NAONA Watanzania Wanajisahau pia. Nchi hii ni CAPITALISM.. Ni hivi Mwenye nacho atakuwa nacho na Ataongezewa zaidi ila Asiyekuwa nacho hata Kile Kidogo alichodhani kuwa anacho kitachukuliwa
Kwahiyo Mtanzania jitahidi kadri uwezavyo kutafuta mali maana usipokuwa nazo Wenye nazo watakutesa sana Katika Haya maisha na Ukizipata Jitahidi kuzilimbikiza,
Hii ni lugha ngumu ambayo ni chungu lakini ndio ukweli, tukifanya masikhara tutaendelea kuita watu wezi na mafisadi.
Parachichi pale Njombe walikuja Wakenya wakawa wananunua na kuexport kupitia Kenya kama brand ya Kenya, wamepiga hela sana.
Watalii walishukia JKIA wakaja Serengeti kutokea Kenya na kuondokea Kenya huku wakiamini Mt Kilimanjaro upo Kenya.
Tuna mapoli mengi sana lakini wakulima waliowengi wanalimba nusu au robo ela, watu wenye mitaji ya kulima kibepari wako mjini wanamiliki lodge na mabaa.
Hawa Matajiri akina Mo, RA, Manji, GSM nk babu zao walipokuja Tanzania walikwenda kuishi mapolini huko, Leo wajukuu zao ndio matajiri mjini, na vizazi vyao vitaendelea kuwa matajiri maana wanakuta mifumo tayari ipo sawa.
Bila kuandaa misingi ya generation yako basi kila siku itakuwa ni kufukuza mwenge tu.
Aliyezaliwa kwenye utajiri mkubwa ana uwezekano mkubwa wa kuwa tajiri Vs aliyezaliwa kwenye familia yenye ufukara.
safarini Hodeidah Yemen.