Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 652
- 1,058
Hata kama inafikiriwa ni watu wachache tu wanafikia hatua ya kuchukizwa na baadhi ya vitendo vya Rais na kuwa haiwezi kuathiri yeye kukosa Urais kwenye uchaguzi ujao bado kuna madhara makubwa sana yanayotokana na kuchukizwa huko na kumwathiri yeye katika maisha ya Urais na hata ya kutokuwa Rais. Ikumbukwe kuwa vizazi huendelea tena na tena - labda kwa wale ambao huwa hawabahatiki kuzaa watoto wakaendeleza koo zao. Hivyo kuna umuhimu pia wa kuwa rational katika uongozi na hasa katika kutoa fair comments ili huko baadaye sio wewe tu hata jamaa zake waje waishi vizuri tu wakipewa haki ya staha.
Kwa muda mrefu nimekuwa nikishuhudia Rais akiwa anahutubia au anafanya maamuzi baadhi baadhi huambatana na maneno ambayo pengine hakupaswa kuwa anayatamka. Tunajua kwa mfano Mkapa alikuwa mkali sana lkn bado alikuwa na staha katika maneno aliyayatoa au kwa wananchi au yaliyohusu viongozi wenzake. Kwa mfano Mkapa alikuwa akifanya mabadiliko ya uongozi sio lazima aelezee sana na kuponda utendaji wa huyo Waziri anayemwondoa. Kikwete hata naye hakuwa hivyo na badala yake aliwasilisha tu hoja zake vema huku akilinda utu wa wenzake na hata wananchi. Sasa kwa Rais wa sasa naona wasaidizi na washauri wake wamekuwa wakishindwa kumwambia kuwa anapaswa pia kulinda hadhi na utu wa wananchi na hata viongozi wake.
Mfano kuna clip inaonesha anamsema Mwananzila hata Ukatibu Tarafa hafai. Nafikiri haikuwa sahihi kusema hivyo kwa wazi namna ile na hasa ukizingatia tu uamuzi wa Mwananzila kugombea ubunge - haki yake - inaonesha kwa tafsri yake Rais ana uchu wa madaraka. Magufuli alipaswa akumbushwe tu na wasaidizi wake kuwa mbona yeye mwenyewe alianzia ualimu kabadili kazi hadi kufikia kuwa Rais - so ina maana na yeye alikuwa na tamaa ya madaraka? Nina amini maneno hayo yamemkaa Mwananzila hata na ukoo wake na watoto wake na wajukuu pia.
Kuna mifano mingi tu - anapoamua kubadili uongozi anatoa hadi maongezi mengine ambayo pengine yalipaswa kuwa siri. Wakati wa JK Magufuli alibadilishwa badilishwa pia katika nafasi ya uwaziri na hakuwahi kusemwa kuwa may be hapa kaharibu hiki au vile. Lkn yeye sasa washauri wake wamekuwa wakimsikia akitamka wazi Mfano "fulani kanipigia simu usiku" "huyu nimeongea naye usiku wa manane", "hiyo ni too academic" n.k. Kuna DED aliitwa mpumbavu kwenye mkutano wa hadhara. Kuna wananchi waliopondwa walipolalamikia njaa. Kuna jamaa wa Igunga aliongea kuhusu ukata wa fedha akajibiwa hafanyi kazi kwa kupondwa sana. Yaani Rais hata km ni mkali alipaswa atumie ukali wa aina ya Mkapa sio wa kugombeza wananchi na viongozi wake hadharani. Kuna mwanamke mwingine aliambiwa "hata mume wake huwa anamlilia sana". Mara "huwa sijaribiwi". Kuna mengi kwa kweli na washauri wake hawaoni.
Najiuliza hivi Rais huwa haruhusu kabisa kushauriwa hata kdg tu kuwa awe mkali lkn achague sana maneno ya kuongea na asioneshe kushambulia watu kwa majina au kwa vidole na badala yake aongee kwa ujumla mpaka itokee kesi ambayo ni so specific. Kwa mfano Kikwete siku anamtimua Balali alionesha ukali lakini hakuvunja utu wa Balali. Kikwete siku anamponda Mgaya - alikuwa kakasirika sana lkn akachombeza tu "akili za kuambiwa ......". Mkapa yeye aliwahi kukiri mbele ya Mwandishi wa habari kuwa alikuwa kakasirika lkn hakuwa anaongea kwa sentensi karaha zenye kujenga chuki ya muda mrefu kwa vizazi hadi vizazi.
Wasaidizi wa Rais, tafadhalini jaribuni kuvaa ujasiri Rais ashauriwe aendelee kuwa mkali lkn asiwe anaongea katika namna ya kushambulia direct. Tunaelekea uchaguzi apunguze au kuacha kabisa maneno ya kushambulia kwa sababu wapiga kura hubadilika siku moja tu - tena dakika tu. Nakumbka siku JK alivyotoa speech ya kuachana na Katiba Pendekezwa Jamii ya Kitanzania ilivyokea hilo. Nina uhakika ingekuwa uchaguzi ni mwezi huo JK asingepita kwa sababu naamini hata akina Warioba wangemsema vinginevyo. Ninavyoona kwa sasa anachofanya JPM cha kutotamka kabisa kuhusu Tundu Lisu kinasaidia sana kiasi kwamba Tundu Lisu anavyomtamka yeye inaonekana Tundu Lisu ndiye mwenye matatizo.