JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Matukio ya wanawake kuuawa kikatili na wapenzi au waume zao yameendelea kutikisa, baada ya mwanamke mmoja mmiliki wa saluni ya Madam Beauty Point iliyopo Sinza Jijini Dar es Salaam anayefahamika kwa jina la Leonia Julius, kudaiwa kuuawa kwa kunyongwa na mpenzi wake wakiwa hotelini.
Inadaiwa tukio hilo limetokea maeneo ya Tegete na tayari mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
Baadhi ya wafanyakazi na ndugu wa marehemu wamezungumza leo Jumapili Juni 19, 2022 na kusema ni kweli mwanamke huyo amefariki na inadaiwa wakati akiingia hotelini kamera zilizopo hotelini hapo zilinasa wakati wakiingia.
Chanzo: Global TV Online