TANZIA Mmiliki wa hoteli ya kitalii ya Snowcrest, William Mollel afariki

TANZIA Mmiliki wa hoteli ya kitalii ya Snowcrest, William Mollel afariki

Wengi tunatembea na magonjwa mengine hatarishi kama pressure,kisukari,unene uliopitikiza nk tujikite kuyatatua hayo manake ndio shida ipo hapo corona inaanza tu ila wamaliziaji tunao ndani yetu tayari!
 
Mzee Ombay alifariki? Mbona sikuiskia hii habari ya kifo chake aisee. Mzee alikua poa sana nimefanya nae sana biashara 3 years back pale karatu na nimefikia sana kwenye hotel zake pale karatu mpaka nikang'oa dem wa kijerumani.Amefanya mambo makubwa sana huyu mzee pale karatu niliacha anamalizia mghorofa wake pale pembeni ya exim bnk ndo sikurudi tena since 2017. RIP mzee Ombay
 
chenyewe kikija kimekuja.

Acha kupotosha watu hapa. Kifo hakina tahadhari? Nenda basi kakatishe barabara bila tahadhari hutakufa. Fanya zinaa bila tahadhari kwani huwezi kufa. Katisha maeneo yenye vibaka usiku bila tahadhari hamna neno.
Kama ukinisoma kuelewa hukuna haja ya kusema naandika ili kupotosha hoja yangu imejikita hasa hapo nilipoji-quote,kwani huyu tunayeambiwa hapa amekufa ali-act yote uliyoorodhesha hapa?

Si amekufa tu akiwa ametulia?kama ni nyumbani au hospital hatujaambiwa amekatisha barabara akagongwa na gari au amepita vichochoroni vibaka wakamvamia.

Uliyoorodhesha hapa yanachangia %0.01 ya vifo vyote duniani ila vingi vinatokana na asili ya uumbaji na hajatokea bado wa kubishana na hili.
 
RIP Mollel

Wito wangu kwa baadhi ya Wafuasi wa Chadema, haipendezi kuombeana vifo, sisi sote ni watanzania na wanaofariki ni Watanzania wenzetu yaani ndugu zetu, majirani na jamaa zetu

Hvyo si busara kila mara kupost taarifa zenye viasharia vya kushabikia vifo au kuombea vifo kwa Watanzania wenzetu,,, tukumbuke tu SISI SOTE NI NDUGU

Wito kwa wana CCM: msingefurahia kwa Lissu kushambuliwa na kufurahia police kuzuia watu wasiende kumuombea lissu.
 
RIP Mollel

Wito wangu kwa baadhi ya Wafuasi wa Chadema, haipendezi kuombeana vifo, sisi sote ni watanzania na wanaofariki ni Watanzania wenzetu yaani ndugu zetu, majirani na jamaa zetu

Hvyo si busara kila mara kupost taarifa zenye viasharia vya kushabikia vifo au kuombea vifo kwa Watanzania wenzetu,,, tukumbuke tu SISI SOTE NI NDUGU
Ila Watanzania Mungu ameruhusu tufungwe akili!
Yaani kwa akili zako Cdm ndiyo inayowaombea kwa Mungu kifo Watanzania!.

Tatizo ni nini! Corona ipo na inakula vichwa, wewe singizia Cdm [emoji107]
 
Kama ukinisoma kuelewa hukuna haja ya kusema naandika ili kupotosha hoja yangu imejikita hasa hapo nilipoji-quote,kwani huyu tunayeambiwa hapa amekufa ali-act yote uliyoorodhesha hapa?si amekufa tu akiwa ametulia?kama ni nyumbani au hospital hatujaambiwa amekatisha barabara akagongwa na gari au amepita vichochoroni vibaka wakamvamia.

Uliyoorodhesha hapa yanachangia %0.01 ya vifo vyote duniani ila vingi vinatokana na asili ya uumbaji na hajatokea bado wa kubishana na hili.
Sikubaliani na wewe kabisa. Kwenye maisha tahadhari ni muhimu sana sana. Huwezi kuishi kwa tahadhari eti ka sababu hata ukichukuwa utakufa tu. Hivi unajua hata kula balanced diet ni kuchukua tahadhari? Unajua kufanya mazoezi ni kuchukuwa tahadhari? Unajua kwenda hospital unapoumwa ni kuchukuwa tahadhari? Unajua kujikinga na neti ni kuchukuwa tahadhari? Ndugu yangu hujasoma mahesabu ya probability nini?
 
Poleni sana, huo ukanda wengi wametutoka, sijui tunatofautiana maumbile! Huku nilipo wengi washakata kutokana na 👉🏽CVD19....Be careful, usipende kuzurura na kukaa katika mikusanyiko.
 
Akizungumza na mwananchi Mpwa wa mfanyanyabiasha huyo,Lemburis Sirikwa amesema Mollel amefariki Jana.

"Ni kweli Mollel ambaye ni mtoto wa dada yangu amefariki Jana baada ya kuugua kwa muda mfupi na taratibu za mazishi zinaendelea"
Yaani haki ya nani Tanzania tumebski na wandishi wa habari Taletale! Yaani Kaka wa mama yako ni Mpwa? Mungu wangu!
 
Sikubaliani na wewe kabisa. Kwenye maisha tahadhari ni muhimu sana sana. Huwezi kuishi kwa tahadhari eti ka sababu hata ukichukuwa utakufa tu. Hivi unajua hata kula balanced diet ni kuchukua tahadhari? Unajua kufanya mazoezi ni kuchukuwa tahadhari? Unajua kwenda hospital unapoumwa ni kuchukuwa tahadhari? Unajua kujikinga na neti ni kuchukuwa tahadhari? Ndugu yangu hujasoma mahesabu ya probability nini?

Brother!

Ikiwa unaamini wote wanaokufa hawachukui tahadhari yoyote hata kufikia vifo kuwakuta basi point tatu zote chukua wewe.tuna uelewa tofauti,mtu achukue tahadhari asichukue tahadhari(kujipatisha ajali etc) still wote wanakufa,hapa ndipo penye point yangu.
 
Arusha. Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha ambaye pia ni mmiliki wa hoteli kadhaa za kitalii , ikiwepo Snow crest , William Mollel amefariki Dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Akizungumza na mwananchi Mpwa wa mfanyanyabiasha huyo,Lemburis Sirikwa amesema Mollel amefariki Jana.

"Ni kweli Mollel ambaye ni mtoto wa dada yangu amefariki Jana baada ya kuugua kwa muda mfupi na taratibu za mazishi zinaendelea"

Amesema Mollel ambaye alikuwa akifanya biashara kadhaa ikiwepo ya kuendesha hoteli za kitalii ameacha watoto watatu.

Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara ,Viwanda na Kilimo(TCCIA) Mkoa Arusha Walter Maeda alieleza pia kusikitishwa na kifo cha mfanyabiashara huyo.

Mollel alinunuwa hoteli hiyo, mwaka 2014 kutoka kwa mfanyabiashara Wilfred Tarimo, hata hivyo aliingia katika mgogoro wa kushindwa kuendesha hoteli kwa ufanisini kutokana na kurithi madeni mengi ya wazabuni na wafanyakazi.
Kwa mara ya mwisho kuzungumza na mwananchi kabla ya kifo chake alisema alinunua hoteli hiyo kwa mkopo wa dola 8 milioni kutoka benki ya PTA na na standard chartered.

"Nilitegemea baada ya kupata mkopo wa kununua hoteli hii niifanye ya kimataifa na kuunganisha na mtandao wa hoteli kubwa duniani''alisema.
Kifo cha Mollel kimetokea takribani mwezi miwili tangu kifo Jacob Ombay mmiliki mwingine wa hoteli nane za kitalii.

Ombay alikuwa anamiliki hoteli za Bougainvillea safari lodge, country lodge karatu,Ngorongoro coffee lodge, lake Eyasi safari lodge,Sangaiwe tented lodge, Thorn tree camp,Hippo Traill camp.
Katibu mtendaji wa chama cha mawakala wa utalii nchini-(TATO) Sirili Akko amesema vifo vya wafanyabiashara hao ni pigo Kwa sekta ya Utalii.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
Scow crest Magufuli alivunja ile front line, ikakosa parking na ndio ikawa mwisho wake.
 
Back
Top Bottom