clouds fm inamilikiwa na kina kusaga,marehemu alex kusaga(babaake joseph kusaga) ndie aliyetoa pesa na ofisi za pale kitega uchumi katika kuianzisha,hivyo mpaka anakufa alikuwa ndie mwenyekiti mtendaji wa hii radio,kuna mtu ana hisa pale lakini hisa nyingi zinamilikiwa na kina kusaga(joseph na ndg zake)
ruge ana hisa clouds?
joseph kusaga na ruge ni marafiki wa siku nyingi sana,wakati jose anapiga disco ruge alikuwa anamtumia sana nyimbo,kipindi hiko ruge anasoma marekani.wakati clouds inataka kuanzishwa joseph akamwambia mshikaji wake(ruge) na ruge akatakiwa atoe dola 20,000 ili awe na hisa,ruge akamwambia mzee wake na mzee wake akamkatalia na kumwambia ruge atafute chuo akasome masters(ndg zetu wahaya na kusoma) hivyo ruge akashindwa na hilo sharti hivyo akawa pembeni kati ya wanahisa wa clouds..
radio ilipoanzishwa,joseph akampa mshikaji wake(ruge) umeneja,hivyo ruge ameajiriwa tu pale clouds,lkn baada ya miaka kwenda nae akaamua kutoka na kitu chake cha pembeni ambacho akakiita tanzania house of talents(THT)
Hivyo ruge ni mwajiriwa tu pale clouds ila ni mmiliki wa THT