Mmiliki wa mabasi ya Super Sami atoweka, gari lake lachomwa moto Serengeti

Mmiliki wa mabasi ya Super Sami atoweka, gari lake lachomwa moto Serengeti

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
IMG_20180309_120749_393.jpg
IMG_20180309_120730_648.jpg
28870378_2061738970509399_5210459689955317991_n.jpg

IMG_20180309_120712_304.jpg




Mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah ametoweka kwa zaidi wiki mbili sasa gari lake aina ya Nissan Patrol kukutwa likiwa limechomwa moto katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara.

Gari hilo lililokutwa likitumiwa na mfanyabiashara huyo ambaye ni mkazi wa Mwanza, lilikutwa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara jana likiwa limeteketea kwa moto.

Ofisi habari wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi (Taboa), Mustapha Mwalongo, aliiambia Nipashe kwa njia ya simu kuwa mfanyabiashara huyo licha ya gari lake kukutwa limeteketea moto, hawakukuta mabaki ya mwili wake.

"Gari lake limeteketea kweli lakini hatujabaini mwili kama na yeye alikuwa kwenye gari lile kwa sababu waliofika eneo la tukio hawajakuta mwili au mabaki ya mwili ya aina yeyote", alisema Mwalongo.

Alisema baada ya mmiliki huyo wa mabasi kutoweka tangu Machi Mosi, Kamati iliundwa ya kufuatilia sababu za kutoweka kwake na wapi alipo ambayo inashirikiana na familia.

"Kamati ilipopata taarifa kuwa kuna gari limeteketea kule Serengeti, walishirikiana na Jeshi la Polisi kwenda hadi eneo la tukio na kubaini kweli ni gari lake lakini hawajabaini kama alikuwepo mle wakati linachomwa", alisema Mwalongo.
 
Alikua kwenye mkakati wa kumsepesha twiga au niaje..?
 
Alikutwa akiwa ameunguzwa ndani ya gari au mwili umekutwa pembezoni mwa gari?
 
Duuuhhh itakuwa kati ya kisasi cha biashara au mambo ya kuchukuliana wanawake lazima.. Mmmmmhh
Inawezekana kuna watu wanataka kurithi mabasi kabla ya muda kufika, wakaona wamuwahishe, kama ana ndugu ndugu ambao wanaonekana viherehere kwenye hayo mabasi kuliko hata familia yake mwenyewe wachunguzwe hao ndugu. Pia washindani wa kibiashara wachunguzwe, pia vimada na waume wa vimada wote wachunguzwe
 
hizo 'zitakua'/huwenda dili tu hazikwenda kama walivyopanga ili zisibumbuluke ni lazima mmoja apotee na taarifa hatarishi dhidi ya wenzake
 
Back
Top Bottom