Mlo wa wiki (Health Diet)

Mlo wa wiki (Health Diet)

Mihogo kaondoka nayo Dokta. Hata ungeitaka ungeipatia wapi??

Mi natia timu next month.... ole wako nikukose.

Tafadhali next month isije kuwa ni baada ya uchaguzi.........njoo mapema ili tujue hii mambo........
 

Mfano mi nakaa Sitimbi, bacon napata wapi? (Itabidi niwaambie wanirostie mbuzi katoliki nusu kilo mixer mchicha) nshaharibu diet
Protein powder nanunua wapi kwa mfano???
Bajeti ya kuunga nå manati ntamudu kununua matunda kama strawbery,almond hapo bado sijaweka gharama za olive oil.

Mi naona hii ya wa kishua
 
Last edited by a moderator:
Mfano mi nakaa Sitimbi, bacon napata wapi? (Itabidi niwaambie wanirostie mbuzi katoliki nusu kilo mixer mchicha) nshaharibu diet
Protein powder nanunua wapi kwa mfano???
Bajeti ya kuunga nå manati ntamudu kununua matunda kama strawbery,almond hapo bado sijaweka gharama za olive oil.

Mi naona hii ya wa kishua

Tena bei ya almond kilo 2 unanunua Nissan March ........
 
Samahani dada Yummie.......
Bacon na almond ni nini?
Niwekee hata tupicha nivijue
 
Last edited by a moderator:
Hebu ngoja kwanza......
Hii inanihusu na mimi wa huku Yaeda au ni nyie wa mjini tu...........

Da Preta umemaliza! Kuna maeneo hakuna supermarket kununua hayo mavitu. But kwa Jf sishangai ndo maisha yalivyo.
 
Baada ya wiki utakuwa urojo kabisa. Hakuna staple food hapo. Sio balanced diet. Hauli vyakula vya kukupa energy utakuwaje fit?
 
Zaidi ni kwa wanaopunguza uzito. But you can add potatoes and rice if you just want to stay health not to loose weight

Okaaay, hapo sasa nimeelewa kumbe ni kwa vibonge wanaotafuta uportable!
 
Hebu ngoja kwanza......
Hii inanihusu na mimi wa huku Yaeda au ni nyie wa mjini tu...........
yaeda supu ulimi,kongoro supu utumbo inahusu,usisahau makanyagio ya kuku kwa lunch,sambusa za viazi kwa dinner na utumbo wa kuku.
 
Habari zenu wanaJF
Hii ni ratiba ya mlo kwa wiki nzima kwa ambao wanapenda kuwa na afya bora pamoja na kujiepusha na baadhi ya maradhi na magonjwa kwa kupitia mpangilio mzuri wa vyakula.

Jumatatu:
Asubuhi- mayai ya kukaanga pamoja na baadhi ya mbogamboga zilizopikwa kwa siagi(butter) au mafuta ya nazi.

Mchana; Changanya mtindi/strawberries au blue berries pamoja na almonds saga kwenye blender kisha kunywa (smoothie).

Usiku; Cheese burger iliwe na mbogamboga na salsa sauce.

Jumanne:
Asubuhi;bacons and eggs

Mchana;brown bread na mboga za majani.

Usiku; Samaki,butter na mbogamboga.

Jumatano:
Asubuhi; mayai ya kuchemsha na mbogamboga

Mchana;Salad ya samaki aina ya kamba waliopikwa kwa olive oil.

Usiku; kuku choma na mbogamboga

Alhamis:
Asubuhi;omelet na mbogamboga

Mchana;Chicken salad iliyoandaliwa na olive oil.

Usiku;Nyama especially steak na mbogamboga.

Ijumaa:
Asubuhi;bacons and eggs

Mchana;Smoothie(saga strawberries tui la nazi almonds na protein powder.)

Usiku;Nyama na mbogamboga

Jumamosi:
Asubuhi;omelet na mbogamboga

Mchana;smoothie

Usiku;meatballs na mbogamboga.

Jumapili:

Asubuhi; bacons and eggs

Mchana;smoothie

Usiku;Chicken wings zilizookwa na mboga za spinach.
menu ya watoto wa masaki.
mkipewa ugali na mboga uji wa chumvi si mtajiua nyie?namkumbuka baba wa taifa
 
Back
Top Bottom