Mmiliki wa ITV na Mfanyabiashara REGINALD MENGI aliwahi kutaja kundi Mtandao la Mafisadi 5 Bora na ROSTAM AZIZI akiwemo kama Fisadi

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Aliyekuwa Mmiliki wa ITV, Radio One and Capital TV na Capital Radio aliwai kuwataja mafisadi 10 nchini, huku ROSTAM AZIZI akishika kwenye 5 bora ya mafisadi nchini. Hii ni video enzi za kikwete kabla ya Magufuli hajawai Rais... na Hawa mafisadi ndio kundi mtandao alilokuwa anazungumzia Humphrey Polepole, hivyo basi maneno ya Humphrey Polepole msiyachukulie kwa mzaha. Ukisikiliza vizuri utagundua hawa mafisadi wengi wao majina yao ni watu wa asili ya nchi za kigeni. Hawana uchungu na nchi, wanashirikiana na watanzania wachache wenye ushawishi au nguvu kuchuma mali za taifa
Your browser is not able to display this video.
 
Hawa ni Kingmakers wanaaumua nani awe Raisi Tanzania na nani afie Lupango kama sio kula udongo.
 
Naombeni kujua wanamitandao maana yake ni nini na kazi yao ni nini hasa? ( ccm mtandao)
 
NAONA Watanzania Wanajisahau pia. Nchi hii ni CAPITALISM.. Ni hivi Mwenye nacho atakuwa nacho na Ataongezewa zaidi ila Asiyekuwa nacho hata Kile Kidogo alichodhani kuwa anacho kitachukuliwa

Kwahiyo Mtanzania jitahidi kadri uwezavyo kutafuta mali maana usipokuwa nazo Wenye nazo watakutesa sana Katika Haya maisha na Ukizipata Jitahidi kuzilimbikiza,
 
Naombeni kujua wanamitandao maana yake ni nini na kazi yao ni nini hasa? ( ccm mtandao)
Mfatilie ndugu slowslow kwa makini sana mzee wa subtitle
 
Naombeni kujua wanamitandao maana yake ni nini na kazi yao ni nini hasa? ( ccm mtandao)
Wana mtandao ni "Network Group" yani sio mtu mmoja pekee, bali ni kundi la watu linalosuka mipango
 
walikua na matatizo binafsi baina yao kwa kumbukumbu zangu, akatumia fursa kumchafua. Unatajaje mafisadi kwa wakati huo bila ya kuwataja kikwete na lowassa?
 
walikua na matatizo binafsi baina yao kwa kumbukumbu zangu, akatumia fursa kumchafua. Unatajaje mafisadi kwa wakati huo bila ya kuwataja kikwete na lowassa?
Kikwete alikuwa Rais muda huo na Lowasa waziri mkuu... uwezi kuwashitumu wakuu wa nchi unless unataka biashara zako ziyumbe ukose msaada... hakuna mfanyabiashara anayewekaga ligi na viongozi wakuu wa nchi.... Dangote mwenyewe pale Nigeria anakuwaga na heshima na mpole mbele ya Rais

Kwa Mengi ilikuwa Rais kuwataja hao wengine kwa sababu sio viongozi wakuu wa nchi.... ukisikia kasema wapo mafisadi 10, ila kaishia kuwataja Wahindi na waarabu tu, hao watano ambao hawakutajwa unaweza kuta ni vigogo serikalini
 
Nani kasema ukiwa CAPITALISM unaruhusiwa kuhujumu uchumi, ufisadi, utekaji na sasa hivi ufiraji ,mambo hayo hatuyaoni nchi ambako mfumo wa ubepari umeanza
 

Hii ni lugha ngumu ambayo ni chungu lakini ndio ukweli, tukifanya masikhara tutaendelea kuita watu wezi na mafisadi.

Parachichi pale Njombe walikuja Wakenya wakawa wananunua na kuexport kupitia Kenya kama brand ya Kenya, wamepiga hela sana.
Watalii walishukia JKIA wakaja Serengeti kutokea Kenya na kuondokea Kenya huku wakiamini Mt Kilimanjaro upo Kenya.

Tuna mapoli mengi sana lakini wakulima waliowengi wanalimba nusu au robo ela, watu wenye mitaji ya kulima kibepari wako mjini wanamiliki lodge na mabaa.

Hawa Matajiri akina Mo, RA, Manji, GSM nk babu zao walipokuja Tanzania walikwenda kuishi mapolini huko, Leo wajukuu zao ndio matajiri mjini, na vizazi vyao vitaendelea kuwa matajiri maana wanakuta mifumo tayari ipo sawa.

Bila kuandaa misingi ya generation yako basi kila siku itakuwa ni kufukuza mwenge tu.
Aliyezaliwa kwenye utajiri mkubwa ana uwezekano mkubwa wa kuwa tajiri Vs aliyezaliwa kwenye familia yenye ufukara.

safarini Hodeidah Yemen.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…