ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 937
Ukijaribu kuwauliza baadhi ya wale wa "enzi za mwalimu" watakuambia siku zile akina mama zenu wengi hawakuwa na kazi na hata kama aliandika mfanyakazi wa ndani yeye alilijitahidi kila kitu kinachomhusu "baba/mumewe" kufanya mwenyewe ikiwemo kumpikia chakula.
Enzi zile akina mama wengi walijua kanuni na kuzizingatia. Ikiwa mume utachelewa kwenye mihangaiko yako, ni lazima atakusubiri ili ahakikishe kuwa umeingia ndani, umeoga na umekuandalia chakula na umekula kabla ya kualala. Ikiwa utajifanya hupendi kula chakula alichopika, hicho chakula hakitatupwa, kitahifadhiwa na siku ya siku wataitwa wazee washuhudie jinsi unavyomfanyia mwenzio. Kwa mila zile, wazee watakulazlimsha tu kula mpaka kikatike chote labda kama mkeo atakuombe msamaha.
Ikiwa mke pia ni mama wa nyumbani, atahakikisha nguo za mumewe za kuvaa kazini kesho zinaandaliwa mapema ili asubuhi asitoke akiwa hovyo hovyo..(ilikuwa ni aibu kwa mke ikiwa mume anaonekana ofisini akiwa hovyo).
Wale wa "enzi za Mwalimu" ndio wanaolaumu hiki kizazi cha sasa cha dotcom cha "copy & paste". Sasa eti hata mke kama hana kazi (mama wa nyumbabi) atataka kuandika/kuajiri binti wa kazi (ainaitwa dada). Huyo ndio anakuwa kama Waziri Mkuu wa familia. Kila kitu atafanya huyo kuanzia kuangalia watoto na hata baadhi ya "welfares" za baba.
Potelea mbali hata kama kipato chenu ni duni, mama hawezi hata kwenda sokoni, hawezi kuthubutu hata kuingia jikoni kuweka chai wa watoto (wengi hawana kabisa hata huo muda wa kujua hata kama vyombo wala jiko liko safi).
Wapo wengine kama hana kazi au ana kazi yeye akiwa nyumbani atashindwa runingani muda wote akiangalia akina "MASANJA, JOTI, FUTUI, KINGWENDU, BAMBO nk kama si kupitia video basi "LIVE"
Wanasema, baba kama hujui kuingia jikoni umeliwa!!! ukirejea umechoka usipokuta kitu ukauliza mama nini kinaendelea jikoni nae anaita kwa sauti kutokea sebuleni, ..." ...we dada umefikia wapi chakula..unapika mawe???"
Pengine chakula kikipikwa hovyo hovyo unajaribu kuonyesha kutofurahishwa, hasira za mama zitahamishiwa kwa "dada" atasimama kumfuata "dada" akimkalipia kwa nini kwa nini kapika chakula kibovu kwa makusudi..., (wengine wanaweza kumtandika hata makofi kudhihirisha mbele yako kuwa si yeye aliyeandaa kile chakula ).
Ukimwambia mama amekosea, anakujia juu kuwa usimwingilie kwa kuwa yeye ndie aliyemtafuta huyo binti wa ndani...pengine ukizidisha utazuliwa kisa na anaweza kumfungashia vilago muda huo huo (hata kama ni usiku) na siku inayofuata utasikia amekuja "dada mwingine"...anadaiwa mshahara wa xTshs.
Hali hii ya maisha ya kutegemea wasichana wa kazi imekuwa ni kama homa ya kuambukiza kwa familia nyingi...Imekuwa ni kama kina mama wamebinafsisha mno majukumu yaokwa wasichana wa kazi na wao kukosa kabisa uthibiti..