Mmiliki wa JamiiForums awajibu wanaosema anatumiwa na mabeberu, baada ya kuitwa ikulu Marekani

Mmiliki wa JamiiForums awajibu wanaosema anatumiwa na mabeberu, baada ya kuitwa ikulu Marekani

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
December 16, 2019

Mwanzilishi wa JamiiForums akizungumzia kuhusu tuzo aliyopewa hivi karibuni na jinsi mtandao huu unavyokabiliana na hali ngumu ya kutenda kazi hasahasa tukiangazia mazingira ya sasa Tanzania.

Hofu inajengwana na waandishi wenyewe lakini kama mitandao inafuata sheria na kanuni za uandishi bora basi changamoto zilizopo huwa zinaweza kukabiliwa bila hofu.

Anabainisha changamoto za waandishi wa habari wa nchi za Nicaragua huko Marekani ya Kusini, India na Pakistan ambayo pia wamepata tuzo kama JamiiForums.

Video/picture caption inaonesha : Mazungumzo ya Makamu wa Rais wa Marekani Mh. Mike Pence, alipokutana na Maxence Melo kama mwakilishi wa mtandao maarufu na mkubwa wa JamiiForums toka Tanzania.

80B9F004-CBF1-4385-AC60-F35CDE9AFD54.jpeg




Sources: DW Swahili Kipindi Kinagaubaga : ABC Habari
Michael Richard Pence is an American politician and lawyer serving as the 48th vice president of the United States. He previously was the 50th governor of Indiana from 2013 to 2017 and a member of the United States House of Representatives from 2001 to 2013. He is the younger brother of U.S. representative Greg Pence.
 
Eeeenh. Maxence, kweli umepewa ujiko.

Hali isingekuwa kama ilivyo sasa hapa nyumbani, ni nani angehangaika na uwepo wa akina Max. duniani!

Heko mkuu. Hii ni alama isiyoweza futika maishani.


Hakika wimbo wa 'mabeberu' sasa utakuandama kama beji ya heshima.

Just do the right thing and leave the rest of the stuff sort itself out.
 
Huyo Musiba anayesifiwa na watawala kuwa ndiye mwandishi bora na mwenye uzalendo wa hali ya juu, mbona hatujamsikia naye kupokea zawadi hiyo??
Hawawezi mpa yeye kama yuko upande wa serikali. Wewe kwa akili yako unafikiri Mike Pence anaweza jua shughuli za Maxence Melo wa Tanzania kweli? Inawezekana hata Magufuli Rais wa Tanzania asimjue sembuse Maxence Melo? Nyie watanzania chezeni tu na wazungu.

Nakuomba utambue mzungu hawezi kuwa rafiki yako hata mara moja. Na hata ukioa au kuolewa na mzungu na mkazaa hata na watoto, usifikiri kuwa wewe utathaminika kama wao wenyewe kwa wenyewe.

Hawa watu wa NGOs na Amnesty International ndiyo wanao wachomekea hawa watu kwenye makadamnasha kama hayo kwa lengo la kuwaghiribu akili na kuwajaza mambo ya uwongo ili waendelee kuleta wasi wasi na vurugu kwenye mataifa machanga kama yetu yanayo jitahidi kujikomboa kiuchumi ili kuleta maendeleo yao.

Wazungu hawapendi mataifa ambayo viongozi wao wanakuwa smart juu ya maisha na maendeleo ya watu wake. Wanataka kutuona sisi tukiwa inferor na wao wanaendelea kuwa juu ili wapone. Kwanini hakupewa hiyo tuzo awamu ya nne? Awamu ya nne Jamii Forum so ilikuwepo pia?

Na ndiyo maana ukimsikiliza Maxence Melo mwenyewe anavyo hojiana na mtangazaji wa habari wa DW utaona kuwa mazungumzo yao yali base kwenye maswala yanayo husu changamoto zinazo wakabili majournalist tu kwenye nchi zao, hawaja gusia chochote kile kinacho husu mafanikio ya nchi yetu na juhudi zake katika kujikomboa kiuchumi na changamoto ambazo Rais anazipata katika kukomesha rusha.

Nilicheka sana Maxence Melo aliposema eti Mike Pence anaijua vizuri Tanzania. Angeijua vizuri Tanzania sidhani kama angekubali kutoa tuzo kwake na sio kwa Rais ambaye anafanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo ya watanzania kwa kutumia fedha zetu kuanzisha miradi ambayo inawasaidia wananchi kupata ajira na kuendesha maisha ya familia zao. Si ndiyo lengo lao wanalopigania kila siku?

Hapo ndipo utapo ona jinsi gani watu kama akina Maxence Melo na wengineo wanavyo kuwa manipulated na kutumiwa kirahisi kupotosha ukweli unao tokea nchini kwa maslahi yao wazungu. Lakini wenyewe nasikitika hawajitambui kwa sababu ni malimbukeni wa wazungu. Unajua kama mtu hajawahi ishi na kukua pamoja na wazungu ina kuwa shida sana kuwajua walivyo.

Mtu anaye wajua wazungu hawezi akalaghaiwa kirahisi namna hiyo. Kwanza angeliuliza hilo shirika la ulinzi wa wahandishi wa habari duniani, CPJ, kwa nini yeye? Mbona waamerika wenyewe wanamsaka Edward Snowden na kumtaka Julian Assange ambaye yuko Uingereza apelekwe Amerika kujibu mashtaka zidi ya serikali yao kwa kutoa siri za activities za serikali ya Amerika juu ya wafungwa wa Islamic Fundamentalists huko Guantanamo Cuba?

Mbona huyo Maxence Melo kama yeye ni Journalist anaye pigania haki za binadamu na freedom of press mbona hakumwuuliza huyo Vice President wa Amerka Mike Pence juu ya usalama wa hao ma journalist wawili?

Zaid ya hayo wao ina wahusu nini kufungua Plattform Tanzania? Mbona kwao kuna waamerika kibao wenye Plattforms kama hizo na husikii wakurugenzi wao wakialikwa States Hous kwa tuzo?

Jiulize sasa kwa nini JF la Tanzania?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maneno Meier,

Mkuu mbona unateseka hivyo, Mh. Makamu wa Rais wa USA mpaka anapeana mikono na Maxence Mello wa JamiiForums pamoja na shughuli zake nyingi kama msaidizi wa Donald Trump, lazima kabla ya kuwakaribisha Ikulu ya White House alipewa taarifa juu ya ukubwa na ushawishi wa JamiiForums.

Hivyo Mh. Makamu Wa Rais wa Marekani Mike Pence kukutana na Mkuu wa JamiiForums, alijisikia faraja kuona kuna waTanzania wengi watu-huru wanaotumia jukwaa la mtandao huu kupeana taarifa mbalimbali.

Na kutokana na ukubwa wa JamiiForums kila taifa kubwa duniani linataka kujua kinachoendelea humu JamiiForums kama ilivyo kwa Afisi za Mtaa wa Lumumba na Serikali yake ya Awamu ya 5 inayoshinda humu kujua kinachoendelea ndani ya fikra za watu-huru.
 
Maneno Meier, Zamani kipindi teknolojia haijakuwa watz waliuliwa sana na watawala kimya kimya sababu za kisiasa bila ya kuonekana, lakin saiv teknolojia imekuwa ule mwanya wa kuuwa na kukandamiza binaadam mwenzenu haupo japo bado mnaendelea na huo mchezo ndio maana melo anapata tuzo kwa kukubali kuruhusu watu watoe mawazo yao kwa uhuru,si unajua mkuu wa malaika alisema anatamani malaika wake washuke wazime mitando ili amwage damu kwa nafasi asionekane na nasikia juzi tu mlijitoa kwenye mahakama za africa ili msijadiliwe kipindi mtakapo kuwa mshamwaga damu za binaadam wasio na hatia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru kuwepo JF, ni faraja na furaha kwangu ni platform niliyokuwa naiwaza mda mrefu sana, hatimaye nimefanikisha kuwepo jukwaani. Hongera sana Max mello

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom