Mmiliki halali wa Jerusalem

Mmiliki halali wa Jerusalem

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
Hakuna mji wowote duniani ambao umekuwa ni mji wenye umuhimu sana kwa watu wengi kama ulivyo mji wa Jerusalem. Mji wa Jerusalem ni mji ambao una umuhimu kwa Wayahudi, Wakristo na Waislamu. Mji wa Jerusalem unajulikana kama mji wa amani lakini Jerusalem ya leo n ahata kihistoria haujawahi kuwa mji wa amani bali migogoro.

Umewahi kuharibiwa X2, na kugombewa X16, kuzingirwa na majeshi X23, matukio ya kushambuliwa X52 na kuthibitiwa na tawala mbalimbali mara kadhaa. Jerusalem imewatenganisha wat una pia kuwaunganisha kutokana na kuwa na Imani mmoja kuwa ni mji wao mtakatifu.

Ni jambo gani linaoufanya mji wa Jerusalem kuwa Maalum lakini wenye vimbwanga?

Hebu turudi mamia ya miaka nyuma.

Mji wa Jerusalem ni mji wa kale sana ukiwa na umri wa miaka 4440 au Zaidi. Kwa Zaidi ya karne 3 ya uwepo wa mji huu, madhehebu matatu yamepigana sana ili kuudhibiti; Wayahudi, Wakristo na Waislamu. Haya madhehebu matatu yote yanachimbuko kutoka kwa Nabii Abraham/Ibrahim kwakuwa haya madhehebu yote matatu yanamchukulia Abraham kama baba wao wa Imani. Vitabu vyote vya madhehebu haya yani, Tora, Biblia na Quran, vinamtaja Abraham.

Wayahudi na Wakristo wao wanadai chimbuko lao ni mtoto wa pili wa Abraham, Isack. Waislamu wanadai chimbuko lao linatoka kwa mtoto wa kwanza wa Abraham, Ishmael. Hii imani ya chimbuko imechangia sana katika kuleta utengano baina yao, japo Jerusalem umekuwa ni mji ambao wote wanauamini kama mji mtakatifu.

Katika lugha ya Kibrania, Jerusalem unajulikana kama Yerushalayim, mji mtakatifu wa Wayahudi. Sinagogi la kwenye mlima wa Jerusalem ni eneo ambalo nyumba mbili za ibada zilizotumiwa na Wayahudi zilikuwepo kwa maelfu ya miaka.

Kwenye ukuta wa Magharibi wa sinagogi na mlima inasemekana ndilo eneo lenye mabaki ya mwisho ya nyumba hizo za ibada. Leo hii eneo hili linachukuliwa kuwa ndilo eneo takatifu Zaidi katika imani ya Kiyahudi.

Wayahudi wanaposali huelekea kwenye ukuta wa Magharibi wa Jerusalem kama ambavyo Waislamu huelekea Kaaba, Makka.

Jerusalem pia ni eneo takatifu kwa Waislamu ambapo kwa lugha ya Kiarabu inajulikana kama Al-Quds, ikiwa na maana ya eneo takatifu. Hili ndio eneo ulipo msikiti wa Al-Aqsa ambapo ni eneo la tatu takatifu katika Uislamu baada ya Makka na Medina.

Juu ya Sinagogi la mlimani kuna Kuba ya mwamba (Dome of the Rock). Hili ndilo eneo ambapo Waislamu wanaamini kuwa Mtume Mohammed S.W alipaa kwenda mbinguni.

Kwa Wakristo, Jerusalem ilitajwa kama Salem kwenye Biblia. Hili ni jina la kale la Kiebrania ambalo limehifadhiwa kwenye jina la sasa, Jeru-Salem. Mji huu ndipo lilipo kanisa la Kaburi Takatifu (Holy Sepulchre) ambapo yesu ndipo alisulubishwa, akazikwa na kufufuka.

Hivyo utaona kwamba Jerusalem ni sehemu muhimu katika imani ya madhehebu haya matatu.

Lakini ni nani mmiliki halali wa eneo hili?

Ni vigumu kupata jibu la moja kwa moja kwa swali hili.

Ila, Jerusalem ni mji wa wote na hakuna mwenye hati miliki yam ji huu. Kila dhehebu limeudhibiti mji huu, na karibia kila dola iliyowahi kuwa na ngumu imewahi kuishikilia na kuithibiti Jerusalem.

Lakini kwa Kauli maarufu kutoka kwa Winston Churchill aliwahi kusema, “Inabidi Wayahudi waachiwe Mji wa Jerusalem; wao ndio walioufanya ukawa maarufu.” – You ought to let the Jews have Jerusalem; it is they who made it famous.

Ni kwa namna gani Wayahudi waliifanya Jerusalem ikawa mashuhuri?

Hebu turudi nyuma tena katika historia.

Mwaka 135 CE ambapo Warumi waliwaondoa Wayahudi katika mji wa Jerusalem na kubadili jina kutoka Yudea (Judea) kuwa Palaestina. Hili ni jina la Kigiriki lililolenga kuondoa muungano wowote walionao Wayahdi kwenye eneo hilo. Wayahudi wote walipigwa marufuku kukanyaga Jerusalem.

Baada ya kuondolewa Yudea, Wayahudi walisambaa katika maeneo mbalimbali yaliyokuwa chini ya utawala wa Kirumi, Ulaya ya leo. Lakini walishambuliwa kila sehemu walipoenda.

Katika karne ya 11, Wayahudi waliuawa na wapigania Kristo (Crusaders) kwa kigezo kwamba wao ndio walimuua Yesu. Kwenye karne ya 14, Wayahudi waliuawa kwa madai kwamba wao ndio chanzo cha vifo vinavyojulikana kama black death. Walituhumiwa kwa kubadili mahubiri ya Yesu na kushambilia majeshi ya Warumi.

Wayahudi waliendelea kushambuliwa mpaka karne ya 19 ambapo baadhi ya Wahudi waliunganisha nguvu ili kulinda chimbuko lao. Walianzisha kitu kinachojulikana kama Zionism. Hii ilikuwa itikadi ya kisiasa, na kidini ambayo ililenga mambo mawili.

  • Ililenga kuzuia Wayahudi kushambuliwa
  • Ililenga kuwarudisha Wayahudi Jerusalem
Wazionist waliamini kwamba Uyahudi sio tu kwamba ni dhehebu, bali ni utaifa. Walidai kwamba Wayahudi hawanabudi kuwa na taifa kama ilivyo kwa Wafaransa walivyo na taifa la Ufaransa. Harakati hizi ndizo ziliwarudisha Israel. Leo hii itikadi ya Zionism ni itikadi ya taifa la Israel.

Kufikia mwisho wa karne ya 19, harakati hizi zilisababisha Wayahudi wengi kwa makundi kuhamia Palestina. Kufikia mwaka 1903, kiasi cha Wayahudi 30,000 walikuwa tayari wameweka makazi yao Palestina. Kufikia mwaka 1914, kulikuwa kuna ongezeko la Wayahudi wengine 40,000.

Hapa sasa ndipo Vita ya kwanza ya dunia ikaanza. Dola ya Ottoman ikaanguka, huku Waingereza na Wafaransa wakiyatawala makoloni ya Asia. Palestina ikawa chini ya Waingereza.

Mwanzoni, Waingereza waliruhusu Wayahudi kuendelea kuhamia Palestina. Lakini, kadri Wayahudi walivyoongezeka mvutano baina ya Waarabu na Wayahudi nao ukaongezeka. Pande zote zilishambuliana huku kila upande ukidai unaonewa. Hivyo, kufikia mwaka 1930, Waingereza walianza kudhibiti Wayahudi kuhamia Palestina.

Kuibuka kwa Nazi – Ujerumani

Mambo yalibadilika tena baada ya kuibuka kwa itikadi ya Nazi. Inakadiliwa kwamba Wayahudi milioni 6 waliuawa. Waliosalia walikimbilia Marekani na Palestina kwa idadi kubwa. Kufikia mwaka 1944, idadi ya Wayahudi wanaoishi Palestina ilifika 33% ya wakazi wote. Hii ilisababisha nchi za magharibi kuanza kuunga mkono kuundwa kwa taifa la Wayahudi. Lakini nchi nyingi za Kiarabu hazikutaka jambo hili litokee.

Mwaka 1947, uadui baina ya Wayahudi na Waarabu uliongezeka. Umoja wa Mataifa ulipitisha mpango wa kuigawa Palestina katika nchi mbili. Moja iwe ya Wayahdi na iitwe Israel na nyingine ibaki kwa ajili ya Waarabu, Palestina. Ambapo Israel iwe na ukubwa wa 56.5% la eneo lote huku Palestina ikibaki na 43.5% ya eneo.

Katiak azimio hilo, mji wa Jerusalem ulipaswa kubaki kuwa eneo la kimataifa kwa kuwa madhehebu yote yanalichukulia kama eneo takatifu. Mpango huu ulishindwa kabisa kufanikiwa.

Waingereza walishindwa kuzuia machafuko, hivyo kujiondoa kabisa na kuwaachia wahusika wadundane wenyewe. Wao waliondoka wakiacha machafuko nyuma. Wayahudi wao walikubaliana na mpango wa Umoja wa Mataifa.

Tarehe 14 Mei, 1948 Wayahudi walidai uhuru wa taifa lao na kuunda taifa lao la Israel. Wapalestina waliona jamb hili ni wizi, na Wayahudi wamewaibia eneo lao. Basi kilichofuata ni migogoro na uadui baina ya Wayahudi na waarabu.

Kwa Zaidi ya miaka 70, wamepigana zidi ya vita 8 zilizo rasmi huku mashambulizi madogo madogo ambayo hayana idadi.

Katika vita hizi na migogoro hizi, Israel aliendelea kujinyakulia maeneo ya Palestina.

Hii ni ramani ya Israel na Palestina mwaka 1947.

before.JPG

Hii ni ramani ya Israel na Palestina mwaka 1948, baada ya vita ya Israel dhidi ya Waarabu

baada 2.JPG
 
Asante sana kwa historia nzuri. Wakafute tu kaeneo kalikobakia,wakachukue kote. Waarabu wote wahamie kwenye hilo eneo kubwa juu
 
Aisee haya mambo yameanza kitambo, vizazi vingi vimekufa kupigania haki za koo zao wakiamini wao ndio watu halali kutawala eneo fulani.
Mungu ameshayaondoa haya Afrika, tukiacha mipaka iliyowekwa na mataifa ya Ulaya miaka ya 1884-5 kuigawa Afrika mpaka sasa waafrika tunaishi kwakuyaheshimu maamuzi yaliyopitishwa kipindi hiko amani ikiwa imetawala pasipo kuwa na territorial expansion.
Hakika waafrika ni werevu...
 
Israel ilipoteza ardhi yake mara mbili pale walipopelekwa uhamishoni na ndipo wahamiaji kama wapalestina walipochukua mwanya huo kukalia hilo eneo.

Hiyo ni kwa mujibu wa maandiko ambayo yanatuambia hiyo ardhi walipewa na Mungu na ndio maana hata mababu zao walizikwa hapo.

Wakati waisraeli wakiishi hapo kabla ya kupelekwa uhamishoni Babeli hao wapalestina walikuwa wapi?
 
Kwani wakati Waisrael wanapewa amri kuua wanyeji wa nchi ile unafikiri walikuwa ni watu gani?
 
Inawezekana kuutatua ama kuujadiri huo mgogoro bila kuhusisha dini na jamii za kale za eneo hilo.

Kama inawezekana basi kati ya hao wahuni wa kipalestina na waisrael feki, kat yao hakuna atakate stahil ilo eneo, maana kihistoria na shahidi za kisayansi hakuna ushahid wa uwepo wa hao wakina ibrahim na yakob, zaid izo stori za wahusika wa kutungwa utazipata ktk vitabu vya hizi dini3.

Historia ya kwel inaprove mtu aliyestahil kuishi eneo ilo n mtu mweus ambaye nae alihama eneo hilo na baadae kuja kukaliwa na mwarabu.

Hata hivyo ilo eneo ni kufuru kulifananisha na ile israel ya vitabu vya dini, maana ile ilikuwa taifa kubwa kieneo, taifa lenye resources nyingi kuanzia madini, mimea mpaka wanyama na udongo mzuri kwa kilimo, leo hii uje useme ilo eneo lenye jangwa na udongo wenye mchanga usiosupport mazao mpka kubust kwa mambolea ndio taifa lile la wale wana wa Mungu?

Nonsense kabisa, mtu mweusi kushabikia huo ugomv bila ya kutumia akili, utapoteza muda wako bure na kuonekana mpumbav na mvivu wa kufikiri, enyi wajinga someni vizuri muache kuwa bendera fuata upepo.

Hakuna umiliki halali wa hiyo ardhi kwa mtu mweupe yeyote yule, maana urithi wa kwel ulikuwa chini ya mababu wa watu weusi kabla ya ujio wa hawa wahuni na wazushi
img_1_1619305297198.jpg
 
Hope sehemu ya pili inakuja maana naona km sijafika mwisho wa tahariri ya mhariri.
 
Nikukosoe
1. Wakristo wanaamini Isaack ni mtoto wa kwanza wa Ibrahim .
2. Waislam wanaamini Ismael ni mtoto wa kwanza wa Ibrahim
 
Hakuna mji wowote duniani ambao umekuwa ni mji wenye umuhimu sana kwa watu wengi kama ulivyo mji wa Jerusalem. Mji wa Jerusalem ni mji ambao una umuhimu kwa Wayahudi, Wakristo na Waislamu. Mji wa Jerusalem unajulikana kama mji wa amani lakini Jerusalem ya leo n ahata kihistoria haujawahi kuwa mji wa amani bali migogoro.

Umewahi kuharibiwa X2, na kugombewa X16, kuzingirwa na majeshi X23, matukio ya kushambuliwa X52 na kuthibitiwa na tawala mbalimbali mara kadhaa. Jerusalem imewatenganisha wat una pia kuwaunganisha kutokana na kuwa na Imani mmoja kuwa ni mji wao mtakatifu.

Ni jambo gani linaoufanya mji wa Jerusalem kuwa Maalum lakini wenye vimbwanga?

Hebu turudi mamia ya miaka nyuma.

Mji wa Jerusalem ni mji wa kale sana ukiwa na umri wa miaka 4440 au Zaidi. Kwa Zaidi ya karne 3 ya uwepo wa mji huu, madhehebu matatu yamepigana sana ili kuudhibiti; Wayahudi, Wakristo na Waislamu. Haya madhehebu matatu yote yanachimbuko kutoka kwa Nabii Abraham/Ibrahim kwakuwa haya madhehebu yote matatu yanamchukulia Abraham kama baba wao wa Imani. Vitabu vyote vya madhehebu haya yani, Tora, Biblia na Quran, vinamtaja Abraham.

Wayahudi na Wakristo wao wanadai chimbuko lao ni mtoto wa pili wa Abraham, Isack. Waislamu wanadai chimbuko lao linatoka kwa mtoto wa kwanza wa Abraham, Ishmael. Hii imani ya chimbuko imechangia sana katika kuleta utengano baina yao, japo Jerusalem umekuwa ni mji ambao wote wanauamini kama mji mtakatifu.

Katika lugha ya Kibrania, Jerusalem unajulikana kama Yerushalayim, mji mtakatifu wa Wayahudi. Sinagogi la kwenye mlima wa Jerusalem ni eneo ambalo nyumba mbili za ibada zilizotumiwa na Wayahudi zilikuwepo kwa maelfu ya miaka.

Kwenye ukuta wa Magharibi wa sinagogi na mlima inasemekana ndilo eneo lenye mabaki ya mwisho ya nyumba hizo za ibada. Leo hii eneo hili linachukuliwa kuwa ndilo eneo takatifu Zaidi katika imani ya Kiyahudi.

Wayahudi wanaposali huelekea kwenye ukuta wa Magharibi wa Jerusalem kama ambavyo Waislamu huelekea Kaaba, Makka.

Jerusalem pia ni eneo takatifu kwa Waislamu ambapo kwa lugha ya Kiarabu inajulikana kama Al-Quds, ikiwa na maana ya eneo takatifu. Hili ndio eneo ulipo msikiti wa Al-Aqsa ambapo ni eneo la tatu takatifu katika Uislamu baada ya Makka na Medina.

Juu ya Sinagogi la mlimani kuna Kuba ya mwamba (Dome of the Rock). Hili ndilo eneo ambapo Waislamu wanaamini kuwa Mtume Mohammed S.W alipaa kwenda mbinguni.

Kwa Wakristo, Jerusalem ilitajwa kama Salem kwenye Biblia. Hili ni jina la kale la Kiebrania ambalo limehifadhiwa kwenye jina la sasa, Jeru-Salem. Mji huu ndipo lilipo kanisa la Kaburi Takatifu (Holy Sepulchre) ambapo yesu ndipo alisulubishwa, akazikwa na kufufuka.

Hivyo utaona kwamba Jerusalem ni sehemu muhimu katika imani ya madhehebu haya matatu.

Lakini ni nani mmiliki halali wa eneo hili?

Ni vigumu kupata jibu la moja kwa moja kwa swali hili.

Ila, Jerusalem ni mji wa wote na hakuna mwenye hati miliki yam ji huu. Kila dhehebu limeudhibiti mji huu, na karibia kila dola iliyowahi kuwa na ngumu imewahi kuishikilia na kuithibiti Jerusalem.

Lakini kwa Kauli maarufu kutoka kwa Winston Churchill aliwahi kusema, “Inabidi Wayahudi waachiwe Mji wa Jerusalem; wao ndio walioufanya ukawa maarufu.” – You ought to let the Jews have Jerusalem; it is they who made it famous.

Ni kwa namna gani Wayahudi waliifanya Jerusalem ikawa mashuhuri?

Hebu turudi nyuma tena katika historia.

Mwaka 135 CE ambapo Warumi waliwaondoa Wayahudi katika mji wa Jerusalem na kubadili jina kutoka Yudea (Judea) kuwa Palaestina. Hili ni jina la Kigiriki lililolenga kuondoa muungano wowote walionao Wayahdi kwenye eneo hilo. Wayahudi wote walipigwa marufuku kukanyaga Jerusalem.

Baada ya kuondolewa Yudea, Wayahudi walisambaa katika maeneo mbalimbali yaliyokuwa chini ya utawala wa Kirumi, Ulaya ya leo. Lakini walishambuliwa kila sehemu walipoenda.

Katika karne ya 11, Wayahudi waliuawa na wapigania Kristo (Crusaders) kwa kigezo kwamba wao ndio walimuua Yesu. Kwenye karne ya 14, Wayahudi waliuawa kwa madai kwamba wao ndio chanzo cha vifo vinavyojulikana kama black death. Walituhumiwa kwa kubadili mahubiri ya Yesu na kushambilia majeshi ya Warumi.

Wayahudi waliendelea kushambuliwa mpaka karne ya 19 ambapo baadhi ya Wahudi waliunganisha nguvu ili kulinda chimbuko lao. Walianzisha kitu kinachojulikana kama Zionism. Hii ilikuwa itikadi ya kisiasa, na kidini ambayo ililenga mambo mawili.

  • Ililenga kuzuia Wayahudi kushambuliwa
  • Ililenga kuwarudisha Wayahudi Jerusalem
Wazionist waliamini kwamba Uyahudi sio tu kwamba ni dhehebu, bali ni utaifa. Walidai kwamba Wayahudi hawanabudi kuwa na taifa kama ilivyo kwa Wafaransa walivyo na taifa la Ufaransa. Harakati hizi ndizo ziliwarudisha Israel. Leo hii itikadi ya Zionism ni itikadi ya taifa la Israel.

Kufikia mwisho wa karne ya 19, harakati hizi zilisababisha Wayahudi wengi kwa makundi kuhamia Palestina. Kufikia mwaka 1903, kiasi cha Wayahudi 30,000 walikuwa tayari wameweka makazi yao Palestina. Kufikia mwaka 1914, kulikuwa kuna ongezeko la Wayahudi wengine 40,000.

Hapa sasa ndipo Vita ya kwanza ya dunia ikaanza. Dola ya Ottoman ikaanguka, huku Waingereza na Wafaransa wakiyatawala makoloni ya Asia. Palestina ikawa chini ya Waingereza.

Mwanzoni, Waingereza waliruhusu Wayahudi kuendelea kuhamia Palestina. Lakini, kadri Wayahudi walivyoongezeka mvutano baina ya Waarabu na Wayahudi nao ukaongezeka. Pande zote zilishambuliana huku kila upande ukidai unaonewa. Hivyo, kufikia mwaka 1930, Waingereza walianza kudhibiti Wayahudi kuhamia Palestina.

Kuibuka kwa Nazi – Ujerumani

Mambo yalibadilika tena baada ya kuibuka kwa itikadi ya Nazi. Inakadiliwa kwamba Wayahudi milioni 6 waliuawa. Waliosalia walikimbilia Marekani na Palestina kwa idadi kubwa. Kufikia mwaka 1944, idadi ya Wayahudi wanaoishi Palestina ilifika 33% ya wakazi wote. Hii ilisababisha nchi za magharibi kuanza kuunga mkono kuundwa kwa taifa la Wayahudi. Lakini nchi nyingi za Kiarabu hazikutaka jambo hili litokee.

Mwaka 1947, uadui baina ya Wayahudi na Waarabu uliongezeka. Umoja wa Mataifa ulipitisha mpango wa kuigawa Palestina katika nchi mbili. Moja iwe ya Wayahdi na iitwe Israel na nyingine ibaki kwa ajili ya Waarabu, Palestina. Ambapo Israel iwe na ukubwa wa 56.5% la eneo lote huku Palestina ikibaki na 43.5% ya eneo.

Katiak azimio hilo, mji wa Jerusalem ulipaswa kubaki kuwa eneo la kimataifa kwa kuwa madhehebu yote yanalichukulia kama eneo takatifu. Mpango huu ulishindwa kabisa kufanikiwa.

Waingereza walishindwa kuzuia machafuko, hivyo kujiondoa kabisa na kuwaachia wahusika wadundane wenyewe. Wao waliondoka wakiacha machafuko nyuma. Wayahudi wao walikubaliana na mpango wa Umoja wa Mataifa.

Tarehe 14 Mei, 1948 Wayahudi walidai uhuru wa taifa lao na kuunda taifa lao la Israel. Wapalestina waliona jamb hili ni wizi, na Wayahudi wamewaibia eneo lao. Basi kilichofuata ni migogoro na uadui baina ya Wayahudi na waarabu.

Kwa Zaidi ya miaka 70, wamepigana zidi ya vita 8 zilizo rasmi huku mashambulizi madogo madogo ambayo hayana idadi.

Katika vita hizi na migogoro hizi, Israel aliendelea kujinyakulia maeneo ya Palestina.

Hii ni ramani ya Israel na Palestina mwaka 1947.

before.JPG

Hii ni ramani ya Israel na Palestina mwaka 1948, baada ya vita ya Israel dhidi ya Waarabu

baada 2.JPG
Ahsante kwa historia nzuri ila rekebisha hapa.Mtume Muhamad hakupaa kwenda mbinguni alikufa kifo cha kawaida na ndio maana kaburi lake liko hadi leo
 
Sijakosea mkuu. Kwa imani ya Kiislamu Mtume Mohamad SW aliwahi paa akaenda mbinguni na kutembezwa kila mahali, ilibaki akutane na Mungu. Baada ya hapo akarudi duniani. Inaitwa safari ya Miraji. Sina hakika kama spelling nimepatia
 
Inawezekana kuutatua ama kuujadiri huo mgogoro bila kuhusisha dini na jamii za kale za eneo hilo.

Kama inawezekana basi kati ya hao wahuni wa kipalestina na waisrael feki, kat yao hakuna atakate stahil ilo eneo, maana kihistoria na shahidi za kisayansi hakuna ushahid wa uwepo wa hao wakina ibrahim na yakob, zaid izo stori za wahusika wa kutungwa utazipata ktk vitabu vya hizi dini3.

Historia ya kwel inaprove mtu aliyestahil kuishi eneo ilo n mtu mweus ambaye nae alihama eneo hilo na baadae kuja kukaliwa na mwarabu.

Hata hivyo ilo eneo ni kufuru kulifananisha na ile israel ya vitabu vya dini, maana ile ilikuwa taifa kubwa kieneo, taifa lenye resources nyingi kuanzia madini, mimea mpaka wanyama na udongo mzuri kwa kilimo, leo hii uje useme ilo eneo lenye jangwa na udongo wenye mchanga usiosupport mazao mpka kubust kwa mambolea ndio taifa lile la wale wana wa Mungu?

Nonsense kabisa, mtu mweusi kushabikia huo ugomv bila ya kutumia akili, utapoteza muda wako bure na kuonekana mpumbav na mvivu wa kufikiri, enyi wajinga someni vizuri muache kuwa bendera fuata upepo.

Hakuna umiliki halali wa hiyo ardhi kwa mtu mweupe yeyote yule, maana urithi wa kwel ulikuwa chini ya mababu wa watu weusi kabla ya ujio wa hawa wahuni na wazushiView attachment 2204264
Hao watu weusi walikuwa ni watu gani na walienda wapi.
 
Israel ilipoteza ardhi yake mara mbili pale walipopelekwa uhamishoni na ndipo wahamiaji kama wapalestina walipochukua mwanya huo kukalia hilo eneo.

Hiyo ni kwa mujibu wa maandiko ambayo yanatuambia hiyo ardhi walipewa na Mungu na ndio maana hata mababu zao walizikwa hapo.

Wakati waisraeli wakiishi hapo kabla ya kupelekwa uhamishoni Babeli hao wapalestina walikuwa wapi?
Wakati "wanapewa"hiyo ardhi... ilikuwa tupu haina watu wanaoishi?
 
Back
Top Bottom