Mlo wa tofauti. Hii itakusaidia

Mlo wa tofauti. Hii itakusaidia

MAMESHO

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
1,432
Reaction score
1,738
Habari za leo ndugu wapendwa.

Ni kwa muda sasa nimekuwa na mazoea ya kula vyakula kama jamii yetu ilivyozoea. Asubuhi chai na maandazi, mikate au chapati, mchana ugali, jioni wali na vitu vingine.

Nimepata mtazamo tofauti ambao naona umenisaidia jana baada ya kuandaa mchanganyiko ufuatao.
Karoti 2
Tango 1
Ndizi mbivu
Tangawizi kidogo
Nyanya 1
Karanga. Nusu glass Zichemshwe.
Katakata vidogo vidogo. Tangawizi ikwaruze changanya kwenye bakuli moja. Mlo mzuri sana wa jioni. Kula kabla ya saa mbili usiku.

Nimeamka vizuri sana asubuhi bila uchovu. Nilipata usingizi mzuri sana.

Nimeshare hapa maana najua kuna watu itawasaidia kiafya lakini pia ni gharama nafuu.

Lakini pia inabebeka kwa urahisi kukuoatia lunch ya mchana ofisini.

Unaweza kuitengeneza popote hata ukiwa safarini.

Siku njema. Kaa na afya njema
 
Kwa familia ni mateso tu
Sio kweli mkuu.
Nilikwenda sokoni
Karoti 6 sh 500
Nyanya 5 sh 500
Tango 4 kubwa sh 500
Ndizi moja 150/=tsh na nyongeza juu.
Mradi tu usivinunue gengeni bei ni kubwa.
 
Kwa familia ni mateso tu
Ila ni swala la fikra zaidi. Nadhani hiyo chakula ikiongezwa zao moja la mzizi kama viazi au muhogo kwa wale wanaokula sana wataanza kuzoea. Japo hakuna kinachomfaa kila mtu. Tunatofautiana sana.
 
Zoezi linaendelea with addition ya kitunguu ocassionally kupata ladha tofauti.
IMG_20210820_155227.jpg
 
Back
Top Bottom