Mmasai nchini Kenya aacha watu midomo wazi kwa akili kubwa aliyotumia kuegesha gari lake

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2021
Posts
630
Reaction score
1,262
Mwanamume wa kimasai aliingia katika benki moja huko Nairobi Kenya kwa lengo la kuomba mkopo.

Alimwambia afisa wa mikopo kuwa anaenda Dubai kikazi kwa wiki nne na anahitaji kukopa 5,000 Ksh.

Afisa wa benki hiyo akamwambia kwamba benki itahitaji dhamana ya usalama wa mkopo huo.
Mmasai akadai anamiliki gari jipya hivyo ataweza kuweka dhamana, basi taasisi ya mkopo ikamtaka kukabidhi funguo za gari jipya kabisa la Mercedes Benz S class 500 lililoegeshwa barabarani mbele ya benki hiyo.

Benk ikaandikisha kilakichomo ndani ya gari katika daftari la kumbukumbu.

Afisa wa mkopo akakubali gari kama dhamana ya mkopo.

Rais wa benki hiyo na maafisa wake wote wakafurahia na kumcheka mmasai kwa kutumia Mercedes Benz ya KSH 15Milioni kama dhamana dhidi ya mkopo wa 5,000 Ksh.

Mfanyakazi wa benki hiyo akaiingiza Mercedes Benz kwenye karakana iliyopo chini ya ardhi ya benki hiyo na kuiegesha hapo.

Wiki nne baadaye, mmasai akarudi na kurejesha 5,000 Ksh alizokopa pamoja na riba ambayo inakadiriwa kufikia 150.41.

Afisa wa mkopo akasema 'Bwana, tuna furaha sana kufanya biashara na wewe na shughuli hii imefanyika vizuri sana lakini tumeshangazwa kidogo.

Ulipokuwa mbali, tulikuchunguza na tukagundua kuwa wewe ni bilionea.

Unajua kinachotutatanisha ni nini? kwa nini ujisumbue kukopa hela ndogo kiasi cha 5,000 Ksh?

Mwanaume wa Kimasai akajibu: 'Ni wapi tena Nairobi ninapoweza kuegesha gari langu kwa muda wa wiki nne kwa 150.41 pekee na kutarajia kulikuta salama nitakaporudi?

images (7).jpeg
 
Hii story nili isikiaga kama miaka mitano hivi nyuma, ahsante kwa kunikumbusha
 
Mtoa mada jiheshimu, aliyekwambia benki ukichukua mkopo dhamana unaiacha hapohapo bank ni nani?
 
Mwanamume wa kimasai aliingia katika benki moja huko Nairobi Kenya kwa lengo la kuomba mkopo.

Alimwambia afisa wa mikopo kuwa anaenda Dubai kikazi kwa wiki nne na anahitaji kukopa 5,000 Ksh.

Afisa wa benki hiyo akamwambia kwamba benki itahitaji dhamana ya usalama wa mkopo huo.
Mmasai akadai anamiliki gari jipya hivyo ataweza kuweka dhamana, basi taasisi ya mkopo ikamtaka kukabidhi funguo za gari jipya kabisa la Mercedes Benz S class 500 lililoegeshwa barabarani mbele ya benki hiyo.

Benk ikaandikisha kilakichomo ndani ya gari katika daftari la kumbukumbu.

Afisa wa mkopo akakubali gari kama dhamana ya mkopo.

Rais wa benki hiyo na maafisa wake wote wakafurahia na kumcheka mmasai kwa kutumia Mercedes Benz ya KSH 15Milioni kama dhamana dhidi ya mkopo wa 5,000 Ksh.

Mfanyakazi wa benki hiyo akaiingiza Mercedes Benz kwenye karakana iliyopo chini ya ardhi ya benki hiyo na kuiegesha hapo.

Wiki nne baadaye, mmasai akarudi na kurejesha 5,000 Ksh alizokopa pamoja na riba ambayo inakadiriwa kufikia 150.41.

Afisa wa mkopo akasema 'Bwana, tuna furaha sana kufanya biashara na wewe na shughuli hii imefanyika vizuri sana lakini tumeshangazwa kidogo.

Ulipokuwa mbali, tulikuchunguza na tukagundua kuwa wewe ni bilionea.

Unajua kinachotutatanisha ni nini? kwa nini ujisumbue kukopa hela ndogo kiasi cha 5,000 Ksh?

Mwanaume wa Kimasai akajibu: 'Ni wapi tena Nairobi ninapoweza kuegesha gari langu kwa muda wa wiki nne kwa 150.41 pekee na kutarajia kulikuta salama nitakaporudi?

Mmasai akili mingi
 
Back
Top Bottom