Mlipuko wa Homa ya Nguruwe (ASF), Kuna nini Wizara ya Mifugo ???

thekop

Member
Joined
Sep 11, 2024
Posts
5
Reaction score
5
Toka mwaka huu uanze kumekuwa na mlipuko mkubwa wa homa ya nguruwe (ASF) kwa mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Pwani, Tanga na sasa Arusha na Kilimanjaro ugonjwa unaendelea kushika kasi. Kwa sasa nyama ya kitimoto inayouzwa kwenye mabucha Arusha na Moshi kwa kiasi kikubwa inatokana na nguruwe walioathirika na ugonjwa huu
Cha kusikitisha Wizara ya Mifugo ipo kimya licha ya maabara kuthibitisha uwepo wa ugonjwa (ASF) huo.

Wizara ya Mifugo lini mtatoa tamko kuhusiana na ugonjwa (ASF) huu ??? Athari za ugonjwa huu kiuchumi kwa wafuga nguruwe ni kubwa sana na kukaa kwenu kimya wakati ugonjwa upo zaidi ya Mikoa mitano kwa sasa (Dar es salaam, Morogoro, Pwani, Tanga na Arusha)ni hujuma kubwa kwa wafugaji wa nguruwe nchini.

Mmekaa kimya kwa sababu wafuga nguruwe ni watu wa dini fulani tuuuu???
 
Nyama haina shida,

Quarantine zimewekwa kwenye maeneo yenye ASF ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo kwenye maeneo mengine yaliyo salama.
Screenshot_20250719-191629~2.jpg
Screenshot_20250719-191426~3.jpg
 
Jamani jamani isiwe hujuma kwa kitimoto yetu.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Toka mwaka huu uanze kumekuwa na mlipuko mkubwa wa homa ya nguruwe (ASF) kwa mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Pwani, Tanga na sasa Arusha na Kilimanjaro ugonjwa unaendelea kushika kasi. Kwa sasa nyama ya kitimoto inayouzwa kwenye mabucha Arusha na Moshi kwa kiasi kikubwa inatokana na nguruwe walioathirika na ugonjwa huu
Cha kusikitisha Wizara ya Mifugo ipo kimya licha ya maabara kuthibitisha uwepo wa ugonjwa (ASF) huo.

Wizara ya Mifugo lini mtatoa tamko kuhusiana na ugonjwa (ASF) huu ??? Athari za ugonjwa huu kiuchumi kwa wafuga nguruwe ni kubwa sana na kukaa kwenu kimya wakati ugonjwa upo zaidi ya Mikoa mitano kwa sasa (Dar es salaam, Morogoro, Pwani, Tanga na Arusha)ni hujuma kubwa kwa wafugaji wa nguruwe nchini.

Mmekaa kimya kwa sababu wafuga nguruwe ni watu wa dini fulani tuuuu???
Kwani hiyo Dini ya wafuga nguruwe wamekatazwa kufuga Mbuzi!?
Cha ajabu sijawai kusikia ugonjwa Kondoo wa Meeeh.
 
Back
Top Bottom