Mlokole ampiga shoka mama yake, amuua

Mlokole ampiga shoka mama yake, amuua

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
attachment.php

Na Dustan Shekidele, Morogoro

KWELI kuelekea mwisho wa dunia, mengi yataonekana. Mtu unawezaje kumpiga shoka mama yako mzazi, aliyekutunza tumboni mwake kwa miezi tisa, akakunyonyesha, kukusomesha hadi kukua na kujitegemea?

attachment.php

Mwili wa marehemu Ndolukasi Lugamo ukitolewa eneo la tukio.
Frank Hillary, 27, aliyetambuliwa kuwa mlokole, amethubutu na kuweza kukatisha maisha ya mama yake, Ndolukasi Lugamo, 50, akitumia shoka kuondoa uhai wa mzazi wake.

Frank Hillary akiwa chini ya ulinzi.
Tukio zima, lilichukua nafasi Alhamisi iliyopita, Mtaa wa Malipula, Kata ya Chamwino, mkoani hapa na inadaiwa kwamba kabla ya mauaji, Hillary alimpiga vibao, mitama na mateke mama yake.

attachment.php

Muuaji Frank Hillary (27), akiwa mikononi mwa wanausalama.
HALI HALISI ILIVYOKUWA
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Pili Athuman, alidai kwamba siku ya tukio, kulitokea mabishano kati ya Hillary na mama yake.
“Yalikuwa mabishano kidogo lakini ghafla yule kijana alimvamia mama yake na kuanza kumpiga,” alisema Pili na kuongeza:
“Yule kijana ni mtoto wa pekee wa yule mama. Tunashindwa kuelewa mpaka sasa chanzo cha tukio hilo. Halafu wale watu ni walokole kabisa na siku zote walikuwa wanaishi kwa upendo.”

attachment.php

Wananchi wakiangalia shoka lililotumika kuondoa uhai wa Ndolukasi Lugamo.
Shuhuda mwingine, Julius Josephat alisema: “Mimi nashindwa kuelewa. Huyu marehemu na mwanaye walikuwa wanapendana sana, wakienda kanisani wanaongozana kama kumbikumbi.
“Kinachosikitisha zaidi ni kuwa mama yake aliumia mkono kama siku tatu kabla, akawa amefungwa plasta ngumu (POP), nahisi ndiyo maana alishindwa kujiokoa.”

Mwili wa marehemu pamoja na shoka lililotumika vikitolewa eneo la tukio kupelekwa kwenye difenda.
Naye Maria Maswika ambaye nyumba yake imepakana na ile ya mama Hillary, alieleza: “Leo (Alhamisi), saa 4 asubuhi nilimsikia huyo mama akipiga kelele za kuomba msada, huku akiingia nyumbani kwangu.
“Nilipotoka chumbani, nilishuhudia kwa macho yangu yule kijana akimpiga shoka mama yake na kumuua palepale. Sababu ya ugomvi wao siielewi. Kwanza nashangaa sana, kwani yule mama wa watu alikuwa anampenda sana mtoto wake.”

attachment.php

Muuaji Frank Hillary akipigwa pingu na wanausalama.
HILLARY AKAMATWA
Mwandishi wetu alifika eneo la tukio mapema na kushuhudia wananchi wakimkamata Hillary, kumfunga kamba kabla ya polisi nao kuwasili, kuandika maelezo na kumchukua mtuhumiwa huyo wa mauaji ya mama yake mzazi.

RPC ANASEMAJE KUHUSU SHERIA?
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, ACP Faustine Shilogile, alisema: “Uchunguzi zaidi wa tukio unaendelea na utakapokamilika, tutamfikisha mtuhumiwa mahakamani.”

attachment.php

Paka
anayetajwa kumilikiwa na marehemu akiwa pembeni ya mwili wa Ndolukasi Lugamo.
PAKA WA KUSHANGAZA
Kitu kilichowashangaza wengi eneo la tukio ni paka anayetajwa kumilikiwa na marehemu ambaye baada ya mama huyo kuuawa, yeye alikwenda kulamba damu kisha akalala kichwani kwenye mwili wa marehemu.

Mtuhumiwa Frank akipandishwa kwenye difenda.
TUTAFUATILIA
Uwazi linaendelea kufuatilia na litaweka bayana sababu hasa ya mauaji hayo na kilichompata kijana huyo mpaka akachukua uamuzi wa kumuua mama yake.

attachment.php

Safari ya kuelekea kituoni imeiva.

Attachments

• MLOKOLE 1.jpg
MLOKOLE 1.jpg
61.8 KB · Views: 588
• MLOKOLEAMPIGASHOKAMAMAYAKEAMUUA2.jpg
MLOKOLEAMPIGASHOKAMAMAYAKEAMUUA2.jpg
48.5 KB · Views: 574
• MLOKOLEAMPIGASHOKAMAMAYAKEAMUUA4.jpg
MLOKOLEAMPIGASHOKAMAMAYAKEAMUUA4.jpg
47.1 KB · Views: 558
• MLOKOLEAMPIGASHOKAMAMAYAKEAMUUA5.jpg
MLOKOLEAMPIGASHOKAMAMAYAKEAMUUA5.jpg
46.7 KB · Views: 532
• MLOKOLEAMPIGASHOKAMAMAYAKEAMUUA6.jpg
MLOKOLEAMPIGASHOKAMAMAYAKEAMUUA6.jpg
58 KB · Views: 552
• MLOKOLEAMPIGASHOKAMAMAYAKEAMUUA3.jpg
MLOKOLEAMPIGASHOKAMAMAYAKEAMUUA3.jpg
43.2 KB · Views: 565
• MLOKOLEAMPIGASHOKAMAMAYAKEAMUUA7.jpg
MLOKOLEAMPIGASHOKAMAMAYAKEAMUUA7.jpg
92.6 KB · Views: 623
Vita yetu sisi si ya damu na nyama bali ni ya kiroho! R.I.P Mother!

viashiria vya udini nchini ni vichwa vya habri kama hiki
Mlokole ampiga shoka mama yake na kumuua
Mwislamu ambaka dada mchana kweupe
Mkristo akamatwa kwa tuhuma za ujambazi

Zamani vichwa vya habari vilikuwa hivi
Kijana akamatwa kwa tuhuma za ujambazi
Mkazi wa Geita amnyonga mpenzi wake

Back to topic...
RIP marehemu

swala ni mauaji na si kuweka neno mlokole kwani mlokole akiua ndio kosa wengine sawa tuache utoaji mbaya wa taarifa huku ni uchafuzi wa imani ya ukristo .

Huyu mtuhumiwa inaonekana akutolewa mapepo vizuri na mchungaj wake..
R.I.P Mama

viashiria vya udini nchini ni vichwa vya habri kama hiki

Mlokole ampiga shoka mama yake na kumuua

Mwislamu ambaka dada mchana kweupe

Mkristo akamatwa kwa tuhuma za ujambazi

Zamani vichwa vya habari vilikuwa hivi

Kijana akamatwa kwa tuhuma za ujambazi

Mkazi wa Geita amnyonga mpenzi wake

Back to topic...

RIP marehemu
Mkuu ulichosema ni kweli kabisa. Waandishi inabidi wajipange upya kwa namna moja au nyingine wanachangia sana mambo ya uchochezi wa kidini.
Mungu amweke marehemu pema peponi

Nyie UWAZI acheni kutoa habari nusu nusu ili muuze gazeti. Habari hizo tumezisikia kwenye vyombo vingine vya habari wakisema kuwa inasemekana huyo kijana ana matatizo ya akili (mgonjwa wa akili) lakini nyie hata hamjagusia hilo zaidi ya kushupalia neno "mlokole" ili muuze gazeti. Kama mlisikia kuwa huyo ni mlokole na mkaandika, natumai pia mlisikia kuwa ni mgonjwa wa akili, mbona hilo hamjaandika? Jifunzeni kufuata maadili ya uandishi.
R.I.P Mama

viashiria vya udini nchini ni vichwa vya habri kama hiki
Mlokole ampiga shoka mama yake na kumuua
Mwislamu ambaka dada mchana kweupe
Mkristo akamatwa kwa tuhuma za ujambazi

Zamani vichwa vya habari vilikuwa hivi
Kijana akamatwa kwa tuhuma za ujambazi
Mkazi wa Geita amnyonga mpenzi wake

Back to topic...
RIP marehemu
hiii ni kweli kabisa ,na mzizi mkavu anapenda sana kuleta mada hizi''mchungaji ambaka mtoto wa miaka .....'' ndio mambo yake udini tutututu
ingesomeka hivi ''kijana morogoro amwuua mama yake kwakumkata na shoka''nafikiri its enough kabisa ULOKOLE HAS NOTHING TO DO WITH THEIR PERSONALITY

Hata mimi, mtu akiniletea ujinga namuua tu. Kwanini nini bana!

Back
Top Bottom