Nyanswe Nsame
Senior Member
- Jul 9, 2019
- 165
- 181
Mmiliki wa The Cask Bar Mwanza afikishwa mahakamani, atimua mbio
Watu watatu wakiwemo raia wa kigeni wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza kwa tuhuma za kuingia nchini na kufanya kazi bila vibali.
Raia hao waliingia nchini na kuanza kufanya kazi bila ya kuwa na vibali kitendo ambacho ni kinyume na taratibu za nchi.
Watuhumiwa hao waliingia nchini kwa msaada wa mmiliki wa Baa maarufu jijini Mwanza ya The CASK iliyopo jengo la Rock City Mall, Joseph Charles Makanyaga.
Raia hao kutoka China wamefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza jana majira ya saa sita mchana.
Watuhumiwa hao, wamefahamika kwa majina ya Yong Chen na Jang Dewei na Joseph Charles Makanyaga.
Raia hao wa kigeni waliingia nchini kwa lengo la kuja kutembea lakini baada ya kufika walianza kufanya kazi katika kiwanda cha mwenyeji wao bwana Makanyaga.
Kiwanda walichokuwa wakifanya kazi watuhumiwa hao kipo Nyakato jijini Mwanza, kinachozalisha mabomba ya kusambaza maji.
Watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani kwa mjibu wa kifungu cha sheria namba 9 (2) ya mwaka 2015.
Kesi hiyo ilitajwa jana mahakamani hapo, imehairishwa na inatarajiwa kusikilizwa aprili 1 mwaka huu.
Kesi hiyo ipo chini ya hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana, Gwai Sumayi.
Watuhumiwa hao wakiongozwa na Makanyaga, mara baada ya kuachiwa kwa dhamana jana saa kumi jioni walitoka wakikimbia.
Pamoja na kutoka wanakimbia, walifunguliwa mlango wa nyuma na mmoja wa watumishi wa mahakama hiyo kwa lengo la kutokomea bila kupigwa picha na wanahabari.
Licha ya kupita mlango wa nyuma wa mahakama hiyo, bado waliwakuta wanahabari ambao waliendelea kuwapiga picha.
MWISHO