Mmiliki wa M-bet ni nani?

Mmiliki wa M-bet ni nani?

Nihaomedia7

Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
32
Reaction score
77
Kuna jamaa anaenezeza uvumi kuwa mmiliki wa kampuni ya M-bet ni Mtanzania, kwanza nimwambie tu mtaji wa kuanzisha kampuni ya kubeti sio wakitoto ambao watanzania wanaweza kumudu. Sembuse Mtanzania amiliki kampuni ya beti inayofanya kazi Tanzania, Kenya, Uganda, Zambia, na Kongo?

Au anachukulia wasafi beti? Wasafi beti kwa taarifa yako no partnership ya kampuni ya Odibet yakenya (my intention kumiliki kampuni ya betting sio Jambo rahisi kuwa kila mtu anaweza kufanya hii biashara inahitaji pesa ndefu) kufungua kiduka Cha kubeti pekee inahitaji sio chini ya MILIONI 20 ambapo utapata gawio la faida ya 40% mpaka 50

Anyway kampuni ya M-bet group inamilikiwa na Dhiresh Kaba na ndipo wakongwe wa betting utasikia wanatamka mhindi mhindi
 
Ndio huyu jamaa ana iliko kiwanda cha kutengeneza Tomato sources na Chili source?
 
Umetoa point za kitoto sana, eti hakuna Mtanzania anaweza kuanzisha kampuni ya kubet ikawa nchi za Africa mashariki na zaidi. Sema Watanzania hawana kipaumbele Cha kuwekeza kwenye kamali. Mtu kama Abbas Tarimba anaweza kuwa na ela za kuanzia kampuni ya kubet ikawa hata nchi zote za Africa.

Nimekupa mfano mdogo sana, kama huna ela ya kufanya kitu fulani sema sina ela ila usiongelee jamii fulani. Watu wanamiliki magari ya mizigo (trucks) au malori ya mafuta zaidi ya 100, au vituo vya mafuta (petrol stations) zaidi ya 50, washindwe kufungua kampuni ya kubet ya kuenea nchi 10?

Hapo naongelea watu wa chini, achana na akina Azam na Rostam. Kuna Mtanzania anaishi uingereza ni mzaliwa wa Singida, anamiliki meli za mafuta, umeshawahi kumsikia? Usiwe unaongea vitu Kwa ujumla kama huna data za kutosha.
 
Mie nadhani kampuni ya kubeti ndio kampuni rahisi zaidi kuanzisha. Kwa sababu unachotakiwa kuwa nacho ni kuwa website na wapi utatangaza.

Kinachofuata ni kupiga debe. Watu 500,000 wanatoa 1000 yao inakuwa 500,000,000 halafu unchagua mmoja wa kumpa 10,000,000 kila wiki na wengine wa kuwapa 100,000 kila siku.

Zinazobaki mnagawana na serikali. Kwa kuwa serikali haijui ujanja ujanja unabaki na 95%. Hata mke wa Mwigulu anayo. Karibu redio na tv zote zina makampuni ya kubeti kwa sasa.
 
Wewe ndio umeongea utumbo kabisa
Kwahiyo na wewe unaamini watanzania hawana ela za kuwekeza kwenye kamali!?.., kwamba ni ela nyingi zinatakiwa ambazo wabongo hawana kama anavyodai mleta mada!??, Kweli vituko havitakaa viishe.., sema wabongo sio ma risk taker wazuri. Wamiliki wa kampuni za kubet wote ni watu wa ku risk sana.
 
Bado na wewe hujajibu ...huyo mhindi ni raia wa nchi gani?
 
Mie nadhani kampuni ya kubeti ndio kampuni rahisi zaidi kuanzisha. Kwa sababu unachotakiwa kuwa nacho ni kuwa website na wapi utatangaza. Kinachofuata ni kupiga debe. Watu 500,000 wanatoa 1000 yao inakuwa 500,000,000 halafu unchagua mmoja wa kumpa 10,000,000 kila wiki na wengine wa kuwapa 100,000 kila siku.
Zinazobaki mnagawana na serikali. Kwa kuwa serikali haijui ujanja ujanja unabaki na 95%. Hata mke wa Mwigulu anayo. Karibu redio na tv zote zina makampuniya kubeti kwa sasa.
Mkuu huyu muanzisha thread anaongea vitu asivyojua. Alipotaja mil ioni 20 kama mfano nikajua viwango vya ela nyingi kichwani mwake vipo chini sana. Milioni 500 hadi bilioni 1 ya kitanzania inatosha sana kuanzisha kampuni ya kubet kubwa tu. Ambazo watu wengi wanazo tu.
 
Mie nadhani kampuni ya kubeti ndio kampuni rahisi zaidi kuanzisha. Kwa sababu unachotakiwa kuwa nacho ni kuwa website na wapi utatangaza. Kinachofuata ni kupiga debe...
Usichanganye betting na kamari nyinyine!
 
Nikiuza nyumba ya urithi wa mzee wangu kariakoo sikosi milioni 800 inatosha kabisa kufungua mdukuzi bet
 
Mkuu huyu muanzisha thread anaongea vitu asivyojua. Alipotaja mil ioni 20 kama mfano nikajua viwango vya ela nyingi kichwani mwake vipo chini sana. Milioni 500 hadi bilioni 1 ya kitanzania inatosha sana kuanzisha kampuni ya kubet kubwa tu. Ambazo watu wengi wanazo tu.
Unatumia nguvu nyingi sana broo humu jf kujibu nonsenses wakati watu wanatumia ID feki. Pengine mleta mada ni mwanao au mjuu wako upo nae hapo hapo sebuleni kwako.
 
Biashara ya betting hauijui ndio unasema milion 500 utaanzisha kampuni ya betting kubwa tu, kwanza kwa huu mtaji hupewi leseni ,, hii no stake ya watu 200 tu he wakishinda utawalipa Nini? kwa uchache kufungua akili yako biashara ya betting ni biashara namba 1 kuingiza mkwanja mrefu ikifuatiwa na MADAWA ya kulevya Kisha maudhui ya ngono , napia biashara hii inahitaji mtaji mkubwa sana ambao unamuweka reheni Yani muda wowote huu mtaji unaweza kuta au kudrop sana batting sio mtaji wa maandazi
Kama umesoma hesabu za probability,uwezekano wa kampuni ya kubet kufirisika haupo,wanaoliwa ni wengi kulliko wanaoshinda,ni desi fulani hivi
 
Usichanganye betting na kamari nyinyine!
Wewe unaongea nini!?.., betting ndo hiyohiyo kamali, betting ni English, kamali ni kiswahili neno jingine Kwa kiingereza ni gambling. Kama unamaanisha soka, hakuna kampuni inayobeti soka tu, zote Zina michezo yote. Kitendo Cha kuweka ela kwamba itashinda timu fulani, au mtu fulani au mnyama fulani(awe farasi, mbwa,etc) hata kama sio viumbe hai ni Virtual zote zinaitwa kamali kwenye kiswahili. Shule mlienda kusomea nini!?
 
Umetoa point za kitoto sana, eti hakuna mtanzania anaweza kuanzisha kampuni ya kubet ikawa nchi za Africa mashariki na zaidi. Sema watanzania hawana kipaumbele Cha kuwekeza kwenye kamali. Mtu kama Abbas Tarimba anaweza kuwa na ela za kuanzia kampuni ya kubet ikawa hata nchi zote za Africa. Nimekupa mfano mdogo sana, kama huna ela ya kufanya kitu fulani sema sina ela ila usiongelee jamii fulani. Watu wanamiliki magari ya mizigo (trucks) au malori ya mafuta zaidi ya 100, au vituo vya mafuta (petrol stations) zaidi ya 50 ,washindwe kufungua kampuni ya kubet ya kuenea nchi 10?, Hapo naongelea watu wa chini, achana na akina Azam na Rostam. Kuna mtanzania anaishi uingereza ni mzaliwa wa Singida, anamiliki meli za mafuta, umeshawahi kumsikia!??!?, Usiwe unaongea vitu Kwa ujumla kama huna data za kutosha.
Umetumia nguvu kubwa sana kumjibu,ungemuignore tu,anakuambia hakuna Mtanzania mwenye kuanzisha kampuni halafu hapo hapo anakuambia labda diamond!
 
Back
Top Bottom