Mmiliki halali wa Jerusalem

Mmiliki halali wa Jerusalem

Hawakuuawa wote bana. Acha uongo. Ndo kisa cha Mungu kuchukia juu ya Joshua. Hivyo pale sio kwao
Waliobaki ni wafilisti na walikuwa Gaza tu na wala sio ukingo wa magharibi wa mto Jordan wala Jerusalem.
 
Sijakosea mkuu. Kwa imani ya Kiislamu Mtume Mohamad SW aliwahi paa akaenda mbinguni na kutembezwa kila mahali, ilibaki akutane na Mungu. Baada ya hapo akarudi duniani. Inaitwa safari ya Miraji. Sina hakika kama spelling nimepatia
mkuu ahsante hebu ngoja na mimi nitatafiti hii habari ya Miraji
 
Wakati "wanapewa"hiyo ardhi... ilikuwa tupu haina watu wanaoishi?
Watu walikuwepo na tena walianza na Mji wa Yeriko maana ulikuwa na ukuta mgumu,tena Yoshua aliwaambia ueni kila mtu hadi watoto(hapa alihofia kuwa hao watoto wakikua watakuja kuanzisha vita juu ya ardhi yao).
Kumbuka kuwa walivuka Mto Jordan na kuanza na Mji wa Yeriko
 
Tatizo moja la eneo hilo ni mipaka ya asili haikufuatwa,ukiangalia ramani ya sasa,Mji wa Yerusalem umepitiwa na mpaka wa Palestina na Israel,kingine sijui kwa nini Israel iliamua kukubali baadhi ya miji yake ya aslli kuwa chini ya Palestina,kwa mfano Yeriko,Hebron na Bethlehem...Ukiangalia mji wa Hebron ni mji ambao Mfalme Daudi wakati anaanza kutawala alianzia Hebron ambako alikaa miaka 7 na miezi 6 ndipo akahamia Yerusalem lakin leo mji huu uko chini ya utawala wa Palestina. Pia Bethlehem kapewa Palestina,huu mji unajulikana wazi kuwa ndio aliozaliwa Mfalme Daudi pia na "MASIHI" .Kwa hiyo Wakristo wanapoenda wakati wa X-mas huwa lazima waruhusiwe na Mamlaka ya Palestina na huwa miaka yote huwa wanaenda kasoro X-mas ya mwaka jana hawakwenda kutokana na vita inayoendelea.
 
Nikukosoe
1. Wakristo wanaamini Isaack ni mtoto wa kwanza wa Ibrahim .
Sio kweli, kama mkristo, hatuamini wala hakuna fundisho la kusema Isaka ni mtoto wa kwanza wa Ibrahim. Wala sio mtoto wa pekee wa ibrahim.
Isaka ni mtoto wa kwanza kwa Sara (mama wa taifa kubwa) na ndiye mtoto wa pekee wa AHADI toka kwa Mungu aliyewahidia Ibrahim na Sara.
2. Waislam wanaamini Ismael ni mtoto wa kwanza wa Ibrahim
HIi ni kwel ni mtoto wa Kwanza ,iko wazi hata katika bible. Anaebisha ana shida zake .
 
  • Thanks
Reactions: I M
Sijakosea mkuu. Kwa imani ya Kiislamu Mtume Mohamad SW aliwahi paa akaenda mbinguni na kutembezwa kila mahali, ilibaki akutane na Mungu. Baada ya hapo akarudi duniani. Inaitwa safari ya Miraji. Sina hakika kama spelling nimepatia
Ahsante kwa kunipa shule hebu ngoja nichimbe hii habari maana nashangaa kuna hadithi mtume mbinguni alipita nje jehanum akasikia kelele za wanawake akamuuliza MUNGU mbona wanawake ni wengi wanaopiga kelele? MUNGU akamjibu hawa viumbe duniani ndio watenda dhambi wakubwa.Na ndio waliomdanganya ADAM
 
Mkuu,bado unachimba tu!😂😂😂
 
Back
Top Bottom