Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Watu wengi hufikiri uchungu wa bia unatokana na pombe. Uchungu wa bia hutokana na mmea unaoitwa hop. Watengenezaji wa pombe hutumia mimea mbalimbali kuzipa pombe ladha mbalimbali. Mmoja wa mmea huo ni hop ambao huzipa bia uchungu. Mmea huu upo jamii moja na mmea wa bangi lakini hauna kemikali kama za bangi.