Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Kiranga me najuaga hii id ni ya she ila kwa hii mistari uliyoshusha mamaa unanifanya nisome kama na flow na beat cuz am a big funny of hip -hop,u gt talent and skills mamaa,big up!!
Kiranga wa mistari, mkali rijali
Mwite she, shari, umenunua zali
Hafuati mila , ndoa bila mahari
Nguvu kaa uvutano kati ya jua na sayari
Galagaza chini chali, hii kubwa gari
Kukurudisha shule ka mtoto na daftari
Mistari mali, yavuma kila pahali
Kaa kidari, cha ndalilo ndali
Toka kuu bahari Bali mpaka jangwa Kalahari
Tenzi tamu asali, tungo urari halali
Wachimba chumvi wasali, toba, kimbunga, hatari
Utalinganisha vipi mwanga wa jua na kibatari?
Napinga mpaka jalali, si dalali wa uBalali
Wenye njaa ya mawazo nashibisha kama wali
Toka vidume mpaka hata wanawali
Mabishoo hata Rastafari wa Sanawari
Mpaka washashi watahayari kwa hiyari
Kiranga kiranja kipanga wa anga toka Upanga via Mkuranga
Hiyo tayari
Kaanga ka karanga, charanga Ananga Ranga,
Hiyo habari