hivi kuja shule..Jamaa alikuwa mweupe kinoma mpaka tukawa tunamuita "Nyeupee".

Siku hiyo tulizenguana uwanjani wakati wa mapumziko nikamuwahi ngumi kadhaa kabla hajanirudishia Kaka Mkuu akatuwahi kutuamua.

Basi Nyeupee alipata hasira, akawa analia mishipa imemtoka na vile alivyo mweupe...kisa aliumia sana mimi kumuotea alafu yeye akazuiliwa kulipiza kisasi.

Ni kama Kaka Mkuu alikuwa upande wangu hakutaka nipigane, na alikuwa bonge la Mtu alichimba biti moja tu"nione Mtu anapigana tena"...hiyo ni mwanzo wa 1990's.

Sijui hata huyu Jamaa yuko wapi na alikuwa Mzuri sana kwa Hisabati.
 
Alikuwa anaitwa Zephania....nilikosea sio Zakaria.
 
Huenda ila mpaka ku connect dots sidhani kama ni rahisi...labda kama nikitaja na shule.
Bila ya shaka akitokea ataomba pambano lirudiwe[emoji38]
 
Kuna muda unampiga mtuu mpaka muda wa kutoka shule unapita njia usizo xijua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…